Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
CHADEMA imeamsha matumaini ya Watanzania hasa baada ya Lissu kupiga krosi moja matata na kuwa Mwenyekiti Taifa. Watanzania walioonesha kuchoshwa na uchawa, ubadhilifu wa mali za umma na mazonge mengine yanayotokea nchini wameanza kupata matumaini huenda mambo yatabadilika for good.
Kuweka mambo sawa Lissu na CHADEMA ni muhimu kukata mzizi wa fitina kutoka kwenye katiba ili kutoka hapo msingi (uchaguzi) uwe imara kuweza kuhumili vishindo vya wanaokuja juu yake. Swali muhimu ni je, wananchi wapo tayari?
Ni jambo moja watu kushangilia na kuona wamepata mkombozi na ni jingine kubeba yale anayoyaamini na kuyafanyia kazi. Sio kumkatisha tamaa Lissu na CHADEMA lakini wanaona wanachofanya sasa inatosha kuwafanya watanzania wasimame kidete kuyataka mabadiliko hayo?
Mimi naona wengi hawapo tayari, siyo kwamba hawaelewi kile Lissu au CHADEMA wanahubiri, hapana, wanawaelewa vizuri lakini hawapo tayari kunyanyua mguu na kuanza kuchukua hatua. Na hili ni kwasababu bado wabongo hawajapigika vizuri, bado hawajaonja joto ya jiwe kufikia hatua ambayo hawana njia nyingine ya ku survive.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wakigeuka hivi serikali/CCM inatoa kitu kidogo wanatulia, kelele zikikolea sana unaona ajira za walimu zinashushwa kundi moja linapiga kimya, wanabaki wachache inakuwa haina maana tena, hata sauti zao hazina athari yoyote. Baadhi watapigia kelele huduma mbaya za afya mara utaona kuna misaada ya uongo na kweli inapelekwa sehemu yanageuka mapambio tena, yaani fulani ana huruma kweli, na harakati zinaishia hapo.
Tunaona wasanii wetu hapa kila kukicha kuwa chawa na kutetea matumbo yao, tunawalia kooni weee alkini atakuja mwenye team yake atakwambia mi huniambii kitu kwa fulani, kama hamumpendi ni nyie.... mwishowe tunaendelea vile vile kwenye mzunguko wa kutumiwa, wanalipwa milions kupumbumbaza watu wakati fedha hizo zingekuwa zinatumika kuboresha huduma zinazozorota na kuchechemea.
Tunatoleana mifano ya Wakenya kila mara na jinsi walivyo wamoja kupigania haki... tunachokikosa kwetu ni hiko, hatujapigika kisawasawa kuelewa thamani yetu, kuelewa thamani ya kile tunachostahili, nguvu yetu na nini tunatakiwa kufanya kuhakikisha kila anayepata nafasi anawajali wananchi na kuhakikisha kuna huduma bora.
Mna mpango mwingine ikiwa wananchi hawatanyanyua miguu na kuchukua hatua ya kwanza?