Pre GE2025 Lissu apinga tuzo aliyopewa Samia na kusema kuwa huo haukuwa uamuzi wa Chama bali maamuzi binafsi ya Mwenyekiti, ataka ahojiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wadau hamjamboni nyote?

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kiswahili

Jambo TV

Akizungumza kupitia mtandao wa Clubhouse usiku huu, Lissu ameeleza kuwa Rais Samia alialikwa na Mbowe kushiriki katika mkutano wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), na walijulishwa tu kuwa mwaliko huo umetoka kwa Mwenyekiti.

Ameongeza kwa kusema kuwa, walishangaa kuona tuzo ikitolewa kwa Rais Samia bila kujulishwa mapema, huku kamati kuu ya chama hiyo ikiwa haijakaa kujadili suala hilo.

"Yalikuwa ni maamuzi ya Mwenyekiti pekee yake kwa haya mambo mawili. Hakuna kikao kilikaa kamati kuu kumwalika Rais Samia au kumpa tuzo," alisema Lissu, akimtaka Mwenyekiti Mbowe kuhojiwa kwa nini alitoa tuzo hiyo na kumleta Samia, wakati chama cha CCM kilikuwa hakijakubali chochote kuhusu maridhiano kati ya pande hizo.

Lissu amekumbusha kwamba masharti ya mwanzo ya maridhiano kati ya CHADEMA na Serikali yalikuwa na vipengele maalum, na kwamba anajiuliza ikiwa hatua ya kutoa tuzo kwa Rais Samia ni matokeo ya maridhiano hayo.?

Tuzo hiyo, aliyopewa Rais Samia Suluhu Hassan, ilitolewa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) mnamo Machi 08, 2023, kwa kumpongeza kwa juhudi zake za kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini, huku akihusishwa na amani, upendo, na mshikamano.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Samia na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa niaba ya BAWACHA wakati wa Kongamano la Siku ya Wanawake lililofanyika mjini Moshi.
Tuzo ilitolewa na BAWACHA lakini wa kukabidhi alikuwa Mbowe! Kwa hiyo, siku hiyo Mbowe alikuwa ni kiongozi wa BAWACHA!!
 
Mbowe tapeli sana!

Siku hiyo akajitutumua kutoa hotuba anamnanga Magagufuli eti "never and never again"

Kumbe alikuwa anafurahia kupata uhuru wa kupiga mihela ya mama Abdul!

Pumbavu sana
Mkuu umeandika vizuri,ila punguza ukali wa maneno, ni ombi tu sio lazima
 
Sijaona shida mpaka hapa mkuu,huyu ndie, kama tunaamini kuwa mwenyekiti lazima kuwa na usiri katika mambo ambayo hayaitji usiri ,tutakuwa niwajinga sana
Hizo ni akili za wana JF

Lakini sio mambo yanavyofanyika kwenye dunia ya siasa na serikali.

Serikalini na kwa nafasi za juu ndani ya chama ‘lazima ujue kuchunga ulimi wako’

Kuna nafasi unakuwa siri nyingi au uelewa wa mambo mengi ya ndani.

Huwezi kuropoka, Lissu hafai kuiongoza CDM jamaa ropo-ropo sijaona.

Hafai
 
Lisu anafaa kuwa mwanaharakati moja kwa moja.Hebu aonyeshe sana alichofanya,hii itamsaidia sana.Mwenzake kajieleza yeye Lisu anashutumu sana na kulalamika.Hii inawapa wapinzani wake nafasi ya kutumia.Huwezi kutuhumu kila siku bila kuonyesha mfano wa ulichofanya.Aonyeshe alichofanya hii itamsaidia
 
lissu is not predictable, is more of aggresive,wild goose. ukisema clubhouse ni matahira ni sawa na kusema jf ni matahira ir every other platforms ambazo kuna watu wana m support, not fair at all.
Ulitegemea Kada yeyote wa Ccm aseme nini zaidi ya hivyo. ?! 🙏
 
Hizo ni akili za wana JF

Lakini sio mambo yanavyofanyika kwenye dunia ya siasa na serikali.

Serikalini na kwa nafasi za juu ndani ya chama ‘lazima ujue kuchunga ulimi wako’

Kuna nafasi unakuwa siri nyingi au uelewa wa mambo mengi ya ndani.

Huwezi kuropoka, Lissu hafai kuiongoza CDM jamaa ropo-ropo sijaona.

Hafai
Sio kweli, kwani alichoongea ,kipo na adhali gani kiusalama wa nchi? Nakubali yapo mambo ukiyatamka yanaweza kuwa na adhali kwa usalama wa nchi ,je alichosema lissu kwa usalama wa nchi ipo adhali yoyote?

Unafikili kwa nini viongozi wetu waliopo madarakani na wasiokua madarakani wanalindwa ? Pale halindwi mtu bali inalindwa nchi kwa usalama wa nchi .

Alicho kiongea lissu sio tishio kwa usalama wa nchi ,asikilizwe , Chadema sio nchi ni chama, ccm sio nchi ni chama japo ndo kipo madarakani , Rais ni raia no moja na mwakilishi wa nchi ila sio taifa.

Taifa kwanza mengine badae ,lissu yupo na hoja ,na kwa hoja zake hajavunja sheria yoyote ya kikatiba ,huu ndo ukweli wa Mungu wangu
 
Wadau hamjamboni nyote?

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kiswahili

Jambo TV

Akizungumza kupitia mtandao wa Clubhouse usiku huu, Lissu ameeleza kuwa Rais Samia alialikwa na Mbowe kushiriki katika mkutano wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), na walijulishwa tu kuwa mwaliko huo umetoka kwa Mwenyekiti.

Ameongeza kwa kusema kuwa, walishangaa kuona tuzo ikitolewa kwa Rais Samia bila kujulishwa mapema, huku kamati kuu ya chama hiyo ikiwa haijakaa kujadili suala hilo.

"Yalikuwa ni maamuzi ya Mwenyekiti pekee yake kwa haya mambo mawili. Hakuna kikao kilikaa kamati kuu kumwalika Rais Samia au kumpa tuzo," alisema Lissu, akimtaka Mwenyekiti Mbowe kuhojiwa kwa nini alitoa tuzo hiyo na kumleta Samia, wakati chama cha CCM kilikuwa hakijakubali chochote kuhusu maridhiano kati ya pande hizo.

Lissu amekumbusha kwamba masharti ya mwanzo ya maridhiano kati ya CHADEMA na Serikali yalikuwa na vipengele maalum, na kwamba anajiuliza ikiwa hatua ya kutoa tuzo kwa Rais Samia ni matokeo ya maridhiano hayo.?

Tuzo hiyo, aliyopewa Rais Samia Suluhu Hassan, ilitolewa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) mnamo Machi 08, 2023, kwa kumpongeza kwa juhudi zake za kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini, huku akihusishwa na amani, upendo, na mshikamano.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Samia na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa niaba ya BAWACHA wakati wa Kongamano la Siku ya Wanawake lililofanyika mjini Moshi.
BAWACHA wakiongozwa na BoniYai watamjibu Lisu kama kawaida yao
 
Sio kweli, kwani alichoongea ,kipo na adhali gani kiusalama wa nchi? Nakubali yapo mambo ukiyatamka yanaweza kuwa na adhali kwa usalama wa nchi ,je alichosema lissu kwa usalama wa nchi ipo adhali yoyote?

Unafikili kwa nini viongozi wetu waliopo madarakani na wasiokua madarakani wanalindwa ? Pale halindwi mtu bali inalindwa nchi kwa usalama wa nchi .

Alicho kiongea lissu sio tishio kwa usalama wa nchi ,asikilizwe , Chadema sio nchi ni chama, ccm sio nchi ni chama japo ndo kipo madarakani , Rais ni raia no moja na mwakilishi wa nchi ila sio taifa.

Taifa kwanza mengine badae ,lissu yupo na hoja ,na kwa hoja zake hajavunja sheria yoyote ya kikatiba ,huu ndo ukweli wa Mungu wangu
Either unapotosha au hujui unachoongea.
 
Wewe mwenye akili timamu nitajie hayo madudu 3 tuu aliyofanya Ili tujue.
Mbona Bawacha hamkuwachukulia hatua walivyochoma vitenge vya picha ya Samia kama yule kijana wa Mbeya alichoma picha ya mama yenu akakamatwa ?
 
Baada ya uchaguzi namwona Lissu akipeperuka zake. Aidha kuhama chama au kutokomea zake ulaya. Hela anayo tayari
 
Hahaha nahisi ukijua saana sheria unaweza kuwa mwehu na bado wakakushangilia.
 
Back
Top Bottom