LGE2024 Lissu: CHADEMA tunahitaji kurudi nyuma na kujipanga upya, kwenda mbele kwenye mazingira haya ni kujihahakishia anguko

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wakati akijibu swali la mwandishi kwenye mkutano wake na waandishi Singida; (Uchaguzi umekwisha wanatakiwa wajipange upya, je, wanaimba mwimbo mmoja) Tundu Lissu amesema;

======

"Mimi napenda kuamini tunaimba wimbo mmoja, kama hatuimbi wimbo mmoja basi tutakuwa na hali mbaya sana. Kama hatuwezi kukubaliana kwamba Samia anahitaji kukabiliwa kwa pamoja na kauli moja na sisi wote, kama kuna wanaofikiria wataenda mafichoni kukutana na Samia na kuteta, tutakuwa na hali mbaya sana, mimi naogopa.
Kupata nyuzi kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

"Kwenye masuala ya msingi kama haya tunahitaji kuwa na kauli moja, na kauli haiwezi ikawa twende tu, kauli inatakiwa iwe tujipange upya. Kwa uchaguzi huu tunahitaji kurudi nyuma kujipanga upya, turudi nyuma kimkakati.

"Kwenda mbele katika mazingira haya ni kujihakikishia anguko mbele."
 
Wakuu,

Wakati akijibu swali la mwandishi kwenye mkutano wake na waandishi Singida; (Uchaguzi umekwisha wanatakiwa wajipange upya, je, wanaimba mwimbo mmoja) Tundu Lissu amesema;

======

View attachment 3150237

Mimi napenda kuamini tunaimba wimbo mmoja , kama hatuimbi wimbo mmoja basi tutakuwa na hali mbaya sana. Kama hatuwezi kukubaliana kwamba Samia anahitaji kukabiliwa kwa pamoja na kauli moja na sisi wote, kama kuna wanaofikiria wataenda mafichoni kukutana na Samia na kuteta, tutakuwa na hali mbaya sana, mimi naogopa.

Kwenye masuala ya msingi kama haya tunahitaji kuwa na kauli moja, na kauli haiwezi ikawa twende tu, kauli inatakiwa iwe tujipange upya. Kwa uchaguzi huu tunahitaji kurudi nyuma kujipanga upya, turudi nyuma kimkakati.

Kwenda mbele katika mazingira haya ni kujihakikishia anguko mbele
Lissu ndiye anasababisha kukosa upamoja wa kukabiliana na Samia kwa vile yeye anataka kugombea Urais na anaamini yeye ndiye bora kuliko wengine

Bado Lissu huyu huyu ndiye aliye haribu maridhiano ambayo Samia alikuja na 4R. Alianza kuyaponda majukwaaani wakati wenzie wanaendelea. Wakati huo 50% ya matakwa ya CHADEMA yalishakubaliwa na Samia.

Sera ya winner takes all ndiyo iliyoharibu maridhiano kwa vile Lissu alikuwa anataka Samia apokee matakwa yao yote.

Mbona ACT wanafanya siasa bila matusi kwenye majukwaa? Tusishangae miaka 15 baadaye ACT ikawa chama kikubwa cha upinzani nchini
 
Lissu anayo elimu dunia sio kama wale vilaza wakiongozwa na Lema na Mdude
 
Lissu ndiye anasababisha kukosa upamoja wa kukabiliana na Samia kwa vile yeye anataka kugombea Urais na anaamini yeye ndiye bora kuliko wengine

Bado Lissu huyu huyu ndiye aliye haribu maridhiano ambayo Samia alikuja nan4R. Alianza kuyaponda majukwaaani wakati wenzie wanaendelea. Wakati huo 50% ya matakwa ya CHADEMA yalishakubaliwa na Samia.

Sera ya winner takes all ndiyo iliyoharibu maridhiano kwa vile Lissu alikuwa anataka Samia apokee matakwa yao yote.

Mbona ACT wanafanya siasa bila matusi kwenye majukwaa? Tusishangae miaka 15 baadaye ACT ikawa chama kikubwa cha upinzani nchini
Acheni kumwangushia gari Bovu msomi Lissu,Mzee Mbowe ndio anastahili lawama zote ,leo chadema kina wasemaji aina ya Mdude kweli?
 
Wakuu,

Wakati akijibu swali la mwandishi kwenye mkutano wake na waandishi Singida; (Uchaguzi umekwisha wanatakiwa wajipange upya, je, wanaimba mwimbo mmoja) Tundu Lissu amesema;

======

View attachment 3150237

Mimi napenda kuamini tunaimba wimbo mmoja , kama hatuimbi wimbo mmoja basi tutakuwa na hali mbaya sana. Kama hatuwezi kukubaliana kwamba Samia anahitaji kukabiliwa kwa pamoja na kauli moja na sisi wote, kama kuna wanaofikiria wataenda mafichoni kukutana na Samia na kuteta, tutakuwa na hali mbaya sana, mimi naogopa.

Kwenye masuala ya msingi kama haya tunahitaji kuwa na kauli moja, na kauli haiwezi ikawa twende tu, kauli inatakiwa iwe tujipange upya. Kwa uchaguzi huu tunahitaji kurudi nyuma kujipanga upya, turudi nyuma kimkakati.

Kwenda mbele katika mazingira haya ni kujihakikishia anguko mbele
Inavyoonekana Kuna mvurugano ndani ya Chadema. Kiini cha kuwepo kwa mvurugano huu huko Chadema kwa maoni yangu ni kutokana na namna Mwenyekiti wa Chama chao hicho Freeman Mbowe kukosa misimamo inayoeleweka kuhusiana na Siasa za nchi hii kwa sasa. Siyo siri hata kidogo, Mbowe akiwa Kama Kiongozi wa Chama Chao hicho, amekuwa ni mtu ambaye Hana msimamo unaoeleweka hali hii imesababisha mkwamo na kuyumba kwa Wanachama wa chama hicho.

Mbowe amekuwa ni mtu asiyeaminika tena kwa sasa ndani ya Chama Chao hicho, watu wengi kwanza wanamchukulia kama ni Mamluki wa Chama tawala ambaye amejipachika kwenye Vyama vya upinzani kwa 'kazi maalumu ya kuvuruga vyama vya upinzani' ili kukinufaisha chama tawala.

'Engine' ya treni ikiharibika mabehewa yote ya treni nayo huyumba na kusimama!
 
Lissu ndiye anasababisha kukosa upamoja wa kukabiliana na Samia kwa vile yeye anataka kugombea Urais na anaamini yeye ndiye bora kuliko wengine

Bado Lissu huyu huyu ndiye aliye haribu maridhiano ambayo Samia alikuja nan4R. Alianza kuyaponda majukwaaani wakati wenzie wanaendelea. Wakati huo 50% ya matakwa ya CHADEMA yalishakubaliwa na Samia.

Sera ya winner takes all ndiyo iliyoharibu maridhiano kwa vile Lissu alikuwa anataka Samia apokee matakwa yao yote.

Mbona ACT wanafanya siasa bila matusi kwenye majukwaa? Tusishangae miaka 15 baadaye ACT ikawa chama kikubwa cha upinzani nchini
Uzuri wa Lissu siyo Mnafiki!
ACT=CCM B
 
Lissu na ubinafsi wake hajali huu uchaguzi wa serikali za mitaa maana yeye hagombei. Anasema tujipange upya kwa vile 2025 apete. Kwanini kama kuna mapungufu wasiombe zoezi kurudiwa
 
Naona Lissu anatupa taulo, kabla hata mechi haijaanza, TKO ya mwamba wa kizimkazi
 
Lissu ndiye anasababisha kukosa upamoja wa kukabiliana na Samia kwa vile yeye anataka kugombea Urais na anaamini yeye ndiye bora kuliko wengine

Bado Lissu huyu huyu ndiye aliye haribu maridhiano ambayo Samia alikuja nan4R. Alianza kuyaponda majukwaaani wakati wenzie wanaendelea. Wakati huo 50% ya matakwa ya CHADEMA yalishakubaliwa na Samia.

Sera ya winner takes all ndiyo iliyoharibu maridhiano kwa vile Lissu alikuwa anataka Samia apokee matakwa yao yote.

Mbona ACT wanafanya siasa bila matusi kwenye majukwaa? Tusishangae miaka 15 baadaye ACT ikawa chama kikubwa cha upinzani nchini
Kwamba ccm yenyewe itaendelea tu kuwa chama tawala, ila nafasi ya chama kikuu cha upinzani itakuwa ya ACT! Kwa uchaguzi gani boss unaofanyika hapa nchini hadi ufikie hitimisho hilo? Kwani hayo maridhiano yalikiwa ya kitaasisi au ni ya Lisu hadi urushe lawama kwake?
 
Back
Top Bottom