Lisilowezekana kwa wanadamu kwa Mungu Linawezekana

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
Lisilowezekana kwa wanadamu kwa Mungu Linawezekana

Siku ya leo nilikuwa katika maombi kwa ajili ya watumishi wa Mungu ambao wamekuwa wakipitia katika changamoto mbalimbali za kidunia.

Moyoni mwangu Mungu alipitisha mistari ya kuomba kwa ajili ya watumishi hao, ambao kwa kweli wanapitia katika changamoto mbalimbali

Katika maombi niliyoyafanya kuna ushuhuda uliingia moyoni Mwangu na ushuhuda huu uko katika kitabu cha Wafalme

Katika kitabu cha Wafalme kulikuwa na kipindi cha ukame nchi nzima kiasi kwamba njaa ilikuwa mbaya ambayo haijawai kutoka duniani

Njaa ilikuwa kali kiasi kwamba baadhi ya wazazi waliwatoa watoto wao kama chakula ili waweze kupona na njaa hiyo.

Siku hiyo ambayo Mungu alikusudia kuleta chakula tele kwa Nyumba ya Israeli , Mungu alimtuma Elisha kwenda katika Nyumba ya Mfalme kwa ajili ya kutangaza Neema ya Mungu juu ya Nyumba ya Israeli (Samaria)

Elisha akaenda kuonana na Mfalme wa Israeli wakipindi hicho alikuwa Ahabu ,Elisha akatoa unabii juu ya changamoto waliyokuwa nayo na Kwamba Mungu amesikia kilio chao na siku ya kesho yake Mungu ataleta chakula kwa nyumba ya Israeli kiasi kwamba bei ya chakula itakuwa ni ya chini kama kiasi kwamba akida wa mfalme akasema haiwezekani hata kama Bwana atafungua madirisha ya Mbinguni?

Ni jambo ambalo hakuna mtu angeweza kuamini , wana wa israeli ambao walikula mana jangwani kwa namna ya ajabu wakambishia Mungu kufungua Madirisha ya mbinguni kama alivyofanya jangwani?

Kuna mambo tunaona kabsa hayaweza sogea au hayawezekani

Nataka kukutia moyo kwa habari hii ya 2 Wafalme sura 7 kwamba Mungu anaweza kufanya zaidi ya kile tunachowaza

Mawazo ya wanadamu yana ukomo, unaweza kupima kwa kipimo chako cha ubinadamu ukaona jambo haliwezekani

Nachokuomba weka imani yako kwa Mungu kama inawezekana

Ibrahimu alipoitwa na Mungu, biblia inasema alimfata Mungu lakini hakujua anakokwenda ila alikuwa na imani na yule aliyemwita

Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.Waebrania 11:8

Unaweza kutokuwa na imani na mazingira yanayokuzunguka kazini, familia , uchumi nk , lakini mazingira hayawezi kumzuia Mungu kufanya kile anachotaka kufanya kwa ajili yako.

Kila jambo kwa wakati wake, leo lile ambalo unaona aliwezekani kesho utakuja na kicheko ukimshukuru Mungu kwamba hakuna lisilowezekana kweke

Sio kwamba maisha yatakuwa raisi, hapana tunamjua aliyetuita, tunamjua Yesu ambaye alisema kwake hakuna lisilowezekana

Sarah alipopewa taarifa ya kupata mtoto akiwa na miaka 99 alicheka, na Mungu alimpa kicheko

Jambo ambalo leo linaonekana ni kichekesho kwako lakini hiko siku ambayo Mungu akifanya waliokua wanakucheka watakusalimia kwa heshima kama muimbaji mmoja alisemavyo

Nataka kukutia moyo ndugu yangu katika Kristo njia za Mungu sio njia za Mwanadamu na Mawazo ya Mungu sio ya Mwanadamu

Yako mengi Mungu amefanya katika maisha yangu na mengine nilikata tamaa hata kuamini kwamba Mungu atafanya lakini kwa wakati wake alifanya

Wakati wa Mungu ni sahahihi, kazi ya wakati ni kuimarisha imani yetu kwa Mungu, na Mungu akubariki.
 
Huyo ni Mungu aliyemtengeneza kichwani mwako au sio??
Acha kuishi kwa ndoto ishi uhalisia.
 
Huyo ni Mungu aliyemtengeneza kichwani mwako au sio??
Acha kuishi kwa ndoto ishi uhalisia.
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Zaburi 14:1
 
Mwakujonga😃 ila mbeya kwa kujipa uchungaji kwa ku fosi mpo vizuri.
Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;

2 Timotheo 1:8
 
Ibrahimu alipoitwa na Mungu, biblia inasema alimfata Mungu lakini hakujua anakokwenda ila alikuwa na imani na yule aliyemwita
Achana na masimulizi ya kihistoria ambayo jayathibitiki miaka na miaka mnahubiri hayo hayo ya Ibrahim, Sisi wasiojulikana wanatumaliza na kuweka watu sijaona huyo Mungu wa Ibrahim kafanya nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…