Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kuna uwezekano kuna watu au kikundi cha watu au Wafuasi wa lissu wakawa na matumaini na matarajio makubwa sana na lissu kwamba anaweza badilisha au lazimisha kufanyika kwa jambo lolote lile analotaka au wanalolitaka wao kwa nguvu au mabavu au kwa shinikizo.
Nipende tu kuwaambieni ukweli mchungu kuwa iwe leo au kesho au kesho kutwa Lissu hana ubavu wala uwezo wala nguvu wala maamuzi ya kufanya jambo lolote lile kubwa liwe la kimfumo au kisheria au kisera pasipo kwanza kukaa kwenye meza ya mazungumzo na CCM na serikali yake.
Ili jambo lolote lifanyike ni sharti CCM iridhie na kukubali. Kwa sababu CCM ndio chama kilichojitawala ndani ya Bunge na kwingine kote kwenye ngazi za uwakilishi.
Kwa hiyo unaposema unataka mabadiliko ya aina yoyote ile iwe ni kisheria au kisera .maana yake unapaswa kujenga hoja na kuridhiana na CCM na serikali yake ambayo ndio yenye wabunge wengi ndani ya Bunge letu.
Mbali na hapo ni kuwa lissu ataishia kupiga makelele yake mpaka achoke na Mwisho wa siku hakuna kitakachobadilika hata kwa herufi moja au tarakimu moja.
Akija kibabe basi CCM tutamkabili na kupambana naye katika namna hiyo hiyo atakayo kuja nayo. Akija kiungwana tutampokea kwa namna hiyo hiyo na kukaa naye mezani kumsikiliza. Akija kwa Shari na chuki basi awe tayari kupata majibu ya aina hiyohiyo.
Hii ni kwa kuwa CCM ndio chama kilichopewa ridhaa na watanzania ya kuwaongoza.Muongozo wa CCM ilikuwa ni ilani yetu ambayo ndio tuliyoinadi kwa wananchi. kwa hiyo kilichopo kwenye ilani yetu ndicho tunachokitekeleza. Kama wewe mwingine una jambo lako basi subiri uchaguzi na nenda kwa wananchi uombe kura zikitosha ndio utekelezage hicho unachokitaka wewe.
Lakini kwa sasa kwa kuwa sisi ndio wenye serikali hivyo huna budi kuja mezani na hoja zenye mashiko ili nasi tukupe hoja zetu juu ya kipi kinawezekana kwa wakati huu na kipi hakiwezekani kwa sasa na kingoje muda fulani au wakati. Mkataba wetu na wananchi ni Ilani ambayo ilichaguliwa na wananchi. tuulizwe na kushinikizwa kutekeleza kilicho kwenye ilani yetu .
Ila kile ambacho hakipo kwenye ilani yetu ni sharti kije kwa njia ya kufanya Mazungumzo na maridhiano. na katika mazungumzo na maridhiano ni lazima uelewe hutapata yoote unayoyahitaji. Bali yapo mengine utapata na mengine utapata kiasi na mengine itabidi usubiri wakati wake ufike.
Kwa hiyo lissu akijifanya kuongozwa na Mihemuko pasipo kutumia akili, busara ,hekima , utulivu, subira na uvumilivu. Basi atakosa yoote na hatakuwa na cha kutufanya wala kufanya wala kubadilisha kitu chochote kile ndani ya katiba au sheria zetu. Kwa hiyo ni lazima aje kwa nidhamu ,hekima na utayari wa kukaa mezani.
Lakini asije na majibu yake mfukoni au Misimamo. Majibu yatapatikana katika meza ya mazungumzo na kuwa na msimamo wa pamoja wa namna ya kusonga mbele kwa pamoja kama Taifa .
CCM ni kama maji usipoyanywa utayaoga tuuu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.