Pre GE2025 Lissu aelewe Ukomo wa Madaraka siyo kwa wenzake tu hata yeye anahitajika kupisha Damu Changa

Pre GE2025 Lissu aelewe Ukomo wa Madaraka siyo kwa wenzake tu hata yeye anahitajika kupisha Damu Changa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Niendelee kutanguliza Msimamo wangu kuwa mimi pia ni Shabiki wa Lissu nakubali akili kubwa aliyobarikiwa,uwezo wa kujenga na kupangua hoja, Uwezo wa kusimamia anachokiamini hadi mwisho, Ujasiri, na hivi karibuni kanifurahisha aliposema hata akishindwa hatatoka CHADEMA ingawa kwa analysis niliyoifanya naona akishindwa nafasi hiyo ya Uenyekiti.

Back to the point nimevutiwa na hoja zake za ukomo wa Madaraka katika nafasi mbalimbali ingawa yeye ametarget Uenyekiti anaogombea na Viti Maalum lakini sababu aliyosema ni moja kupisha Damu Changa na kutoa nafasi kwa wengine,kimsingi hii ni hoja nzuri sana kwasababu bila Wengine kuondoka hata huyo Mbowe asingeonekana.

Soma: Kuelekea 2025 - Lissu ataka Ukomo wa Madaraka kwenye nafasi za uongozi CHADEMA. Asema itapunguza 'Uchawa'

Ila nataka kuboresha kwa Lissu kwamba asiishie hapo tu aende zaidi ya hapo hadi kwenye Ubunge,Ugombea Urais,Makamu Mwenyekiti,Katibu nk kote kuwe na Ukomo wa muda na ili tuone vipaji vingine,hili limguse na yeye kwasababu ameshahudumu kwa miaka 20 aonyeshe mfano kuwa inatosha wengine waendelee.

Ni mtazamo tu masela msijenge Chuki ingawa kiuhalisia Mbowe,Lissu,Lema,Heche wanahitajika bado kwenye kuongoza mabadiliko.

Ni hayo tu.
 
Kwani alishawahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa miaka mingapi? au mleta uzi umepiga chang'aa!!
 
Back
Top Bottom