Uchaguzi 2020 Lissu awasha moto Morogoro: Umma wampokea kwa kishindo

Uchaguzi 2020 Lissu awasha moto Morogoro: Umma wampokea kwa kishindo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Vijana walisema kitimutimu kimeingia leo, kwenye myumba ya Shetani Mwendawazimu kaingiaje?

Kweli msemo huo wa vijana ulikuwa na maana pana ya kifalsafa ndani yake. Jana Tundu Lissu katia timu katika ngome ya CCM ya Morogoro mjini na kisha kwenye Jimbo la Mikumi lililo chini ya profesa J na kuwasha moto mkali sana.

Akiwa Mikumi Lissu alizungumza juu ya uhuru na dhana ya uhuru. Akasema pamoja na hitajio la watu kufanya kazi kama serikali hii inavyojinadi, watu pia ni lazima wawe huru.

Akasema kufanya kazi kama manamba bila kuenjoy uhuru ni mambo ya kikoloni ambapo walikuwa wakiwafanyisha kazi manamba bila uhuru.

Lissu akasema Miundo mbinu ambayo Magufuli anajitapa nayo, siyo yeye wa kwanza kuanza kuijenga maana hata maraisi waliopita kila mmoja alijenga miundo mbinu kulingana na wakati husika, na pia hatokuwa mwisho kujenga maana hata serikali zijazo nazo zitajenga kwa kuwa kujenga miundo mbinu ni kazi basic ya serikali yoyote ile duniani!

Kwa nondo zaidi msikilize wewe mwenyewe hapa:

Morogoro Mjini sijui huwa wanafeli wapi, wamezoea kumpa kura yule jamaa miaka yote kisa huwa anawasaidia kuwazika ndugu zao, yaani akili za watu huwa zinatekwa kirahisi sana.
 
Morogoro Mjini sijui huwa wanafeli wapi, wamezoea kumpa kura yule jamaa miaka yote kisa huwa anawasaidia kuwazika ndugu zao, yaani akili za watu huwa zinatekwa kirahisi sana.
Eti huwa anawapungizia nauli, wabongo bana sijui akili zao zinakuwaje tu
 
Morogoro Mjini sijui huwa wanafeli wapi, wamezoea kumpa kura yule jamaa miaka yote kisa huwa anawasaidia kuwazika ndugu zao, yaani akili za watu huwa zinatekwa kirahisi sana.
Kukosa elimu bora na maarifa ndio tatizo la watanzania walio wengi wakiwemo baadhi ya ma-professors!
 
Morogoro Mjini sijui huwa wanafeli wapi, wamezoea kumpa kura yule jamaa miaka yote kisa huwa anawasaidia kuwazika ndugu zao, yaani akili za watu huwa zinatekwa kirahisi sana.
Umasikini wa akili unawasumbua hao, wanaamini mwarabu anaweza kuwaleteea maendeleo
 
Back
Top Bottom