Uchaguzi 2020 Lissu, Kiburi si maungwana!

Uchaguzi 2020 Lissu, Kiburi si maungwana!

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
LISSU; KIBURI SI MAUNGWANA!!

Imeandikwa, kiburi si maungwana na mtoto mkaidi hawezi kufaidi hadi siku ya Iddi. Tundu Lissu anaingia ktk kundi hili kwa kushauriwa vibaya au kukaidi ushauri mzuri.

1. Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya NEC anaweza kuendelea na shughuli za Chama kama Makam Mwenyekiti wa Chama amemshauri vibaya.

Tundu Lissu ni mmoja, hakuna nafsi mbili ktk mtu mmoja. Popote atakapokuwa Tundu Lissu ndipo alipo Mgombea wa Urais wa Chadema na Makam wa Mwenyekiti wa Chadema. Hakuna mstari wowote wa kutenganisha kati ya Lissu Mgombea na Lissu M/Mwenyekiti.

Kukosekana kwa tofauti hiyo ndio maana popote alipo mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli ndipo alipo Rais wa JMT. Huwezi kuutofautisha ugombea wa John Pombe Joseph Magufuli na Urais wake au Uenyekiti wake wa CCM. Hivyo hivyo huwezi kuutofautisha ugombea wa Tundu Lissu na Umakam Mwenyekiti wake vinginevyo ni kujidanganya tu.

Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa anaweza kuendelea na kazi za kisiasa amemdanganya, amemshauri vibaya na amempotosha bure. Anachagiza vurumai za bila sababu. Lissu ashauriwe vizuri, ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake ni alfa na Omega, huwezi kuvitenganisha. Kimoja kinaathiri kingine!

2. Aliemshauri Lissu kuwa, kufungua matawi ya Chama au kutembelea masoko sio shughuli za Kampeni amemshauri vibaya, amemdanganya. Ni bahati mbaya kuwa Lissu licha ya kuwa Mwanasheria amedanganyika kirahisi mno. Mazingira na wakati vinanguvu zaidi ktk kuamua kesi, Lissu anafahamu hilo. Hakuna mstari wowote unaotenganisha kufungua matawi ya chama, kutembelea masoko na shughuli za Kampeni kwa wakati huu. Wakati uliopo sasa na mazingira anayokwenda kutembelea Tundu Lissu ni ushahidi wa wazi kuwa ameamua kufanya kampeni kwa mlango mwingine. Ni kosa, ni ukaidi.

Kampeni ni hamasa, kampeni ni ushawishi. Kufungua matawi ya vyama ni hamasa na ushawishi kuwa Chama kipo hai, hii ni kampeni zaidi kuliko kufanya mkutano wa hadhara.
Kuwatembelea watu ktk soko na maeneo ya wazi ni hamasa na ushawishi pia. Watu waliosoma elimu maalumu watanielewa vzr hapa kwamba kuna lugha ya picha na alama. Unaweza kufika mahala bila kuongea jambo lolote, ukasabahi kwa ishara na kuondoka lkn mavazi yako na muda vika-deliver ujumbe uliokusudiwa kwa watu. Kwenda Kibaha, kukutana na Wanachama au Wananchi hata bila kuongea jambo lolote ni kampeni kwa Lissu. Kati ya nafasi ya Umakam Mwenyekiti na nafasi ya Ugombea Urais kwa Lissu inayotangulia kwa sasa ni ya Ugombea. Hii ni principle ya wakati!!

Ushauri:

1. Mwambieni Tundu Lissu akili nyingi mbele ni giza. Awasikilize wenzake, aachane na mpango huu hauna faida. Polisi watamzuia kwa sababu hawawezi kutofautisha Ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake. Sio Polisi tu, hata wewe huwezi kwa sababu hakuna tofauti hiyo.

Polisi ndicho chombo chenye dhamana ya kusimamia na kushurutisha utekelezaji wa sheria. Ninahisi wataendelea na kusimamia utaratibu huu bila kujali kwa sababu ni wajibu wao, tusiwalaumu.

2. Mwambieni Tundu Lissu aache kukifanya kichwa chake kigumu, kitavunjika na asipate dawa. Aache kutukana watu kila kukicha, binadamu tumeumbwa na vinyongo. Siku Polisi wakikinai kuitwa wajinga au siku wakitamani kuufanya ujinga hadharani itakua hatari kwa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sote, tuilinde!!

3. Mwambieni Lissu, walio nyuma yake ni ndugu zake ktk Chama, ndugu zake ktk damu na ni Watanzania wenzetu. Asiwatumie vibaya, majuto ni mjukuu. Likitokea la kutokea hasara ya kwanza ni kwetu sisi kama nchi, aachane na mzaha huo. Ni kosa kutumia njia haramu kuutafuta mwisho halali, Ikulu mtu hawezi kwenda kwa kupita ktk mifereji ya damu za watu. Aache mara moja!!

#MitanoTenaKwaJPM.
MenukaJr.
 
Mungu anawaadhibu vizuri sana CCM mwaka huu. Yaaani anamnyanyua Lissu kwenye huo huo ufedhuli wenu mnaomfanyia.

Kama hujui kutafsiri sheria kaa tulia tu. Mlimzuia kufanya kampeni sio kwenda sokoni, sio kufanya vikao vya ndani vya organaizesheni kama kiongozi wa Chama.

Mwaka huu lazima hadi mtavua nguo kwa kuwehuka. Mlikuwa hamumjui vizuri huyo mpakwa mafuta wa Bwana. Huyo ndo mpaka mafuta wa Mungu Tundu Antiphas Lissu.

Vumilieni tu sindano zake😂😂
 
Unataka Lissu kwasababu kasimamishwa na Tume ndio asifanye shughuli zake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema?

Hizi akili zinapatikana Lumumba tu, nyie tutawaweka makumbusho vizazi vijavyo vije kuwashangaa tena kwa viingilio mliingizie hili taifa kipato.
 
Mbona Baba ako anendelea na Urais na juzi usiku mzito kamtumbua Mtu! Kama unataka Lissu asifanye chochote zaidi ya ugombea urais kwa kuwa haifai kutenganisha ugombea wake na umakamu mwenyekiti, basi mzee Baba naye aache kazi zozote za urais kwa sababu kama ulivyo sema, hatuwezi kutenganisha ugombea wake na urais wake! Hesabu rahisi tu, siyo kunya anye kuku, akinya bata, kaarisha!
 
Ni rahisi kama hivi...

Unaponitoa chumbani nisilale, haina maana kuwa sitapata usingizi popote nitakapo amua kulala...

Umenizuia kulala chumbani kwako lakini kamwe & naturally huwezi kufunga mlango wa usingizi wangu nikiamua kulala popote pale..!!

Sasa kama utakwenda kunishitaki mahakamani kwanini nilala usingizi pengine wakati ulinifukuza chumbani kwako, basi wewe utakuwa mjinga kwelikweli....!!

Sina hakika kama utakuwa umenielewa, maana nyie binadamu mnaoishi mtaa wa Lumumba - CCM akili na ufahamu wenu umefungiwa kwenye chupa iitwayo "CCM" na hazifurukuti mpaka aliyewafungia aruhusu kufunguka....!!
 
Popote alipo mgombea wa CCM, ndipo alipo Rais wa nchi. Ndiyo maana unamuona hadi yule mpambe(ADC) wa Rais na lile gari la mavyuma vyuma na walinzi wa Rais.


Sasa kwa Nini alipo mgombea wa CDM asiwepo na makamu wa mwenyekiti wa chama?
 
Lumumba, policcm, necccm, na wengineo wengi mngekua na IQ walau inayokaribia na ya Mh.Lissu, wala msingepata kabisa shida ya kumdhibiti au kuendana nae!!

Kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena!! Ngoja awanyooshe tu. Mlitusumbua sana nyinyi mchwa kwa miaka yote hii mitano.

Ni wakati wetu wa kupumua sasa na kutembea vifua mbele maana tumempata na sisi mkombozi wa Demokrasia ma mabadiliko nchini.
 
Kwa mtazamo wako huo mi naona njia nzuri ya kumfungia Lissu ili asiweze kufurukuta ilikuwa ni kumpeleka gerezani segerea, keko au ukonga ili aisiweze kutoka na kuonana na yeyote.

Vinginevyo haiwezekeni kabisa kumfanya Lissu akae tu ndani nyumbani kwake kisa kafungiwa kufanya kampeni.

Haiwezekani aache kufanya shughuli zake binafsi za kila siku zisizohusiana na kampeni eti kisa kafungiwa kufanya kampeni.
 
Unataka Lissu kwasababu kasimamishwa na Tume ndio asifanye shughuli zake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema?

Hizi akili zinapatikana lumumba tu, nyie tutawaweka makumbusho vizazi vijavyo vije kuwashangaa tena kwa viingilio mliingizie hili taifa kipato.
Hahahaa hii komenti nimeipenda zaidi ahhaaahaaa
 
Kwa iyo asiende hata sokoni kununua maitaji ya familia yake mkuu,alafu vyeo ni ofisi sio mtu, ila huwakilishwa na mtu katika nyakati tofauti , Wala sio tahaluma ya kusomea, kwa iyo cheo Cha kugombea nafasi ya urais alichopewa na nec kwa Sasa ofis ya cheo hicho ipo mapumziko, anaendelea na cheo chake katika ofis ya makam mwenyekiti wa chama chake,na ofis ya nyumbani kwake Kama baba,so lazima aende sokoni kuhemea kwa ajili ya familia yake,tatizo liko wapi
 
Back
Top Bottom