"Chama chetu kinamjadala mkubwa sana kwasababu ya kusema hayo na nje ya huo mjadala tutapata suluhu ya matatizo hayo kwasababu rushwa sasa inazungumzika, tunaweza tukaikabili."
"Kwasababu Samia amekataa mabadiliko ya Katiba na tume expose huu uongo wa maridhiano ndio maana tunazungumza habari ya 'No reform, no election', tusingefanya hivyo tungeambiwa kwamba mambo yanaenda vizuri, msijali watu wanaendesha maisha yao. Kwahiyo maneno yangu, ukweli niliousema…nasisitiza ni ukweli."
"Mimi sio mropokaji kama ambavyo nimesema wasingenipa dhamana yote hii ambayo waminipa miaka yote…nimesahau nilikuwa…waliniteua kuwa mgombea wa Urais wa nchi hii mwaka 2020 kwa uropokaji wangu na kwa haya yote wanayo yasema haya, ni maneno ya watu ambao hawana hoja yoyote ya maana kuhusiana na Uchafu ambao nimeuweka wazi."
"Niongeze kingine, kuna mambo ambayo kama ningeyasema hadharani….kuna mambo ambayo kama nikiyasema hadharani watu watakimbia sana."