SI KWELI Lissu asema hawawezi kuzuia Uchaguzi Sababu wamechelewa, pia wameamua kuachana na 'No reform no Election'

SI KWELI Lissu asema hawawezi kuzuia Uchaguzi Sababu wamechelewa, pia wameamua kuachana na 'No reform no Election'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Naombeni ufafanuzi wa hii watu wa JamiiCheck. Naona Lissu na CHADEMA yake wanatuchanganya sana. Siamini kama kasema haya, nisingempigia kura kabisa.
LISSU_JAMBO_TV_4MAR25 (1).jpg
LISSU_JAMBO_TV_4MAR25 (2).jpg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mnamo tarehe 02 Machi 2025 pamoja na viongozi wengine wa chama hicho walifanya mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) makao makuu ya Chama.

Pamoja na mambo mengine katika mkutano huo Lissu alisisitiza umuhimu wa mabadiliko ya kikatiba kuelekea uchaguzi mkuu 2025 ili kuchochea uwepo wa uchaaguzi huru na haki. Kumekuwapo taarifa zinazosambazwa mtandaoni kutokana na mkutano huo ambazo zimekuwa na lengo la kupotosha.

JamiiCheck inakukumbusha kufanya uthibitisho wa kila taarifa unayoipata kabla ya kuiamini na kusambaza kwa wengine. Mfano mzuri mara nyingi kumekuwapo na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikimuhusisha Lissu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya chama chake. Rejea hapa, hapa, hapa na hapa.

Kumekuwapo na taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ikiwa na kichwa cha habari 'Lissu asema hatuwezi kuzuia uchaguzi huu kwa sababu tumechelewa'

Uhalisia kuhusu taarifa hiyo.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa chapisho hilo si la kweli, limetengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Jambo TV.

Hata hivyo katika mkutano huo Lissu alisema "Bila mabadiliko hakuna uchaguzi na siyo bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi, hiyo siyo lugha yetu, lugha yetu ni bila mabadiliko uchaguzi hautafanyika, ndiyo lengo letu."

Aidha Chapisho lingine lilimhusisha Lissu kuwa amesema msimamo wa No Reforms, No Election umefeli hivyo wameamua kuachana nao.

Uhalisia wa Chapisho hilo.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa chapisho hilo si la kweli, limetengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Jambo TV.

Hata hivyo Lissu hakutoa kauli yoyote kuashiria kuachana na ajenda hiyo bali alisema "tumesema siyo hatutasusia uchaguzi, tutazuia uchaguzi, lugha siyo kususia uchaguzi lugha ni kuzuia uchaguzi, na tumesema tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma, tutawaalika Watanzania wahakikishe uchaguzi huu haufanyiki."
Back
Top Bottom