Lissu apiga kura uchaguzi TLS akikumbuka alivyopigwa risasi

Lissu apiga kura uchaguzi TLS akikumbuka alivyopigwa risasi

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ameshiriki kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaoendelea jijini Dodoma huku akikumbushia namna alivyopigwa risasi miaka saba iliyopita.

Lissu ambaye ni mwanasheria, amesema hayo leo Ijumaa Agosti 2, 2024 jijini Dodoma alipozungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya kupiga kura na kueleza namna uchaguzi huo ulivyo muhimu kwa mustakabali wa nchi.

“Siku ya leo inanikumbusha mambo mengi sana, mara ya mwisho kulikuwa na mawakili wakichagua namna hii na ambayo nilishiriki mimi Machi 18, 2017 siku niliyokuwa nagombea urais nilipigiwa kura kama hivi Arusha. Miezi mitano baadaye nikapigwa risasi hapa Dodoma, sijashiriki tena kwenye shughuli kama hii mpaka leo, kwa hiyo inanikumbusha mengi sana ya miaka ile.
 
Back
Top Bottom