Lissu amkubali Sitta

Lissu amkubali Sitta

sita.jpg

Dodoma. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya chama au ya kundi la watu wachache.

Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu ya watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu wakiingia katika uchaguzi, wataangushwa na Sitta.

“Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake,” alisema Lissu.Alisema katika kipindi ambacho aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.

Akizungumzia tetesi kuwa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ameonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo, alisema hayuko tayari kumuunga mkono.

Lissu alisema Chenge hataweza kuliongoza Bunge hilo na kwamba kama atachaguliwa, litavunjika likiwa mikononi mwake.

Kuhusu Samia Suluhu Hassan anayetajwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti , alisema hana shaka pia ingawa hajaonyesha makeke yake mbele ya vikao muhimu kama vya Bunge, lakini ni mzoefu wa muda mrefu serikalini na katika nafasi mbalimbali.

chanzo:Mwananchi
Sitta ni muumini wa serikali mbili ndio maana ccm wamemkubali
 
Sitta ni muumini wa serikali mbili ndio maana ccm wamemkubali

Sitta ni smart sio muumini wa serikali mbili bali ni muumini wa serikali tatu akiamini akishindwa urais wa Muungano basi akwae wa Tanganyika yeye kutamka serikali mbili ni strategy kwa kujua akisema serikali tatu atakosa kura za urais NEC kwahiyo lazima atamke kutokana na mtizamo wa CCM wengi. Huo ndio usmart wa mtu na shule yake isiyo ya kuangalizia kama Kikwete
 
alikwambia ndio mkakati wake? au unamtilia maneno?
 
alikwambia ndio mkakati wake? au unamtilia maneno?

Crabat, kumbuka Zanzibar wajumbe wengi zaidi hawataki serikali tatu, iwapo mtu una ndoto na mipango ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano ukawa ni muumini wa serikali tatu technically uko nje iwapo hoja ya serikali tatu haitapita, ndio litakuwa zengwe lako
 
Sitta anakubarika na wajumbe wote wa bunge la katiba na watanzania wote.
Haha..lazima tumpende kwani si tulikuwa tunamtumia km kuwadi wetu kwa maccm mengi 50 na office ya spika kutumiwa kwa kazi ya CDM. Hili Bunge mnayo kazi laani nyie
 
Mtu akimpinga sitta atakuwa anachuki binafsi japo chuki zake haziwezi kufua dafu.

MAGAMBA bwana!! Mngempiga chini muone... Maana Bungeni mlimtosa eti kwa kuwapendelea wapinzani... Sasa yako wapi...?? Siasa za mizengwe za CCM kweli ni laana...!! Nyerere 1995 alisema wakati wa kuchagua viongozi wetu kwa mizengwe umeshapita...!!

Haya sasa nyie timu ya Lowassa limewashuka!!!
 
Sitta kama sita ni mtu mwenye msimamo. Lakini Sita kama kada wa CCM sijui. Kumbuka CCM wana msimamo wao ambao wako tayari kufa kuliko kuubadilisha katika Katiba hii inayotengenezwa!
 
Huyu mzee ana misukule karibu 500 yote ikihamie bungeni lazima kila mtu amuogope including Baba Prince
 
Crabat, kumbuka Zanzibar wajumbe wengi zaidi hawataki serikali tatu, iwapo mtu una ndoto na mipango ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano ukawa ni muumini wa serikali tatu technically uko nje iwapo hoja ya serikali tatu haitapita, ndio litakuwa zengwe lako

Kama kura itakuwa ya wazi watakua wengi kidogo kwanii wataogopa yalompata Mansour Yusuf .
Lakini ikiwa kura ya siri wengi wanataka tatu.
Hata hivyo katiba hii kupiita bila ya serikali tatu ni tabu na ukweli tutakua tumepoteza tu fedha zetu.
Nikkiangalia lazima ipite kwa kurra zaidi ya 2/3 hilo naliona gumu upande wa zanzibar.
Hivyo tutaendelea tu na katiba iliyopo na kuendelea na matatizo yetu na huku Uamsho wakiamsha watu kama alovosema Karume.mwisho wote watakua macho ya mchana
 
Sitta ni poa ni yeye pekee ndani ya CCM aliyebaki anapigania taifa wengine wote wezi wakiongozwa na baba yao Lowassa
Mkuu, Mwanamutapa, CCM ni chama cha mafisadi na walarushwa wakuu, mwenye afadhali kati ya mafisadi hao wa CCM ni EL, yeye keshashiba, sasa angalau anarudisha japo kidogo kwa wananchi kupitia harambee mbalimbali!, wengine japo wameshiba hadi kuvimbiwa, wanaendelea kula tuu mpaka matumbo yapasuke!.

Sitta nae anao ufisadi wake, kwa vile na mimi namfagilia sana Sitta kwenye uenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum, naomba nisiutaje ufisadi wake kwa sasa, ila just a tip, kwenye sakata la Richmond, Sitta alimnusuru mwenye zigo halisi la Richmond, na badala yake kumbakia EL kwa kumbebesha hilo zigo ahangaikenalo also kuinusur CCM!.
Naomba nikupe hizi tip tatu uzifanyie kazi...
  1. Matibabu: Akiwa spika, matatizo madogo madogo na magonjwa madogo madogo, akienda hospitali, husisitiza asipewe dawa za hospitalini, na badala yake aandikiwe tuu prescription ya dawa na dawa za kujitibia atanunua mwenyewe toka kwenye maduka ya dawa, na ofisi ya bunge italipia!. Sasa fanya utafiti toka ofisi ya bunge, hizo dawa alizinunua toka duga gani specific, linalomilikiwa na nani, na kikubwa zaidi, find out ghara za hizo dawa zilizolipwa na ofisi ya bunge!.
  2. Nyumba:Kipindi cha usipika alipangiwa kuishi nyumba nzuri tuu ya serikali, zile zenye hadhi kama za mawaziri!, Jamaa aligoma kuwa nyumba hiyo haina hadhi ya kuishi spika, kwa hoja kuwa kwenye hiearachi ya utawala, wakuu wa mihimili mitatu ya dola, wana hadhi sawa, yaani mkuu wa the executive, the judiciary na the legislature wanatakiwa kuishi nyumba zenye hadhi ya nafasi zao!, hivyo akaruhusiwa kutafuta nyumba ya kupanga ya hadhi yake na serikali itailipia!. Jamaa alitafuta nyumba ya kupanga yenye hadhi ya kukaa spika ikapatikana, kodi ya pango ni doleri 10,000 za kimerekani kwa mwezi!. Serikali ililipia nyumba hiyo!, find out mmiliki halisi wa nyumba hiyo yenye hadhi ya kuish spika ni nani, ambaye ndiye aliyelipwa hiyo kodi ya pango!.
  3. Gari: Kwa kawaida serikali inavyo viwango tofauti vya magari kwa viongozi tofauti, hadhi ya gari ya spika ilikuwa ni sawa na hadhi ya gari ya Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Makamo wa rais. Jamaa alipoingia alilikataa gari alilopewa eti lina hadhi ya chini, gari hilo ni Mercedes Benz S Class ya 350, yeye akataka S Class 500! yenye hadhi kama benzi ya rais!. Find ou from ofisi ya bunge hivo benzi S Class 500 kwa sasa iko wapi?. Anna Makinda baada ya kuchaguliwa, amenunuliwa benzi nyingine mpya S Class 350!.
Nakuomba ukiisha yapata majibu ya hizo tip tatu, please just kaa nayo fyi only na usiyalete humu, kwa sasa acha tuendelee kumpigania Siita awe Mwenyekiti wa kudumu wa bunge letu maalum, hata mimi nimemfungulia uzi maalum kumkapenia
Ni Busara Wajumbe Wote Wa Bunge la Katiba, Kumuunga Mkono Sitta

NB. Kuna watu ndani ya CCM ukiwaweka kwenye mizania ya uadilifu na EL, utashangaa kumkuta kumbe EL ni kama malaika!, wee acha tuu!

Pasco.
 
sita.jpg

Dodoma. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) amesema ameupokea kwa furaha, uteuzi na uamuzi wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wa kugombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.

Lissu amesema uadilifu na misingi mizuri aliyonayo Sitta itasaidia kupata Katiba ya wananchi badala ya ile ya masilahi ya chama au ya kundi la watu wachache.

Tundu alisema kwa kuzingatia hayo, hakuna sababu ya watu wengine kutamani kiti hicho kwa sababu wakiingia katika uchaguzi, wataangushwa na Sitta.

“Kwanza niseme kuwa mimi Lissu kwa mtazamo wangu binafsi, nakubaliana na uamuzi wa mzee yule (Sitta), hakuna mtu wa kuliweza Bunge hili zaidi yake na kwa vyovyote vile, mambo yatakuwa mazuri mbele yake,” alisema Lissu.Alisema katika kipindi ambacho aliongoza Bunge la Tisa, watu wote walimkubali na kuamini kuwa angeweza kuwa kiongozi bora wa Bunge la sasa, lenye changamoto kubwa.

Akizungumzia tetesi kuwa Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ameonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo, alisema hayuko tayari kumuunga mkono.

Lissu alisema Chenge hataweza kuliongoza Bunge hilo na kwamba kama atachaguliwa, litavunjika likiwa mikononi mwake.

Kuhusu Samia Suluhu Hassan anayetajwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti , alisema hana shaka pia ingawa hajaonyesha makeke yake mbele ya vikao muhimu kama vya Bunge, lakini ni mzoefu wa muda mrefu serikalini na katika nafasi mbalimbali.

chanzo:Mwananchi

Samia Suluhu hafai, na wamuweke huyo mzee Kificho. Kama hapana budi basi awekwe Katibu wa BLW. Yahya Khamis
 
Back
Top Bottom