Lissu: Kama Mbowe ametoa mabilioni kwenye chama aoneshe documents, hakuna fedha ya chama inayoweza kutumika bila nyaraka za kuthibitisha

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Tundu Lissu ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa, ametoa wito kwa Freeman Mbowe, kueleza kwa uwazi kuhusu madai ya kutumia mabilioni ya fedha ndani ya chama.

Akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa Clubhouse, Lissu amesema kuwa, Mbowe amekuwa na mchango mkubwa kwa chama kwa kusaidia kifedha, ikiwemo kutoa mikopo iliyosaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za chama.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kila matumizi ya fedha ndani ya chama yanapaswa kuwa na nyaraka za kuthibitisha.

“Ni kweli mwenyekiti wetu Mbowe amekisaidia sana chama. Alitukopesha fedha na tukazilipa kupitia ruzuku za chama. Hata chopa tulizoamua kama chama zitumike, tulishalipa zote,” alisema Lissu.

Lissu ameongeza kwa kusema kuwa, hana taarifa za kina kuhusu madai ya mabilioni yaliyotumika zaidi ya gharama zilizojulikana na kukubaliwa na chama.

“Sasa nasikia kuna mabilioni ametumia, sijui ni yapi hayo. Lakini ninavyojua, gharama zililipwa kutokana na kile tulikubaliana kama chama,” alibainisha.

Akizungumzia uwazi wa matumizi ya fedha za chama, Lissu amesisitiza kuwa hakuna fedha inayoweza kutumika bila nyaraka za kuthibitisha.

“Kama kuna mtu ameweka mabilioni kwenye chama, atoe document kuhusu hizo fedha. Hakuna fedha isiyo na document, hakuna fedha ya chama isiyo na document,” alisema kwa msisitizo.

Lissu pia ameeleza kuwa mbali na Mbowe, wanachama wengine wengi wamejitolea na kuwekeza katika chama kwa njia mbalimbali. Hata hivyo, alifafanua kuwa mikopo yote iliyochukuliwa imekuwa ikilipwa kwa uwazi na kufuata makubaliano ya chama.

“Hata sisi wengine tumewekeza kwenye hiki chama. Watu wengi wamekitumikia chama kwa hali na mali, lakini fedha za kukopwa zimelipwa,” aliongeza.

Kauli ya Tundu Lissu inadhihirisha umuhimu wa uwajibikaji wa viongozi katika kudumisha imani ya wanachama na wananchi kwa ujumla kwa kusisitiza uwazi kuhusu matumizi ya fedha huku akisisitiza kwamba mafanikio ya chama yanapaswa kujengwa juu ya misingi ya uadilifu na ukweli.

Hatua hii si tu inalenga kuimarisha mshikamano ndani ya chama, bali pia inatoa mfano wa aina ya uongozi unaohitajika katika kujenga demokrasia imara nchini.

Jambo TV
 
TAL kama vile hajui kama kuna ukaguzi na repoti za CAG kila mwaka.
Hivi kweli anakumbuka ile ndege iliyomtoa Dom hadi Nrb nani alitoa hela kuilipia kwa ajili ya kuokoa maisha yake??
Hakika dunia duara
Jan 21 siyo mbali kivile
 
Kama ameaanza kuwasema vibaya watu waliomsaidia je wale ambao hawakumsaidia itakuaje ?? Huyu hafai kuwa kiongozi !!!
Namkumbusha tu bila ya Mbowe saa hizi angekuwa shimo la tewa !
Nadhani Mbowe anajutaaa kumsaidia mtu kama huyu !
 
Lisu angetulia tu kuna maisha baada ya haya mambo, ni hatari kuendelea kujilimbikizia maadui mwili wenyewe umejaa vyuma tupu.
 
Sisi team Mbowe tinasubiri kuhujumu kura za urais za Lissu come 2025.Hatutazilinda
 
Uzi umejaa maCCM huu. ID mpya hata hazijulikani zimetoka wapi, zote zinadai kumuunga mkono Mbowe
 
Tundu Lissu ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa, ametoa wito kwa Freeman Mbowe, kueleza kwa uwazi kuhusu madai ya kutumia mabilioni ya fedha ndani ya chama.

Akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa Clubhouse, Lissu amesema kuwa, Mbowe amekuwa na mchango mkubwa kwa chama kwa kusaidia kifedha, ikiwemo kutoa mikopo iliyosaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za chama.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kila matumizi ya fedha ndani ya chama yanapaswa kuwa na nyaraka za kuthibitisha.

“Ni kweli mwenyekiti wetu Mbowe amekisaidia sana chama. Alitukopesha fedha na tukazilipa kupitia ruzuku za chama. Hata chopa tulizoamua kama chama zitumike, tulishalipa zote,” alisema Lissu.

Lissu ameongeza kwa kusema kuwa, hana taarifa za kina kuhusu madai ya mabilioni yaliyotumika zaidi ya gharama zilizojulikana na kukubaliwa na chama.

“Sasa nasikia kuna mabilioni ametumia, sijui ni yapi hayo. Lakini ninavyojua, gharama zililipwa kutokana na kile tulikubaliana kama chama,” alibainisha.

Akizungumzia uwazi wa matumizi ya fedha za chama, Lissu amesisitiza kuwa hakuna fedha inayoweza kutumika bila nyaraka za kuthibitisha.

“Kama kuna mtu ameweka mabilioni kwenye chama, atoe document kuhusu hizo fedha. Hakuna fedha isiyo na document, hakuna fedha ya chama isiyo na document,” alisema kwa msisitizo.

Lissu pia ameeleza kuwa mbali na Mbowe, wanachama wengine wengi wamejitolea na kuwekeza katika chama kwa njia mbalimbali. Hata hivyo, alifafanua kuwa mikopo yote iliyochukuliwa imekuwa ikilipwa kwa uwazi na kufuata makubaliano ya chama.

“Hata sisi wengine tumewekeza kwenye hiki chama. Watu wengi wamekitumikia chama kwa hali na mali, lakini fedha za kukopwa zimelipwa,” aliongeza.

Kauli ya Tundu Lissu inadhihirisha umuhimu wa uwajibikaji wa viongozi katika kudumisha imani ya wanachama na wananchi kwa ujumla kwa kusisitiza uwazi kuhusu matumizi ya fedha huku akisisitiza kwamba mafanikio ya chama yanapaswa kujengwa juu ya misingi ya uadilifu na ukweli.

Hatua hii si tu inalenga kuimarisha mshikamano ndani ya chama, bali pia inatoa mfano wa aina ya uongozi unaohitajika katika kujenga demokrasia imara nchini.

Jambo TV
Mbowe amesema wapi kuwa anaidai CDM mabilioni? Lissu atakiri vipi kuwa Mbowe alikisaidia chama halafu ageuke na kusema atoe uthibitisho kuwa kweli alikisaidia chama! Mbowe alisema wazi kuwa wengi wamechangia chama. Amesema kuwa wanatumia pesa zao wenyewe kuendesha baadhi ya shughuli za chama.

Kama Lissu alisema haya, alikosea sana. Ni mfano wa kuchafuana aliozungumzia Mbowe.

Amandla...
 
Back
Top Bottom