Sitta ni poa ni yeye pekee ndani ya CCM aliyebaki anapigania taifa wengine wote wezi wakiongozwa na baba yao Lowassa
Mkuu, Mwanamutapa, CCM ni chama cha mafisadi na walarushwa wakuu, mwenye afadhali kati ya mafisadi hao wa CCM ni EL, yeye keshashiba, sasa angalau anarudisha japo kidogo kwa wananchi kupitia harambee mbalimbali!, wengine japo wameshiba hadi kuvimbiwa, wanaendelea kula tuu mpaka matumbo yapasuke!.
Sitta nae anao ufisadi wake, kwa vile na mimi namfagilia sana Sitta kwenye uenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum, naomba nisiutaje ufisadi wake kwa sasa, ila just a tip, kwenye sakata la Richmond, Sitta alimnusuru mwenye zigo halisi la Richmond, na badala yake kumbakia EL kwa kumbebesha hilo zigo ahangaikenalo also kuinusur CCM!.
Naomba nikupe hizi tip tatu uzifanyie kazi...
- Matibabu: Akiwa spika, matatizo madogo madogo na magonjwa madogo madogo, akienda hospitali, husisitiza asipewe dawa za hospitalini, na badala yake aandikiwe tuu prescription ya dawa na dawa za kujitibia atanunua mwenyewe toka kwenye maduka ya dawa, na ofisi ya bunge italipia!. Sasa fanya utafiti toka ofisi ya bunge, hizo dawa alizinunua toka duga gani specific, linalomilikiwa na nani, na kikubwa zaidi, find out ghara za hizo dawa zilizolipwa na ofisi ya bunge!.
- Nyumba:Kipindi cha usipika alipangiwa kuishi nyumba nzuri tuu ya serikali, zile zenye hadhi kama za mawaziri!, Jamaa aligoma kuwa nyumba hiyo haina hadhi ya kuishi spika, kwa hoja kuwa kwenye hiearachi ya utawala, wakuu wa mihimili mitatu ya dola, wana hadhi sawa, yaani mkuu wa the executive, the judiciary na the legislature wanatakiwa kuishi nyumba zenye hadhi ya nafasi zao!, hivyo akaruhusiwa kutafuta nyumba ya kupanga ya hadhi yake na serikali itailipia!. Jamaa alitafuta nyumba ya kupanga yenye hadhi ya kukaa spika ikapatikana, kodi ya pango ni doleri 10,000 za kimerekani kwa mwezi!. Serikali ililipia nyumba hiyo!, find out mmiliki halisi wa nyumba hiyo yenye hadhi ya kuish spika ni nani, ambaye ndiye aliyelipwa hiyo kodi ya pango!.
- Gari: Kwa kawaida serikali inavyo viwango tofauti vya magari kwa viongozi tofauti, hadhi ya gari ya spika ilikuwa ni sawa na hadhi ya gari ya Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Makamo wa rais. Jamaa alipoingia alilikataa gari alilopewa eti lina hadhi ya chini, gari hilo ni Mercedes Benz S Class ya 350, yeye akataka S Class 500! yenye hadhi kama benzi ya rais!. Find ou from ofisi ya bunge hivo benzi S Class 500 kwa sasa iko wapi?. Anna Makinda baada ya kuchaguliwa, amenunuliwa benzi nyingine mpya S Class 350!.
Nakuomba ukiisha yapata majibu ya hizo tip tatu, please just kaa nayo fyi only na usiyalete humu, kwa sasa acha tuendelee kumpigania Siita awe Mwenyekiti wa kudumu wa bunge letu maalum, hata mimi nimemfungulia uzi maalum kumkapenia
Ni Busara Wajumbe Wote Wa Bunge la Katiba, Kumuunga Mkono Sitta
NB. Kuna watu ndani ya CCM ukiwaweka kwenye mizania ya uadilifu na EL, utashangaa kumkuta kumbe EL ni kama malaika!, wee acha tuu!
Pasco.