- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu jamiiCheck je ni kweli Lissu ameyasema haya?
Pia nimekutana na hii inadai kuwa Kasema "BORA NCHI IWAKE MOTO TUANZE UPYA "KUNA UKWELI KUHUSU MANENO HAYO
Pia nimekutana na hii inadai kuwa Kasema "BORA NCHI IWAKE MOTO TUANZE UPYA "KUNA UKWELI KUHUSU MANENO HAYO
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025 amkimshinda Freeman Mbowe ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 20.
Mnamo mwezi februari 12, 2025 mwenyekiti huyo wa CHADEMA alifanya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Chama hichoMikocheni Dar es salaam.
Madai
Mara nyingi kumekuwapo na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikimuhusisha Lissu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya chama chake. Rejea hapa, hapa, hapa na hapa.
Kumekuwapo na taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV kwamba Lissu amesema wamepokea ushauri wa viongozi wa dini kuhusu amani na kushiriki uchaguzi na wametii.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Lissu hakutoa kauli hiyo kuhusu kupokea ushauri wa viongozi wa dini juu ya masuala ya uchaguzi na amani. Tazama hapa mkutano huo.
Vilevile chapisho lililobeba taarifa hiyo halikuchapishwa na Jambo TV katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii bali wapotoshaji walitumia utambulisho wa televisheni hiyo ya mtandaoni ili kusambaza taarifa hiyo isiyo ya kweli. Rejea hapa kuona taarifa zilizowahi kupotoshwa zikitumia tambulisho wa chombo hicho.
Aidha akizungumzia umuhimu wa viongozi wa kidini katika kupigania mabadiliko alisema wananchi wanawasikiliza zaidi viongozi wa kidini kuliko viongozi wa kisiasa akitoa wito kwa viongozi hao kushughulikia matatizo ya kila siku yanayowakumba wananchi na si kuishia kwenye masuala ya kiroho tu. Rejea hapa 1:21:35
Madai
Mdau pia amehitaji kupata uhalisia iwapo Lissu alisema kuwa ni heri nchi iwake moto ili tuanze upya taarifa ambayo imechapishwa na katika ukurasa wa cheche times.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa Taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli kwani katika hotuba aliyoitoa Lissu hakuna mahali aliposema kuwa bora nchi iwake moto ili tuanze upya.
Katika hotuba yake Lissu alizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo kuhusu mapungufu mbalimbali yaliyotokea kwenye chaguzi zilizopita na namna ya kuboresha mfumo ili kuepukana na changamoto zilizojitokeza kwenye chaguzi zilizopita. Aidha aligusia pia kuhusu mapungufu ya sheria za uchaguzi zilizopo na akatoa mapendekezo bila kuchochoea mafuko
View: https://www.youtube.com/live/CvEotwzc8_c?si=9iYlgaV60cSdidY2&t=4895