- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kamanda Tundu Lissu amekanusha madai yaliyotolewa hapo nyuma kidogo na Lema kwamba Mbowe ndio aliyeshika chupa ya damu wakati akipelekwa Nairobi kwa matibabu.
Amesema aliyeshika chupa ya damu aliyokuwa akiongezewa ni Mchungaji Peter Msigwa mwanasiasa nguli asiyeogopa hila na figisu.
Wataalam wa mambo ya siasa za kusini mwa jangwa la sahara wanasema hii kauli imebeba maana kubwa sana.
Amesema aliyeshika chupa ya damu aliyokuwa akiongezewa ni Mchungaji Peter Msigwa mwanasiasa nguli asiyeogopa hila na figisu.
Wataalam wa mambo ya siasa za kusini mwa jangwa la sahara wanasema hii kauli imebeba maana kubwa sana.
- Tunachokijua
- Mnamo September 7, 2017 Makamu Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA alinusurika kifo baaada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari la jijini Dodoma. Muda mchache baada ya tukio hilo Tundu Lissu alikimbizwa hospitali ya General Dodoma na baadaye Nairobi kwa ajili ya matibabu na kunusuru Maisha yake (Soma hapa).
Baada ya matibabu ya awali Tundu Lissu alihamishiwa nchini Ubelgiji ambako alipata matibabu yote mpaka kuwa katika hali salama na kuweza hata kugombea Urais wa nchi mwaka 2020 Soma (hapa).
Kuanzia mwezi Mei, 2024 chama cha CHADEMA kimekuwa kikifanya uchaguzi wake wa ndani kuchagua viongozi wa Kanda mbalimbali. Baadhi ya Kanda zimeonesha ushindani mkubwa na na kupelekea Wagombea kukata rufaa ya kutokubaliana na matokeo baada ya kushindwa soma (hapa). Jambo hili na mambo mengine kuelekea uchaguzi yamezua sintofahamu nyingi ndani ya chama soma hapa, hapa, hapa na hapa.
Kuanzia mwezi Juni, 2024 ikiwa ni miaka sita na miezi nane tangu kutokee tukio la Lissu kushambuliwa na Risasi (Soma hapa), kumeibuka hoja mpya ikitoa taswira tofauti ya siku ya tukio wakati Tundu Lissu anapelekwa kwenye matibabu jijini Nairobi. Hoja hizo ni za pande mbili, moja inadai siku ya tukio hilo Mbowe ndiye aliyeshikilia chupa iliyokuwa ikimuwekea damu Lissu wakati anasafirishwa kwenda Nairobi, hoja hii imetolewa na Godbless Lema kupitia akaunti yake ya X (Twitter) Soma (hapa). Kwa upande mwingine kuna kauli zinadai Mchungaji Msigwa ndiye aliyeshika mfuko huo wa damu wakati akikimbizwa hospitalini Nairobi.
Upi ukweli wa Sakata hili?
JamiiCheck imefuatilia Sakata hili kwa kupitia vyanzo vya kauli za wahusika wote wanaotajwa kwenye tukio hili (Lissu, Mbowe, Lema na Mchungaji Msigwa) kuhusu sakata linalotajwa kaka ifuatavyo:
Lissu akiwa Singida katika Mkutano wa kisiasa Jukwaani alionekana kwenye video na kusikika akisema:
Yeye (Mchungaji Msigwa) ndiye aliyekuwa amebeba chupa ile ya damu wakati ule napatiwa damu, katika watu wamesaidia sana tuko pamoja leo niko naishi ni pamoja na huyu rafiki yetu Mheshimiwa Peter Msigwa, naombeni mumpigie makofi ya shukrani. Na amekuja kutokea Iringa hajawekewa mafuta na mtu, hajapewa posho na mtu yeyote. Nimemwambia Mchungaji njoo tufanye mikutano tuzungumze na Wananchi wa Singida akasema Lissu nakuja
Video hiyo ya Lissu (hii hapa) ilichukuliwa na Mchungaji Msigwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wake. Hii ikiwa ni ishara ya Msigwa kuunga mkono kile kilichosemwa na Lissu.
Picha ikionesha video ya Lissu aliyoichapisha Mchungaji Msigwa wakati anaongelea sakata hilo
Kwa upande wake Mbowe, kuna video (hii) ya Juni 12, 2019 inamuonesha akiwa kwenye Mkutano wa ndani wa Chama akisimulia kwa kirefu namna ilivyotokea siku ya tukio la kushambuliwa kwa Lissu. Akieleza kuhusu aliyeshika mfuko wa damu alisema:
Tukampakia kwenye ndege Lissu hapo alikuwa anaendelea kupata huduma muhimu ya damu na Oksijeni. Kuna mtungi wa Oksijeni lakini unavuja kidogo pale juu kwenye ile valvu. Kwahiyo inabidi kupampu wakati wote ili asikose Oksijeni, kazi hiyo naifanya mimi. Msigwa amekamata damu maana yake mahali pa kutundika ile dripu iweze kushusha damu kwenye mwili hapapo. Kwahiyo lazima ashike dripu ile juu. Madaktari walikuwa wakimziba Lissu ili asipate maumivu na kuhakikisha oksijeni inaingia. Yaani ilikuwa shughuli.
Picha inayoonesha Video ya Mbowe akisimulia harakati za kumsafirisha Lissu kwenda Nairobi zilivyokuwa
Video hiyo ya Mbowe ililetwa pia na Mwanachama wa JamiiForums Jokakuu akiileta kutoa ushahidi na kupinga hoja ya Godbless Lema kuwa aliambiwa Mbowe ndiye alibeba chupa ya damu.
Hivyo, kutokana na kauli hizi za wahusika waliokuwawepo siku ya tukio kufanana na kukubaliana, JamiiCheck inaona kuwa hoja ya Lema kuwa Mbowe ndiye alishika mfuko wa damu haina ukweli.
Nini mtazamo wako kuhusu sakata hili?