Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025 amkimshinda
Freeman Mbowe ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 20.
Mara nyingi kumekuwapo na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikimuhusisha Lissu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya chama chake. Rejea
hapa,
hapa, hapa na
hapa.
Mnamo Januari 29, 2025 kwa mara ya kwanza Lissu alipokelewa katika makao makuu ya chama hicho baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti na kutoa hotuba yake
akisisitiza kauli ya "Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi." (No Reforms No Election) na kwamba chama hicho hakitasusia uchaguzi.
Kumekuwapo na
taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Mwanahalisi Digital kuwa Lissu amesema yeye ni mfaidika nambari moja wa maridhiano, hivyo ni muhimu yakawepo.
Je, ni upi uhalisia wa Chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haikuchapishwa na
Mwanahalisi Digital kama inavyoonekana bali wapotoshaji walitumia utambulisho huo kutengeneza na kusambaza taarifa isiyo ya kweli.
Aidha katika mikutano yake aliyoifanya hivi karibuni Lissu hakutoa kauli hiyo ambapo katika mkutano wa hadhara alioufanya akiwa Ikungi Singida aliendelea
kukosoa maridhiano akisema hayakuwa na msaada wowote kwani bado yaliyofanyika katika utawala uliotangulia bado yaliendelea kufanyika baada ya utawala huo.
Hata hivyo Chapisho hilo limebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayolitofautisha na machapisho rasmi ya Mwanahalisi Digital ambapo sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kukosekana kwa alama ya Mastari unaolizunguka chapisho upande wa juu, utofauti katika mpangilio wa maandishikwenye kichwa cha habari (Title)