Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Watu wakiishiwa hoja, husingizia jinsia ama dini!
Lissu sifahamu kama ni Mkristo ama dini gani. Ninachojua Tundu Lissu kwake suala la dini, ni la mtu na Mungu wake na siyo Tanzania inajisiwe na mtu awaye yote kwa sababu ya dini yake
Inapotokea kiongozi yeyote anakuwa kinyume na sheria za nchi, haijalishi ni muumini wa dini gani, kwa Tundu lissu, lazima ubaya wa mtu huyo utaanikwa tu.
Amewaanika viongozi wa dini ya Kikristo na ataendelea kuwaanika na wengine pia.
Ieleweke hivi, watanzania tunapaswa tuwe na mtazamo wa kama Tundu Lissu, viongozi wanapovunja katiba bila kujali wanatoka dini gani, tusimame kwa pamoja kukemea uovu huo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeondokana na hili la mtu anaposemwa eti inakuwa anasemwa kwa sababu ya dini yake.
Tukifanya hivyo tutafika mbali sana.