Lissu amkubali Sitta

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441

Dodoma. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya chama au ya kundi la watu wachache.

Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu ya watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu wakiingia katika uchaguzi, wataangushwa na Sitta.

"Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake," alisema Lissu.Alisema katika kipindi ambacho aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.

Akizungumzia tetesi kuwa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ameonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo, alisema hayuko tayari kumuunga mkono.

Lissu alisema Chenge hataweza kuliongoza Bunge hilo na kwamba kama atachaguliwa, litavunjika likiwa mikononi mwake.

Kuhusu Samia Suluhu Hassan anayetajwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti , alisema hana shaka pia ingawa hajaonyesha makeke yake mbele ya vikao muhimu kama vya Bunge, lakini ni mzoefu wa muda mrefu serikalini na katika nafasi mbalimbali.

chanzo:Mwananchi
 
Sitta anakubarika na wajumbe wote wa bunge la katiba na watanzania wote.
 
Mtu akimpinga sitta atakuwa anachuki binafsi japo chuki zake haziwezi kufua dafu.
 
sasa LISSU ameanza kupevuka kale katabia ka kupinga kila kitu hata kizuri annanza kuiacha .yes masilahi ya taifa mbele chama nyuma ahsante kwa hilo.
 
Kwa kuwa hakuna mkamilifu yeye atafaa zaidi kumlinganisha na wenzie walowahi kukalia kiti cha uspika lkn tusimsifu kwa kupitiliza naye ana mapungufu yake, tukumbuke issue ya richmond alionesha msimamo mkali lkn baadae akabadirika na kuondoa mjadala bungeni ghafla sijui alitishwa au aliahidiwa kitu flani, kwa hiyo tupunguze ukubwa wa matarajio kwake japo anafaa.
 
Wananchi tuna imani naye. Anafaa tumechoka ona maspika wasio na mvuto. Mpeni mzee wa viwango kiti
 
Mgema akisifiwa--- yangu macho mumwagieni mi sifa ila akiyakoroga msibadilishe kauli. Nafasi hiyo wange mpa Komba au kingunge nisingekuwa na shaka.
 
Damu ya uchama ningumu kuitoa sidhani kama atafanya kinyume na matakwa ya chama hata kama atachaguliwa...
 
Sitta ni upepo wa same hazuiliki maadui zake nendeni taratibu
 
Damu ya uchama ningumu kuitoa sidhani kama atafanya kinyume na matakwa ya chama hata kama atachaguliwa...

Ni kweli ana uchama ndani ya moyo wake na kama kweli angekuwa Msafi na mkweli basi leo hii tusingekuwa tunaendelea kuongelea RICHMOND
 
Sitta for Presidency...kumbe ni Uspika wa BMK
 
Mgema akisifiwa--- yangu macho mumwagieni mi sifa ila akiyakoroga msibadilishe kauli. Nafasi hiyo wange mpa Komba au kingunge nisingekuwa na shaka.
mkuu umenichekesha sana, sasa komba hoja zikimuelemea si ataanza kutumbuiza pale kwenye kiti mbele ya bunge? na yeye ndo muamuzi wa mwisho, nani atamkataza?
 
Lissu lazma amkumbali Sitta WA CCM, sababu CCM Ni chama makini na kina watu makini.
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi. Slaa alimwita Mnafiki, leo Lissu anamwita Muadilifu. Mwenyekiti wa Bunge anaweza kutoka Chama chochote ila Mwenyekiti Bora lazima atoke CCM.
 
Ukweli ni kwamba, Samwel Sita anaungwa mkono na wengi, na hii ni kutokana na uwezo wake aliounyesha tangu alipokuwa spika wa bunge, hapa ushabiki wa vyama tuweke pembeni, cha msingi Sita alinde matumaini waliyonayo watu juu yake, kwa kuhakikisha analiendesha bunge ipasavyo pasipo kujali itikadi za chama au maslahi ya kundi fulani, uwezo anao, labda aamue tu kufanya ya kwake, na kwa kufanya hivyo, ajue kuwa atakuwa ameliangamiza taifa.
 
Mtu akimpinga sitta atakuwa anachuki binafsi japo chuki zake haziwezi kufua dafu.
sasa kama mnalijua hilo, kwa nin mlimtoa kugombea kiti cha spika badala yake mkatuwekea yule mama mwenye wigi kuuubwa????????????.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…