Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

nilianza na uji wa unga wa muhogo

nilikua naupika wa nazi siweki sukari wala chumvi

nambadiliahia naweka maziwa nikiweka maziwa nikawa naweka sukar kwa mbali na chumvi

nikajamsagia lishe, nauchanganya na maziwa anakumywa asubuh

mchana namsagia ndiz mbivu au nachanganya ndiz mbivu na parachichi sometimes chungwa nalikamua nampa

wakati mwengine namchemshia ndizi bukoba kwenye supu aidha yasamaki au nyama then nablend nachanganya na maziwa narudisha jikoni
vichemke kidogo naepua vikipoa nampa vikkwa vya uvuguvugu saa kum jion maziwa fresh baada ya hapo analinyonya tu ziwa la mama yake

pia hua napenda kumbadilishia badilishia sometimes nachemsha mchele has uive naepua naweka kwenye blender lakini namwaga maji badala ya kisaga na maji nasagia maziwa fresh narudisha kwenye sufuria naweka sukari kidogo narudisjha jikon vichemke pamoja

au

nachukua yai na ndizi bukoba nachemsha vikiwa tayari naepua namenya yai nachukua kiini na ndizinasaga pamoja na vijichumvi kwa mbaaali na maziwa kidogo nampa
 
Wangu ana miezi & anapenda sana mchanganyiko wa ndizi parachichi na embe.
Namsagia inakuwa smooth kwa blenda.
Uji nampa dona.nachanganya na maziwa,blubend,
Anapenda machungwa mno.
Kila siku nambadilishia smoothie ya matunda mchanganyiko ili asikinai.
Anaku ugali pia.
Alianza kuota meno na 4 morth
Sasa ana miezi 8,
Ana meno 6,
Anasimamia vitu na kuna mda mwingine anasimama dede mwenyewe
 
Wangu ana miezi saba.
Asubuhi anakula rojo la samaki mbichi+ maini siku moja moja+mboga ya majani iliosagwa/carrot
Mchana, ugali laini + mboga yoyote iliopo wakati huo
Jioni kiini cha yai la kienyeji+maziwa
Usiku kunyonya tu kwa mama ake.
 
Maziwa gan mkuu haya ya kopo ama
 
Wooow maskini
 
Toba!!! Mwezi 1 mlimuonea jamani mngekua mnampa maziwa ya kopo kama ya mama hayatoshi vipi kabla ya hapo mlimshauri dokta wake au mliamua wenyewe tu?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti tobaa
 
Kutayarisha na SIO
Kutaarisha!
Kiswahili fasaha.
Asante.
 
Lishe ya mtoto kwanzia miezi 6 na kuendelea,hata mtu mzima anaweza tumia pia.
1.Maindi lishe
2.Soya
3.Karanga/Korosho
4.Mbegu za maboga
5.Iriki
 
Waoohhh asante kwa somo
 
Kaka upo kimya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…