Mathayo Fungo
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 319
- 511
Imeandaliwa na Umoja wa Wamachinga Iringa
Kauli ya mgombea urais wa CHADEMA, Tundu Lissu kuahidi kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kwenye mitaa mbalimbali ya miji na majiji tunaipinga vikali kwasababu inataka kutuingiza kwenye umasikini.
Katika kampeni zake, Lissu alisema kuwa wamachinga wamekuwa wakifanya biashara katika mitaa na kuzuia hadi maduka ya watu. Kwamba akiingia atawahamisha mitaani ili akawajengee nje ya mji.
Alipoingia madarakani Rais Magufuli aliamua kubuni mbinu ya kuwarasimisha wamachinga na wengine wakiwemo mama na babalishe ambao mitaji yao iko chini ya shilingi millioni nne ili wafanye biashara rasmi bila kubughudhiwa na mgambo wa miji na majiji lakini Lissu anasema atafuta vitambulisho hivyo na kuwaondoa wajasiriamali kutoka maeneo waliopo sasa.
Ahadi hii ya Lissu inadhihirisha jinsi gani asivyo mzalendo na nchi yake kwani alipaswa kufikiri kwa kuzungumza juu ya namna gani atafanya ili kuendeleza hatua nzuri alizotufikishia Rais Magufuli na sio kuja na maneno ya kuturudisha nyuma.
Katika Awamu ya Tano, wamachinga tumepata fursa nyingi ikiwemo mikopo, uhuru wa kufanya shughuli zao na hata bima za afya mambo ambayo hatukuwahi kufikiria kuyapata. Tunajisikia faraja kuwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya nchi kutokana na kodi tunayolipa na kufarijika kuona huduma mbalimbali za kijamii zinaboreshwa kupitia hili.
Sisi tutaendelea kuunga juhudi za Rais Magufuli na Serikali ya CCM kwani imekuwa ikitusikiliza na kushirikiana nasi katika kutatua kero zetu. Tutailinda misingi ya uzalendo iliyootoshwa na Serikali kwetu wamachinga, katu Lissu hatoweza kuivunja kwani imeota mizizi.