Lissu akihama CHADEMA atahama na wanachama zaidi ya asilimia 90

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Nimemsikia Lissu akinukuu maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere aliposema kuwa CCM siyo Mama yake wakati wowote anaweza kuondoka vile vile Lissu naye kasema kuwa CHADEMA SIYO mama yake.

Maneno haya Lissu ni mazito sana. Nadhani kuna tatizo ndani ya CHADEMA na hili linatakiwa lipatiwe ufumbuzi.

Kama kweli kuwarudisha COVID 19 ambao walikisaliti Chama naungana na Lissu kwa asilimia 100 wasirudishwe kwenye Chama hao tayari walikwishafukuzwa.

Hapo hakuna mjadala na kama wanawatetea namuunga Lissu aachane na CHADEMA.

Kama Lissu atahama CHADEMA basi atahama na karibu asilimia 90 ya wananachama. Ngoja tusubiri wakati ukuta.
 
Sijawahi kuwa na mrengo wowote wa chama cha siasa Tanzania, lakini kwa mtazamo wangu nikwamba.....
Hakuna chochote kitakacho tokea ikiwa Lisu ataihama CHADEMA, na badala yake itakua ni upepo tu uliovuma kama alivyo Dr. Slaa alivyo ondoka CHADEMA ama Lowasa alivyo ondoka CCM.
 
"Kuna tatizo ndani ya CHADEMA" hili siyo jambo jipya, tumekuwa tukilisema humu JF kwa muda kitambo sana. Tatizo lilianza na hao mabinti kuchukua ubunge wakati chama kilipokuwa kwenye hali ngumu sana chini ya Magufuli. Hawa mabinti kamwe wasingeweza kufanya jambo lile bila ya uhusika wa kiongozi/viongozi kuwa nao karibu na kuwapa ushirikiano.
Sababu za kufanya hivyo huku chama kikiwa kimeporwa kila nafasi baada ya "uchafuzi" alioufanya Magufuli, bado hazieleweki.
Lakini sasa hakuna shaka yoyote kuhusu ushiriki wa "KIONGOZI" mkubwa katika kukihujumu chama hicho wakati huo.

Alipo ingia 'Chura Kiziwi', na kuingiza hadaa za "maridhiano"; hapa ndipo Mbowe alipo zolewa moja kwa moja na kusahau kwamba anakitumbukiza chama chake katika matatizo makubwa.

Sina shaka hata kidogo, mambo haya mawili ndiyo yaliyo kimaliza hiki chama.

Tundu Lissu kuondoka CHADEMA wakati huu itakuwa ni hasara kubwa katika jitihada za kuiondoa CCM madarakani; kwani muda uliopo kabla ya chaguzi hizi ni kidogo sana. Hawezi kwenda kwenye chama kingine na kujenga nguvu za kutosha kuisambaratisha CCM kwa sasa.

Kungekuwepo na kundi lenye nguvu ndani ya CCM lenye kutaka kukibadili chama hicho kitokane na ulaghai ulioko huko sasa hivi, ingewezekana akaungana na kundi hilo, lakini kwa sasa wote ni watu wanaotegemea fadhila na utegemezi kwa chama ili kukidhi mahitaji yao binafsi.

Ndani ya CHADEMA, kuna kundi lisilokubali kuuzwa chama chao kwa 'Chura Kiziwi'. Lissu afanye kazi kuliongoza kundi hili lipambane na CCM hii iliyo oza.
 
Sijawahi kuwa na mrengo wowote wa chama cha siasa Tanzania, lakini kwa mtazamo wangu nikwamba.....
Hakuna chochote kitakacho tokea ikiwa Lisu ataihama CHADEMA, na badala yake itakua ni upepo tu uliovuma kama alivyo Dr. Slaa alivyo ondoka CHADEMA ama Lowasa alivyo ondoka CCM.
Maana yake ni kwamba una mlengo wa CCM ulio kutia upofu mkubwa akilini; pengine bila kujitambua.
 
Nimemsikia Lissu akinukuu maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere aliposema kuwa CCM siyo Mama yake wakati wowote anaweza kuondoka vile vile Lissu naye kasema kuwa CHADEMA SIYO mama yake.

Maneno haya Lissu ni mazito sana. Nadhani kuna tatizo ndani ya CHADEMA na hili linatakiwa lipatiwe ufumbuzi.

Kama kweli kuwarudisha COVID 19 ambao walikisaliti Chama naungana na Lissu kwa asilimia 100 wasirudishwe kwenye Chama hao tayari walikwishafukuzwa.

Hapo hakuna mjadala na kama wanawatetea namuunga Lissu aachane na CHADEMA.

Kama Lissu atahama CHADEMA basi atahama na karibu asilimia 90 ya wananachama. Ngoja tusubiri wakati ukuta.
Ahamie wapi mganga njaa mkubwa, walimuona Dkt Slaa mjinga na wakaungana kutaka kumdhuru. Hahaha na mbowe atawamaliza ile ni project ya familia ya mbowe hakuna chama hapo
 
Nimemsikia Lissu akinukuu maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere aliposema kuwa CCM siyo Mama yake wakati wowote anaweza kuondoka vile vile Lissu naye kasema kuwa CHADEMA SIYO mama yake.

Maneno haya Lissu ni mazito sana. Nadhani kuna tatizo ndani ya CHADEMA na hili linatakiwa lipatiwe ufumbuzi.

Kama kweli kuwarudisha COVID 19 ambao walikisaliti Chama naungana na Lissu kwa asilimia 100 wasirudishwe kwenye Chama hao tayari walikwishafukuzwa.

Hapo hakuna mjadala na kama wanawatetea namuunga Lissu aachane na CHADEMA.

Kama Lissu atahama CHADEMA basi atahama na karibu asilimia 90 ya wananachama. Ngoja tusubiri wakati ukuta.
Your thinking and wishes! he will shift with some of them, not to that tune! Kwa iyo chadema ni Lisu......very strange
 
Aende tu CHADEMA kitabaki imara lakini asisahau mWAMBA NDO ALIEMNUSURU kIFO !
 
Back
Top Bottom