Lissu: Kuna Siri halali na Siri haramu ninazozitoa kwenye media ni Siri haramu ambazo zinakidhoofisha chama na Wanachama

Newforce

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2024
Posts
430
Reaction score
708
===
Lissu akijibu swali kuwa yeye hana "KABA" yaani hana siri,

Lissu amesema Kuna Siri aina mbili Kuna Siri kwa masilahi ya chama hizi zinaitwa Siri HALALI lakini Kuna zile ziri zinazokigharimu chama kama rushwa na uongo wa Mwenyekiti hizo ni Siri haramu na yeye hawezi acha kuzisema na kuzitafutia dawa ili kukiponya chama.

Soma Pia: Mdahalo wa Wagombea Uenyekiti CHADEMA Taifa
 
Lissu si wakumpa siri kabisa maana hana dhamana hata sekunde
 
Siri ni siri tu, kama hawezi kutunza siri hafai kuwa kiongozi.
 
Kwa sababu ya kuwa mkweli Lissu awe mbaya?Ikiwa Watanzania tumejengwa kwa nguzo hii ndiyo maana CCM wanatawala kwani kule uongo ni sera..Enzi za mwendazake uomgo ulifika mahali kusikiliza chombo cha habari cha serikali ni kinyaa.
 
Kwa sababu ya kuwa mkweli Lissu awe mbaya?Ikiwa Watanzania tumejengwa kwa nguzo hii ndiyo maana CCM wanatawala kwani kule uongo ni sera..Enzi za mwendazake uomgo ulifika mahali kusikiliza chombo cha habari cha serikali ni kinyaa.
Ukweli unalipa zaidi
 
Siri nyingine ni zile kesi zilizokua zinaiandama nchi kimataifa
 
Yupo sahihi.
Kwa mfano utaratibu wa hivyo kuwapata viti maalumu uliogubikwa rushwa zote ikiwemo ya ngono kwa mwenyekiti kwa nini zisisemwe ili zitafutiwe dawa na kukomeshwa?
Matumizi mabaya ya fedha za chama au ufisadi katika mchakato wa ukusanyaji pesa za JOIN THE CHAIN nao ufichwe kama siri za chama? Lazima wanachama waambiwe ukweli
 
Sawa Mungu amtangulie LISSU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…