Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 450
- 3,368
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Tundu A. Lissu amewasilisha Maombi mahakama kuu ya Tanzania akiomba kuunganishwa kwenye shauri namba 8323/2025 lililofunguliwa na SAID ISSA MOHAMED na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama.
Mhe Lissu anaiomba mahakama aunganishwe kwenye shauri hilo maarufu kama “kesi ya wazanzibari” (kutokana na kufunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Zanzibar) ambapo Mhe Lissu anaomba kuunganishwa kama mdaiwa.
Mtakumbuka kwamba kesi hii ndiyo ilisababisha Chama kuzuiliwa kufanya shughuli za siasa pamoja na zuio la kutotumia rasilimali za Chama uamuzi uliotolewa na Jaji Hamidu Mwanga.
Maombi hayo, yameshasajiliwa mahakamani na kinachosubiliwa kwa sasa ni wito (summons) kwa wajibu Maombi hayo ili taratibu za kusikiliza Maombi hayo zianze rasmi.