Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Ndugu zangu Tlaatlaah johnthebaptist FaizaFoxy Lucas Mwashambwa na genge lenu bado mnaona Lissu 'anaropoka' au dawa ishaanza kuwaingia?

Ila kwa jinsi vyombo vya habari vinavyolipwa kumchafua Lissu sasa hivi mtakuwa mna mhaho wa hatari!
=====
Lissu anasema kwa 78% ya kura zake walizopata, CCM ilistahili kupata wabunge 88 wa viti maalumu, lakini wakihesabiwa wako 94.
Lakini pia CHADEMA ilipata 16% ya kura zote halali za wabunge, ambapo walistahili kupata viti vya wabunge 18, mmoja alitoka wapi mpaka wamefikia 19?
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Sasa hili lilitokeaje?
Kura za vyama vidogodogo ambavyo havifikishi 5% zinakusanywa pamoja, zikikusanywa pamoja zinazidi 5% halafu wanafanya idadi ya wabunge wanaoweza kupatikana kutokana na idadi ya kura walizopata.
Kwa uchaguzi wa 2020 jumla ya kura za vyama vidogovidogo ilikuwa 6% na kwa hiyo kanuni ya 5% ya kura ikupatie wabunge wa viti maalum kuna jumla ya viti 7 vya wabunge wa viti maalum ambavyo vilipaswa viende kwenye hivi vyama vidogo vidogo kama wangepata kura zilizofika idadi halali ya kura ingewawezesha kuapata wabunge.
Hivyo kwakuwa vyama hivyo havikufikisha 5% ya kura havikupata hata kiti kimoja. Tume ilichofanya, kwenye viti hivyo 7 ikaipa CCM 6 na mmoja akaongezewa CHADEMA! Covid 19 ilikuwa waitwe Covid 18!
Lissu ameongeza kuwa hizi ndio rafu zinazofanyika kila mwaka wa uchaguzi kwa wao kunyimwa haki ya kuwa na wabunge halali lakini pia ruzuku wanayostahili na kwamba bila kufanya mabadiliko hali hii itaendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatano Februari 12, 2025.
Pia soma