PreGE2025 Lissu na kauli mbiu ya “No Reforms, No Election” ni mipango ya Mungu au ya Shetani kutusambaratisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Mungu na Shetani
Hiii ni moja ya Mada zangu za holistic approach zinazotumia dhana dhanifu ya Mungu na shetani。

Hii ni mada fikirishi.
Outline.
  1. Utangulizi
  2. Declaration of Interest
  3. Holistic Approach
  4. Mungu na Shetani ni nani na wako wapi.
  5. Mpango wa Mungu na Mpango wa Shetani.
  6. No Reform No Election ni Mpango wa Mungu au Shetani?.
  7. Tundu Lissu ni Mpango wa Mungu au ni Ajent wa Shetani?
  8. Msingi Mkuu wa Nchi Yetu ni Katiba na Inapata Mamlaka kutoka kwa Wananchi
  9. Haki Mbili Kuu za Kikatiba,Kuchagua na Kuchaguliwa,zimeporwa Kishetani!Reforms Zitazirejesha!。
  10. Vyama vya Siasa Tanzania ni Public Parties Lazima Vitangulize Mbele Public Interests
  11. Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa Sio Tu ni Insane Bali Baadhi ni Ma Ajent wa shetani!
  12. Insanity Inawapataje Viongozi wa Siasa?..
  13. Mtu Kuwa Insane Sio Kosa, ni Hali Tuu, Lakini Kikundi cha Watu, Chama, Kikao au Wanachama Wote Kukubali Kufuata Ushauri wa Isane, Wote Mtaonekana Insane!.
  14. Je Kila Uamuzi wa Kugomea Jambo au Kususia Kitu ni Ujinga, Insane ?
  15. Hitimisho
1. Utangulizi
JF ni ukumbi huru wa kuhabarishana, kuelimishana, kuburudishana, na kitu kikubwa zaidi, kusaidiana. Kama kuna kitu unakijua, na unaona kinafanyika ndivyo sivyo, unajitolea kusaidia kuwaelimisha wengine kuhusu kitu hicho, na hiki ndicho mimi ninachofanya humu JF, kuwaelimisha wengine kile nilichobahatika kukifahamu, na elimu hii naitoa humu jf, kupitia makala zangu za kwa Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo pia zinachapishwa kwenye magazeti ya Mwananchi na Nipashe, kila Jumatano na Jumapili na pia zinakwenda sambamba na kipindi cha TV cha jina hilo hilo la KMT, kinachoruka kila Jumapili saa 3:00 usiku na Jumatano saa 9:30 alasiri on Channel Ten

Declaration of Interest
Mimi ni kada wa chama cha siasa, ila ninapoandika hapa, siandiki kama kada, bali naandika kama Mtanzania Mzalendo, ambaye ni mwandishi wa habari aliyehudumu newsroom kwa zaidi ya miaka 30, na pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, hivyo ukinisoma with preconceived opinions kuwa huyu ni kada wa chama fulani, hutaweza kuiona the rationale behind bandiko hili, na elimu ninayoitoa, hivyo nakushauri bora uishie hapa.

3. Holistic Approach
Mada ya leo, japo ni mada ya kisiasa,lakini naijadili kwa mtindo wa holistic approach kwa kutumia dhana dhanifu ya Mungu na Shetani。Kila kinachotokea duniani, jambo lolote, ni ama ni mpango wa Mungu ama ni mpango wa Shetani.

4. Mungu na Shetani ni nani na wako wapi.
5, Mpango wa Mungu na Mpango wa Shetani.
6. No Reform No Election ni Mpango wa Mungu au Shetani.
7. Je Tundu Lissu ni Mpango wa Mungu au ni Ajent wa Shetani?
8. Msingi Mkuu wa Nchi Yetu ni Katiba na Inapata Mamlaka kutoka kwa Wananchi。
9. Haki hizi mbili za kuchagua na kuchaguliwa ndio haki kuu mbili za msingi sana za kisiasa ndani ya katiba yetu.
10. Vyama vya Siasa Tanzania ni Public Parties Lazima Vitangulize Mbele Public Interests
11. Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa Sio Tu ni Insane Bali Baadhi ni Ma Ajent wa shetani!.
12. Insanity Inawapataje Viongozi wa Siasa?.Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?
13。Mtu Kuwa Insane Sio Kosa, ni Hali Tuu, Lakini Kikundi cha Watu, Chama, Kikao au Wanachama Wote Kukubali Kufuata Ushauri wa Isane, Wote Mtaonekana Insane!. Wale Wasio Insane, Wasikubali Maamuzi ya Kijinga!.
14. Je Kila Uamuzi wa Kugomea Jambo au Kususia Kitu ni Ujinga, Insane ?
Hitimisho.
Kwa vile vyama vya siasa ni public parties, viongozi wa vyama, mna wajibu wa kuviendesha vyama vyenu kwa kutanguliza mbele maslahi ya umma na sio maslahi binafsi ya viongozi wenu, msiruhusu ignorance, insanity, selfishness na utumishi wa shetani kwa baadhi ya viongozi wenu wabinafsi, kuviangamiza vyama vyenu kwa ignorance, insanity, selfishness yao, na mpango wa shetani wakati miongoni mwenu sio wote mko insane.

ila inawezekana hii no reforms no election ni mpango wa Mungu kwa Tanzania anao letwa kwa mtindo wa blessing in disguise,ili hizo reforms ziondoe ule ushetani uliofanywa kwenye katiba yetu,hivyo Chadema ni mpango wa Mungu na Tundu Lissu ni mpango wa Mungu kuwakomboa Watanzania kurejeshewa haki zao。

Kipimo cha mwisho NRNE na Tundu Lissu kama ni mpango wa Mungu au wa shetani,tutakipima kwa performance and the end justifies the means,kama NRNE ni mpango wa Mungu,then Mungu atatenda,reforms zitafanyika kabla ya uchaguzi na tutafanya uchaguzi huru kweli na wa haki kweli na kama kusipofanyika reforms,uchaguzi haitafanyika, sio Tundu Lissu, Chadema na wafuasi wao kukinukisha,bali kwa Mungu Baba muweza wa yote kufanya kitu kitakachofanya uchaguzi usifanuike!。

Kama NRNE,ni mpango wa shetani,hakutafanyika reforms zozote,na uchaguzi utafanyika kama kawaida,huo mpango haramu wa kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike,utashindwa!, mipango ovu ya maajenti wa shetani,washindwe na walegee!

Mungu Ibariki Tanzania!

Nawatakia Jumatatu Njema na mapumziko mema ya Karume Day。

Paskali
 
Ukila Hela za watu unaweza kurupushwa hata saa Tisa usiku ukiwa uchi WA mnyama ukaacha unyumba na KUSHIKA keyboard 🎹 Yako kuanza kuandika Kile mlambisha asali anataka.... LISSU amewashika pabaya sana HII NO REFORMS NO ELECTION imewashika pabaya sana... In loving memory of president John magufuli " Mayala kwetu kule wasukuma maana yake ni Njaa" wakuu tutafte pesa aisee
 
No Reforms No Election ni mpango wa CHADEMA wala si wa hata Papa wala nani. Mungu si mtanzania wala hana muda na siasa za majitaka. Jitahidi mwanangu kumuondoa Mungu kwenye mambo yenu. Mungu alikaa wapi na nani kuamua na kutangaza huu mpango wako? Kwanini usiseme wewe ni CHADEMA na unatafuta kujustify mambo yenu? Nakataa kata kata. Ukiamini usanii huu, kesho machawa watakuja kama wewe na kusema mfuga chawa ni chaguo au mpango wa Mungu wakati ni mpango wa machawa. Kumuingiza Mungu kwenye usanii wa kusiasa kunaweza kutafsirika kama kuishiwa kimawazo. Ni ushauri tu
 
Kuna namna hii No Reform No Election inakunyima kabisa usingizi mleta mada ambaye ni kada rasmi wa CCM. Hii sijui ni mada yako ya ngapi ndani ya masaa 24.
Kuna kitu kizito nimenusa.
Muda utajibu.

..yaani Tundu Lissu anagombaniwa utadhani mpira wa kona. Sijui amewakosea nini baadhi ya ndugu zetu?🤣
 
Haya mambo ya kuamka usiku wa manane na kutetea uhuni wa watawala, ni suala la muda tutakuwa na vikundi vya waasi watakaopigania kuporwa rasilimali na haki zao na watawala dhalimu.. Juzi tu nilikuwa Kalemie DRC..Wakongomani wanasema mlipoteza kiongozi muhimu (Magufuli) katika kulinda rasilimali za nchi.. namuona Tundu Lisu km Mkombozi mpya ajaye..
 
Lissu hataki amani wala maendeleo ya taifa lake..

Hata bwawa la umeme rufiji amelipinga hadharani na anaendelea kuliponda mpaka leo hii

Lissu makinikia alikuwa anawatetea acacia na barrick kama na yeye ni m canada vile
 


Sijawahi kuona agent wa shetani kwa nchi ambayo ina rushwa kama yetu halafu yeye ni msafi. Lissu hana kashfa ya rushwa. No reform ni manadiliko siyo ya kujinufaisha Lissu binafsi bali ni usawa kwa wote. Kwa yaliyotokea 2019, 2020 na 2024 Agent wa sherani ni wote walio iba chaguzi na haki za watanzania. Agent wa sherani ni wote wanaounga mkono kwenda kwenye chaguzi wakijua kabisa usalama na Polisi wanaiba kura. Machawa ni ma Agent wengine wa mashetani
 
P nimpango wa Mungu ,hata ukimuuliza shetani atakuambia kwenye mpango huo hama mimi sisogezi kanyagio zangu.
 
Na wewe umetoa wapi hiyo authority ya kujua Mungu kapanga nini (kama yupo) unaongea kama unaishi naye chumba cha pili mnapiga naye stori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…