SoC03 Lishe na Magonjwa

SoC03 Lishe na Magonjwa

Stories of Change - 2023 Competition

Dickson Peter

New Member
Joined
Sep 22, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Lishe bora ni kitu muhimu sana kwa afya yetu na ustawi. Lakini bado, wengi wetu hushindwa kupata lishe bora kila siku kwa sababu ya aina ya vyakula tunavyokula na mitindo yetu ya maisha imejaa vitu visivyofaa.
Leo ningependa kukupatia hadithi kuhusu jinsi lishe bora inavyoweza kubadilisha maisha yako.

Pseudonym anaumri wa miaka 44 alikuwa akisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya kama vile shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari. Ametumia dawa nyingi kwa muda mrefu lakini hali yake bado haijaanza kupona hata kidogo. Daktari alimueleza pseudonym kwamba matatizo yake yanatokana na ulaji wake wa vyakula visivyofaa. Kwahiyo Dactari akampatia rufaa ya kwenda kumuuona mtalaamu wa lishe (nutritionist) ili yeye ampatie ushauri lishe ili kuacha vyakula visivyofaa.

Pseudonym baada ya kufika kwa mtalaamu wa lishe, mtalaamu wa lishe alimueleza kuzingatia lishe bora kwa kula mlo kamili huku akimsisitiza kuepuka vyakula vyenye mafuta sana na sukari nyingi na badala yake ale aina tofauti ya vyakula kama matunda, mboga mboga na protini chache.

Pseudonym alisikia ushauri wa mtalaamu wa lishe na akaanza kubadilisha mtindo wa maisha. Kuanzia siku hiyo, alibadilisha chakula chake na kuzingatia lishe bora. Aliongeza matunda na mboga mboga katika lishe yake, alianza kutumia sukari kidogo na mafuta, na akawa akipika chakula mwenyewe badala ya kununua vyakula vilivyopikwa.

Baada ya siku kadhaa, "Pseudonym" alianza kuhisi mabadiliko katika mwili wake. Alikuwa na nguvu zaidi, na hali za uchovu zilipungua. Afya yake ilianza kuboreshwa pole pole, ugonjwa wa kisukari ukadhibitiwa. "Pseudonym" aligundua pia jinsi chakula kizuri kina athari kubwa katika mfumo wake wa kinga, kwani hakuwa tena anaugua mara kwa mara.

Miaka michache baadaye, pseudonym amekuwa na afya nzuri kabisa. Anamshukuru sana daktari wake kwa kumpa ushauri wa lishe bora, kwani bila hiyo maisha yake yangelikuwa tofauti kabisa.
Kwa sasa pseudonym anafikiria kusaidia kuelimisha jamii yake kuwa na afya bora kwa kupitia ushauri na elimu ya lishe bora aliyoipata kutoka kwa Dactari wake.
Kama pseudonym , tunaweza kuchukua hatua madhubuti ya kubadilisha mtindo wetu wa maisha na kuzingatia lishe bora. Inahitaji kuchukua muda kidogo na uvumilivu ili kuona matokeo thabiti ya kiafya na kuwa mwenye maisha marefu yenye afya bora.

Andiko hili linasisitiza juu ya kuzingatia kuonana na watalaamu wa lishe tufikapo hospitalini, na kuzingatia elimu tunayoipata juu ya ulaji unaofaa.
 
Upvote 2

Ninaombeni kula zenu
 
Back
Top Bottom