Pre GE2025 Lissu ataka mabalozi wa nchi mbalimbali wawepo kama waangalizi wa Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ili "kuongeza macho"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wowote wale atakaoona wanafaa si Kila mtu anatakiwa kushinda mechi zake au?
 
Mbowe atakubali haya masharti. Hapo ndipo Lissu atasogeza tena magoli. Anaweza kudai wanao hesabu kura wasivae nguo zozote na wasiwe na nywele ndefu.

Amandla...
Hili siyo suala la Mbowe kukubali ama la! Ombi hili Lisu amelitoa kwa wazee na washauri washauri wa chama. Sijajua hawa wanatumikaje huko chadema
 
Ili wamsaidie nini Sasa?


Sawa watakuja ila na Mbowe akiamua kuleta watu wa Serikali kuwa waangalizi asije kuanza kupayuka kama mwehu.
Watu wa serikali wapo indirectly.Wewe hujui kwanini jamaa anaogopwa na system.
 
Wowote wale atakaoona wanafaa si Kila mtu anatakiwa kushinda mechi zake au?
Jaribuni muone..

Mwamba huyu mwaka 2017 (uchaguzi wa TLS) wakati wa Jiwe Pombe Magufuli mlitumia njia hizihizi kuhakikisha hawi Rais wa TLS, mliweza..?

Mlishindwa vibaya na jamaa akawapiga kwa TKO...

Mlipoona hivi, mkaja na option ya kumuwinda kwa bunduki za SMG na AK47, risasi 16 zikaingia mwilini, hazikuondoa uhai wake...

Hujiulizi tu huyu ni mtu wa namna gani..?

Mbona mko kama wale Wayahudi wajinga waliomtungia mashitaka ya uhaini wa uongo Yesu Kristo, akahukumiwa adhabu ya kifo, akawaambia siku ya tatu nitafufuka na ndio mwisho wa mambo yenu, na bado alipofufuka, wakamuona kwa macho yao lakini bado wakaendelea kuwa wajinga tu...?

Kwanini nanyi mu wajinga kiasi hiki? Wewe ChoiceVariable unaweza kupona kweli hata ukipigwa na Jiwe dogo tu la manati matakoni mwako..?

Acheni kuwa wajinga. Acheni kupambana na wakati wa Mungu. Alilopanga <Mungu liwe, hakuna wa kuzuia..

Njooni siku hiyo TISS na UVCCM wote muone mtavyoaibika...
 
TLS Haina maslahi yeyote ya maana na Serikali.

Hata huo uchaguzi wenu Serikali itaangalia kipi kinafaa maana hata Sasa Mwabukusi ni Rais wa TLS sawa na alivyokuwa Lisu je Kuna Cha maana walibadilisha? 😆😆
 
Reactions: Tui
Maonyesho ya mtu mweusi hasa mtanzania ni vituko na burudani
 
M

Muungwana na mkweli akishindwa hukubali haraka. Asikilizwe ili kuziba kelele. Waalikwe tu. Na Mbowe akiomba jambo la wazi naye asikilizwe halafu matokeo yawekwe hadharani , kwani nini tatizo.
Ndivyo inavyopaswa iwe. Lakini watu wakianza kusema " kama uchaguzi utakuwa wa haki mtu wetu atashinda" hao wanaonyesha kuwa lengo lao ni mgombea wao ashinde kwa namna yeyote ile. Na mgombea nae akisema " nitakubali matokeo pale tu uchaguzi ukiwa huru na wasi" anapanda mbegu za kukataa uchaguz kama hatapendezwa na matokeo. Hii mbegu inamwagiwa maji na wapambe wake na uchaguzi ukifika itabaki kuvuna tu. Ubaya wa hiki wanachofanya ni kufanya watu watilie shaka zote za huko mbele hata yeye akiwa Mwenyekiti. Anachokifanya hakina tija kwa chama lakini inaelekea afya ya chama sio priority kama yeye kushinda.

Amandla...
 
Reactions: Tui
Hiyo ni sawa , Kama unapewa na kukubali kula pesa yao we kubali na kupekuliwa
 
Hili siyo suala la Mbowe kukubali ama la! Ombi hili Lisu amelitoa kwa wazee na washauri washauri wa chama. Sijajua hawa wanatumikaje huko chadema
Kama alivyotoa yeye ombi hilo, Mbowe nae anaweza kutoa ushauri unaopingana na huo. Kitu muhimu ni wagombea wote ( sio Mbowe na Lissu tu) waridhike na taratibu zitakazowekwa.

Kwa vile inaelekea ombi hilo amelitoa hadharani inaonekana ni kama njia ya kuwa pressurize ili wakubaliane nae.

Amandla...
 
Reactions: Tui
Inanesha Mbowe ana tabia mbaya (za wizi wa kura) ndiyo maana makamu wake anajihami.
 
It’s obvious dude is compromised

It’s beyond me to those who think he is the messiah they’ve been waiting for.

Sakata la makanikia lilionyesha huyu ni mtu wa aina gani.

Compromised
 
Mungu amlinde Sana lissu, uwazi na uadilifu ndo sifa yake kuu.Huyu ndo kiongozi anayefaa kwa sasa kwa taifa letu
 
Kwa wakati huu chadema inamtihani wa kuonyesha kwa vitendo vile vitu wanavyovipinga kwenye uchaguzi wetu wa nchi, kura zipigwe kwa uwazi, mchana kweupe, wajumbe waitwe mmojammoja kwenda kupiga kura, zihesabiwe sehemu ya wazi nk.
 
Inanesha Mbowe ana tabia mbaya (za wizi wa kura) ndiyo maana makamu wake anajihami.
Leta mfano lini Mbowe aliiba kura?Wacheni ujinga na ushabiki wa kipumbavu. Asipopingwa huyu mwisho atadai VAR.
Kwani sasa hivi haiamini Kamati ya Uchaguzi wala Kamati Kuu wala wagombea huku anataka achaguliwe.Vioja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…