Maneno haya Lissu ni mazito sana. Nadhani kuna tatizo ndani ya CHADEMA na hili linatakiwa lipatiwe ufumbuzi.
"Kuna tatizo ndani ya CHADEMA" hili siyo jambo jipya, tumekuwa tukilisema humu JF kwa muda kitambo sana. Tatizo lilianza na hao mabinti kuchukua ubunge wakati chama kilipokuwa kwenye hali ngumu sana chini ya Magufuli. Hawa mabinti kamwe wasingeweza kufanya jambo lile bila ya uhusika wa kiongozi/viongozi kuwa nao karibu na kuwapa ushirikiano.
Sababu za kufanya hivyo huku chama kikiwa kimeporwa kila nafasi baada ya "uchafuzi" alioufanya Magufuli, bado hazieleweki.
Lakini sasa hakuna shaka yoyote kuhusu ushiriki wa "KIONGOZI" mkubwa katika kukihujumu chama hicho wakati huo.
Alipo ingia 'Chura Kiziwi', na kuingiza hadaa za "maridhiano"; hapa ndipo Mbowe alipo zolewa moja kwa moja na kusahau kwamba anakitumbukiza chama chake katika matatizo makubwa.
Sina shaka hata kidogo, mambo haya mawili ndiyo yaliyo kimaliza hiki chama.
Tundu Lissu kuondoka CHADEMA wakati huu itakuwa ni hasara kubwa katika jitihada za kuiondoa CCM madarakani; kwani muda uliopo kabla ya chaguzi hizi ni kidogo sana. Hawezi kwenda kwenye chama kingine na kujenga nguvu za kutosha kuisambaratisha CCM kwa sasa.
Kungekuwepo na kundi lenye nguvu ndani ya CCM lenye kutaka kukibadili chama hicho kitokane na ulaghai ulioko huko sasa hivi, ingewezekana akaungana na kundi hilo, lakini kwa sasa wote ni watu wanaotegemea fadhila na utegemezi kwa chama ili kukidhi mahitaji yao binafsi.
Ndani ya CHADEMA, kuna kundi lisilokubali kuuzwa chama chao kwa 'Chura Kiziwi'. Lissu afanye kazi kuliongoza kundi hili lipambane na CCM hii iliyo oza.