Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mgombea uenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema baada ya 'mastori ya town' kusambaa anataka kugombea uenyekiti aliitwa kwenye kikao na watu watatu wanaoheshimika kwenye jamii, anasema kwenye kikao hicho Mbowe alisema hatagombea uenyekiti lakini pia alimkatalia Lissu asigombee nafasi hiyo kitu ambacho Lissu alikikataa.
Lissu anasema mpasuko wake na Mbowe ulianzia mbali kabla ya kutangaza nia, mpasuko wao ulianzia baada ya kuhoji maridhiano yaliyoingiwa na Mbowe. Lissu amesema chama cha CHADEMA kimepoteza watu wengi wa maana kwa sababu ya 'watu kuatamia madaraka'.
Lissu amesema yeye binafsi anajiona anatosha kwenye nafasi ya uenyekiti na anavyojiona kunaenda kuthibitishwa na wanachama wa Chadema wenye sifa za kupiga kura January 21.
Clouds TV