LGE2024 Lissu akiri CHADEMA kuhusika na mauaji ya wanachama wao

LGE2024 Lissu akiri CHADEMA kuhusika na mauaji ya wanachama wao

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hili suala linachanganya sana, wengi wanasema Lissu anazuiliwa kugombea uwenyekiti na ndio inapelekea yeye kuanika uovu wanaofanyiana. Kwanini watanchi tuchague watu wa namna hii?


Video ya Juu ni ile inayopotosha, video ya Chini ni ile inayozungumza Ukweli kutoka BBC.

images.jpeg

Tundu Lissu​
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ambapo mwaka 2017 Alikuwa Rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kwa miezi mitano kabla ya kushambuliwa kwa risasi. Mwaka 2010 mpaka 2020 alikuwa ni mwakilishi wa wananchi Bungeni wa jimbo la Singida Mashariki.

Lissu anasifika kutokana na haiba yake ya kutokuogopa kukemea vitendo ambavyo vinakiuka taratibu za kidemokrasia na haki za binadamu iwe ndani ya chama chake au nje ya chama chake. Mara kadha kauli zake zimekuwa zikitumiwa vibaya katika muktadha tofauti lengo likiwa ni kupotosha.

Kumekuwepo na video ambayo inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Lissu akifanya mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza ambapo anaonekana akisema CHADEMA wana ruhusa ya kuuana na kwamba Chacha Wangwe aliuwawa na CHADEMA huku akimtaja Freeman Mbowe kuwa ndiye aliyemuua Ali Kibao.

Ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutoka kwenye video halisi ambayo chanzo chake ni BBC kwani katika video halisi Lissu hakutaja CHADEMA wala Mbowe kuhusika katika mauaji ya viongozi wa chama hicho.

Kilichofanyika katika video hiyo inayopotosha ni kukata vipande vidogovidogo kutoka video halisi ya BBC na kuviunganisha hatimaye kutengeneza video inayopotosha uhalisia wa video ya awali.

Mnamo septemba 12, 2024 BBC ilirusha matangazo ya Dira ya dunia ambapo yalikuwa mbashara kupitia mtandao wa Youtube, katika matangazo hayo Leonald Mubali alifanya mahojiano na Tundu Lissu wakiangazia hali ya kisiasa nchini Tanzania pamoja na matukio ya utekaji.

Aidha Lissu akijibu swali la Mubali juu matukio ya mauaji ambayo imekuwa ikidaiwa kuwa wahusika ni kutoka ndani ya CHADEMA, Lissu alisema

“Nimenza kusikia maneno hayo miaka mingi sana hata kushambuliwa kwangu walisema hivyohivyo, haya mambo ya CHADEMA, Mbowe, kwanini katika nchi hii kama ni kweli yanafanywa na CHADEMA, na wanachama au viongozi wa CHADEMA kwanini miaka tangu wameanza kutusingizia, kwanini hata mara moja hawajawahi kuchukua hatua kuyachunguza na kuyatolea taarifa ya uchunguzi na kuyapeleka mahakamani ili wauaji hawa wakachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za Tanzania, haya maneno ni maneno ya aidha wahusika wenyewe au wauaji wenyewe au wapambe wao, au walinzi wao au wanaofaidika na mauaji haya”

Kadhalika Lissu alisema hawana imani na jeshi la polisi, idara ya usalama wa taifa pamoja na serikali ya Rais Samia hivyo kuitajaserikali kuleta mamlaka za uchunguzi za kimataifa dhidi ya mauaji ya Ali Kibao aliyetekwa na kuuawa.

Aidha video hiyo iliyopotoshwa na kuonekana kuwa ni ya BBC haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya shirika hilo lakini pia video hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo kuruka kwa sauti kutokana kuunganishwa katika sehemu zisizofanana, lakini pia kutokuonekana kwa picha ya Lissu akimtaja Mbowe lengo la wapotoshaji likiwa ni kuficha kuonekana kwa utofauti wa sauti na utamkaji wa maneno ya Lissu jambo ambalo lingerahisisha kujulikana kwa video hiyo kuwa imepotoshwa.

Video hiyo inayopotosha imehifadhiwa hapa na hapa.
Back
Top Bottom