Pre GE2025 Lissu, kuna baadhi ya mambo busara inakutaka usiyazungumze in Camera mpaka inapokulazimu kufanya hivyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hilo sio tatizo la mkemeaji sasa, bali ni la taasisi inayapaswa kupambana na rushwa.
Ndio maana nimesema hiyo ni taasisi ya Wala Rushwa inayotaka kupambana na Rushwa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Kukemea hadharani,gizani unavuta Mlungula itakusaidia nini? πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ndio maana nimesema hiyo ni taasisi ya Wala Rushwa inayotaka kupambana na Rushwa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Kukemea hadharani,gizani unavuta Mlungula itakusaidia nini? πŸ˜‚πŸ˜‚
Narudia tena, huo ni wajibu wa Takukuru kupambana ni hiyo rushwa.
 
Siku zote sijawahi kuamini kama Lissu ana busara hiyo unayotaka awe nayo.
 
All in all you have my support until then! @Erythrocyte
"usiyazungumze hadharani...".... Huo ndio unafiki ulioifikisha CCM ilipo sasa hivi. Ni ajabu kwamba bado kuna watu wanataka hata CHADEMA ifuate njia hiyo hiyo!

COVID-19, wamefika hapo walipo fikia kwa "kufunika kombe".

Mambo ya "Maridhiano" ni sumu hiyo hiyo inayokitafuna chama; halafu watu wanataka yasizungumzwe?
 
Ninayo matumaini, kwamba huko huko ndani ya CHADEMA kuna kundi kubwa linalokubaliana na Lissu. Hawa itabidi wajizatiti kupambana na kundi lililo nunuliwa na CCM ndani ya chama hicho.

Kuondoka ndani ya CHADEMA wakati huu ambapo muda hautoshi, itakuwa ni kuwapa CCM ushindi wa chee moja kwa moja.

Wanao kubaliana na Tundu Lissu ndani ya CHADEMA sasa ni lazima wajizatiti kweli kweli kupambania wanacho kiamini badala ya kuogopa kupoteza maslahi yao binafsi ndani ya chama.
 
Wapi Huwa haikemewi hadharani? Watu waliacha kuchukua? 🀣🀣🀣🀣

Eti ishara
Kwani CCM hawakemei rushwa? Kama wanakemea basi kuna Wapokea rushwa. Hauwezi kuhubiri kwamba acheni uzinzi, ina maana unajua kuwa unaowahubiri wamo wazinzi. Unatakiwa kusema msifanye uzinzi ni dhambi. Siyo acheni
 
Na unadhani mambo haya mawili, ya Mwalimu Nyerere na Mwinyi, na haya aliyo yasemea Tundu Lissu kuhusu kuchunguza tuhuma ndani ya chama yanafanana; kwamba Tundu Lissu anakosa busara kwa kushauri uchunguzi kusafisha chama?
Ni kiongozi gani ndani ya chama hicho (CHADEMA) asiye taka chama kionekane kuwa safi, na kuona habari ya kufanyiwa uchunguzi ifanane na habari za kuangusha serikali iliyopo madarakani?
 
Kwa muda mrefu sana nimewaasa CDM kwamba ni wakati Mbowe aondoke.
Mbowe ameishiwa mbinu hana nguvu za uongozi wala maono mapya.

Mbowe anafahamu chaguzi huleta matatizo kwa vyama vyote, kwa uzoefu wa siku za nyuma na kwingine.

Uchaguzi wa kanda ya nyanda za juu ulikuwa na kila dalili ya kuanza matatizo, haukutakiwa kufanyiwa mzaha.
Ni ima Mbowe alitaka au alikaa kimya ili kutaka. M/Kiti Mbowe alivyosimamia suala hilo ni hovyo sana.

Baada ya Msigwa kuhama Mbowe akijitokeza kutoa kauli '' kuwa upinzani si kazi rahisi''
Ni moja ya kauli za kipuuzi kwasababu alitakiwa azuie madhara na si kuja kudanganya watu na vimameno

Ni maneno ya hovyo kama aliyosema '' Ukraine ipo vitani na Russia lakini wanaongea kuhusu suluhu' akishadidia maridhiano ya kipuuzi yaliyoishia na aibu kwake kwa kutapeliwa kitoto.

Tuhuma za TAL kuhusu rushwa ni kubwa na zinapaswa kuwa addressed. Mbowe kajificha mtifuano ukiendelea.

Alijificha katika chaguzi nyingine hadi akina Lema wakajitoa.
Kwa ufupi kuna kila dalili Mbowe ana '' orchestrate' haya mambo kwa faida anazozijua

Mbowe amekuwa Mwenyekiti kwa miaka 30 hana sababu za kuendelea.
Ikiwa katiba na anataka, Mbowe akubali ushindani na aache kutumiaVijana kuzua '' frustrations'

Mzee Mtei hakukaa miaka 30, Bob Makani hakukaa miaka 30, ' 'MBOWE MUST GO'

Mbowe akiwa Magereza CDM ili imarika kama taasisi tena TAL akiwa nje.
Harakati za katiba zilipamba moto. Mbowe alipotoka na kukimbilia Ikulu kila jambo limevia!
Mbowe ni polazrizing figure, he must go.

Habari za kurudi kwa COVID 19 '' behind the scenes'' Mbowe anaziingiza kiani! Huo ni ukweli
Mnakumbuka aliposema wiki chache zilizopita ''... ni wakati watu wasameheane katika chama..''

CDM kama mnataka chama imara, simameni katika ukweli.
Msitafute mchawi CCM au JF, mkabilini Mwenyekiti na kumwambia ukweli. Thank you for everything, it's time you pack an go.! Mbowe anapasua chama akitumia kikundi cha Vijana wake wasiotaka ukweli.

Pascal Mayalla JokaKuu
 
Binadamu tunatofautiana sana uoni, haya watu mnayasema leo, niangalieni mimi mwenzenu niliyasema lini CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! humo nilisema Ushauri huu ulitolewa 2010, ungefuatwa , 2015 ilikuwa Chadema inatinga ikulu!.
P
 
Binadamu tunatofautiana sana uoni, haya watu mnayasema leo, niangalieni mimi mwenzenu niliyasema lini CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! humo nilisema
Ushauri huu ulitolewa 2010, ungefuatwa , 2015 ilikuwa Chadema inatinga ikulu!.
P
Hapaana! Mimi nimesimama siku zote kueleza kwamba Mbowe ni tatizo. Rejea mabandiko yangu yote
Ninachowaambia sasa hivi ni ku prove kile nilichosema miaka mingi iliyopita

Ni hivi , Mbowe alipofanya vizuri nilimsema, alipokosea nilimsema. Nipo katika rekodi
Hivi karibuni nimeeleza jinsi alivyokuwa tatizo na anavyo handle mambo hovyo ikiwemo la 'maridhiano' na uchaguzi wa kanda. Sitetei mshindi au mshindwa yoyote, ninachosema ni poor handling kwasababu ya kukosa leadership ya Mbowe. Matatizo yote unayosikia sasa hivi ni Mbowe!

Tunasema sasa hivi ili waliochimbia vichwa mchangani, wasikie hata kama vwamegoma kufukua vichwa

Mbowe must go for CDM to survive and thrive

Tukianza kuorodhesha failure zake ! sijui itakuwaje. Ni hivi aondoke kwa hesima lakini aondoke
 
Hatima yake itakuwa poa tu maana ana ushawishi, cdm kama chama ndio itapoteza. Kwa taarifa yako Lisu akibaki cdm itaendelea kuwa na mvuto, kuliko Lisu akiondoka na Mbowe akabakia.
TAL asiende popote kwasababu anachosimamia ndio msimamo wa mtu mwenye akili.
Hapa ndipo ninatofautiana na Msigwa , kwamba, ameondoka halafu anasema ''mabaya' Nilidhani alipaswa kuyasema mabaya hata kama atafukuzwa ili aondoke akiwa ''clean''. Kwa anachokifanya ni tumbo tu!

Nilitofautiana na akina Kitila , Mgamba na Zitto kwa msimamo huo huo, kwamba, kama walijua kuna matatizo walipaswa kuyaweka wazi. Walichokifanya ilikuwa 'usaliti' . Laiti wangesema na kufukuzwa hiyo ni habari nyingine kabisa.

Ni hivi matatizo yote ni kwasababu ya Mbowe! amekosa leadership skill na nadhani hana jipya.
Mbowe anaogopwa na baadhi ya watu hivyo anajiona ni mfalme fulani na ka udikteta.

TAL yupo sahihi, huenda wameongea huko hakuna hatua kwasababu ''Mbowe' yupo nyuma ya matatizo.

Ukitaka kujua kwamba Mbowe anadhani yeye ni CDM, ni hatua yake ya kutoka Magereza kwenda kujadili mambo ya Chama Ikulu bila kuwaona wanachama wake waliompigania, viongozi wenzake n.k.

Mbowe ni 'polarising figure'' hawezi kuleta utangamano katika chama
Chama chake hakiwezi kuwa katika mtamziko halafu amejificha na kuzunguka na chopper, huyu ni tatizo

Mbowe must go!
 
Mshaanza kumtisha
 
Hizi Tabia za kupenda chama kuliko nchi ndo zimetufikisha hapa

Yaani mijitu ile rushwa, iogelee kwenye rushwa, ifanye mizengwe ya kuuza harakati kwa vipande 30 vya fedha halafu etu ilindwe kwa hoja ya kuyazungumzia ndani?

Hizi Tabia za kufugafuga madalali wa kisiasa ndo zimepelekea hadi CCM kuwa chama cha kulinda na kukingia kifua mafisadi.

Lissu yuko sahihi.
Rushwa ni adui wa haki, lazima ikemewe sirini na hadharani!

Mbowe amefikia ukomo, hana mpya, jipya wala upya. Amejitahidi kukifiksha chama hapa kilipofika, tunamshukuru, tunampenda, lakini sasa tuko tayari kunywa naye chai tu!. Lakini hana uwezo wa kukipeleka mbele chama kutoka hapa kilipofika. Ana uwezo wa kung'ang'ania kwa mujibu wa udikteta, lakini sanasana atabomoa kazi ya mikono yake mwenyewe tu na ya wengine walioijenga Chadema kwa miaka zaidi ya 30 kwa machozi, jasho na damu!.
 

Ukiona hivi kaguswa Nkulunziza.

Hapo wenye vibiongo lazima kukurupuka kutoka mashimoni macho pima, utafikiri ni mijusi iliyobanwa kwenye mlango.

Hasira za nini ndugu zangu? Au ni Yale maokoto ya kutetea watu hata kama hakuna hoja?

Kwamba ni dhidi ya Lissu?

Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Lissu hachafuliki kireja reja hivyo. Kwamba wako wapi waliosalia katika wasafi?

Hiiiiiiii ...iiii!

Alipo tupo!
 
Lissu anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ili akirudishe kwenye misisngi yake, sio huyo Mbowe vuguvugu. Na CHADEMA itadondoka kutokana na kiburi Cha Mbowe.

Unaukumbuka uzi wako huu?

Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Kulikoni kukubali kutishwa au kununuliwa kwa vipande vya fwedha?

You backtracked, but what did it serve?

Kwamba Lissu ni chaguo lililo bora zaidi kwani nani asiyejua?

Kwamba ni hawa chawa wa kulipwa au ma CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…