SI KWELI LISSU: Mbowe ametuharibia chama na uchaguzi wa ndani ya chama katika kupata wagombea kisa ahadi za Uwaziri Mkuu 2025

SI KWELI LISSU: Mbowe ametuharibia chama na uchaguzi wa ndani ya chama katika kupata wagombea kisa ahadi za Uwaziri Mkuu 2025

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
LISSU: Mbowe ametuharibia chama na uchaguzi wa ndani ya chama katika kupata wagombea kisa ahadi za Uwaziri Mkuu 2025

IMG_20241113_130102_465.jpg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni Makamu Mwenyekiti bara wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Pia Tundu Lissu amewahi kuwa mgombea wa Uraisi kupitia cha hicho mwaka 2022.

Novemba 12, 2024 Lissu aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa anazungumzia mambo kadhaa ikiwemo mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika 27, Novemba 2024.

Baada ya Mkutano huo kuliibuka grafiki inayodaiwa kuwa ya Jambo Tv ikiwa na ujumbe unaosema Lissu: Mbowe ametuharibia chama na uchaguzi wa ndani wa chama katika kupata wagombea kisa ahadi ya uwaziri Mkuu 2025 (Tazama hapa)

Je, uhalisia ni upi?

JamiiCheck imefatilia na kubaini kuwa taarifa na Grafiki inayoonekana kama ya Jambo Tv Si ya kweli, Aidha Lissu hakusema maneno hayo siku ya Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Singida mjini, Novemba 12, 2024.

Lissu alizungumzia kuwa CHADEMA walikubali kufanya Maridhiano na Samia ambayo Lissu anasema kuwa walidanganywa na kukubali kudanganyika kuwa wasiwe wakali watapewa Serikali ya umoja wa kitaifa na wakaacha hoja za msingi kama Katiba mpya na hakumtaja Mbowe kama ndiye aliyesababisha.

"Katikati hapa tumedanganywa tukadanganyika, tumeletewa lugha laini ya maridhiano lakini ni ya uongo.

Lugha laini lakini ni ya uongo, tukazungumzishwa kwa mwaka mzima tunapigwa maneno, tukapigwa maneno kwa mwaka mzima, tukazungumzishwa kwa mwaka mzima tunapigwa maneno.

Na tukakubali kupigwa maneno, tukaacha hoja za msingi, katiba mpya, mfumo mpya wa uchaguzi, tukaacha kuzungumza kwa nguvu habari ya katiba mpya, ya mfumo wa kidemokrasia ya nchi yetu ya mfumo huru wa uchaguzi.


Tukaingiziwa vijineno vinavyosema hivi, msiwe wakali sana, mtapewa Serikali ya nusu mkate, Serikali ya umoja wa kitaifa, baadhi yenu mtakuwa Mawaziri, wengine Mawaziri Wakuu labda, wengine Makamu wa Rais, wengine Wabunge, mtapewa viti vya ubunge na CCM vya bure msiwe wakali.

Tukaingia laini, tukaacha kuwa wakali, tukaacha kudai mabadiliko ya kidemokrasia ya nchi yetu, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mfumo huru wa uchaguzi, sasa Samia ametutangazia na ameitangazia Duania kama bado kuna mtu anafikiria habari ya nusu mkate, habari ya kupewa ubunge wa bure, ya kupewa uwaziri sijui kitu gani kama bado kuna mtu anafikiria"...
Alisema Lissu (Tazama)

Vile vile, JamiiCheck imepitia kurasa za Jambo Tv na kubaini kuwa hakuna taarifa kama hiyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Back
Top Bottom