PreGE2025 Lissu na kauli mbiu ya “No Reforms, No Election” ni mipango ya Mungu au ya Shetani kutusambaratisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Illusions za kujustify fweza za abdul, uzuri tulishaambiwa mapema sana mafungu yanatoka sana ni kujichotea tu!
 
Huo ni usemi tu, Hii nchi hatuwezi kuwaachia vijana. Bado sana. Lissu ni sawa tu na viongozi wengine wa upinzani he has nothing special.
 
Du! Hujui!
Yani we una mamlaka gani hadi umchagulie huyo mungu vya kumuhusisha navyo? Unajuaje kama hayupo kwenye tv anamtazama simba anavyoitesa sisiemu? Mambo ya kufikirika yabaki kufikirika na ya mayala kujustify fungu lake nayo ibaki hivyohivyo tusubiri outcome
 
Mayala kwa Kisukuma ni NJAA - John Pombe Magufuli, Ikulu ya Magogoni, November 7 mwaka 2016.
 
Kama wewe umemhusisha kwani ni wako peke yako nami nisimhusishe? Nimemjibu Paskal kuwa huo si mpango wa Mungu kama alivyotaka tuamini. Kwanini humuulizi yeye juu ya hayo mamlaka unayoniuliza mie?
 
JF ni ukumbi huru wa kuhabarishana, kuelimishana, kuburudishana, na kitu kikubwa zaidi, kusaidiana. Kama kuna kitu unakijua, na unaona kinafanyika ndivyo sivyo, unajitolea kusaidia kuwaelimisha wengine kuhusu kitu hicho
 
Sio vitu vyote ambavyo sio mapenzi wa Mungu ni Mapenzi wa shetani, ndo maana kuna:

1. Mapenzi ya Mungu.
2. Mapenzi ya Mungu makamilifu
3. Makamilifu yanayompendeza.

Mamfano:

1. Sio mapenzi ya Mungu uwe Chawa.
2. Sio mapenzi ya shetani uwe Chawa, ni njaa zako!

Kindly change the tittle, fool!
 
Mimi sikujua kwamba kuna haki ya kuchaguliwa. Hii inapatikana wapi, Bro. Mayalla? Nijuavyo mimi, kuna haki ya kuomba kuchaguliwa!
 
Paskal mimi nafikiri katika haki ya kuchagua na kuchaguliwa umeonyesha uchawa wako kwa kueleza tu vyama vinaweza kumnyima mtu kugombea,hakuna kitu kama hicho!Kura ya mwananchi hivi sasa haiheshimiwi.Pili,uchaguzi unaingiliwa na dola na tume iko kwenye kuisaidia dola iliyopo iweze kushinda!Kwa madhila waliyopitia watz ni bora kutokufanyika uchafuz kuliko kuendelea na mambo ya kijinga mpaka marekebisho!Rejea uchaguz wa serikali za mitaa 2024 kile kilikuwa kitu gani?
 
PASKALI Mayala wa cc👇👇
Uchaguzi wa kidemokrasia una misingi yake ili kukidhi vigezo vya uwazi, uhuru na haki!
Tanzania hiyo misingi haipo. Bali iliyopo inaamuliwa na mfumo wa upendeleo kwa mgombea wa ccm! Wananchi kwa sasa wanaelewa ubovu wa hiyo mifumo!
Na huo ndo msingi wa wananchi kususia chaguzi! Fuatilia data utaona trends za mdororo wa wananchi kushiriki chaguzi!
Ni kweli, Wananchi wanaamini ili kupata viongozi Bora maamuzi yao ni sehemu ya mchakato. Lakini ccm imechomekea mifumo inayowapora wananchi hiyo haki ya msingi! Yaani chaguzi zimekuwa kama vile mazingaombwe au comedy shows!

Ujio wa Lissu unaanza kutuonesha wapinzani ni kina nani, wazalendo ni kina nani, wajasiria-siasa na wasakatonge ni kina nani!!
Kumbe siku zote wengine wakipigania reforms wengine wapo busy kusaka vyeo na umalaya wa kisiasa! No wonders matamko yalikuwa mengi vitendo zero!

CHADEMA wazalendo kama wapo serious wakomae na hiyo No Reforms No Elections! Na ikibidi waungane na vyama vingine wasusie uchaguzi 2025.
Hakuna haja ya kulinda status quo!
Kwanini washiriki kuonja sumu ya uchaguzi wanayofahamu madhara yake?

Vyama vya siasa vinatakiwa kusoma alama za nyakati na kwenda na mitazamo ya wananchi!
Kimsingi wananchi wengi hawajitokezi tena kwenye michakato ya uchaguzi hasa kujiandikisha, kuhakiki majina na kupiga kura!
Hii ni kwa sababu wengi wao wanaamini NO REFORMS NO ELECTIONS! Kifupi idadi ya wanaosusia chaguzi nchini Tanzania inazidi kuongezeka!

Kwa muda mrefu sasa wananchi wanataka REFORMS! Upinzani usiendelee kuwasaliti wananchi!
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu.
 
Shina la mabaya yote ni kupenda sana fedha .

Ukiona viongozi au wanasiasa wanapenda sana fedha basi ujue hao ndio mawakala wa shetani.

Tundu Antipas Lisu ni mpango wa Mungu kwa Watanzania na tishio kubwa sana kwa wapenda sana fedha bila kujali haki na utu wa wengine
 
Similarly to: expecting results from what you know

Kutegemea matokeo toka kitu ama jambo unalo lijua yaani kutegemea matokeo chanya kwenye "uchafuzi"

Vie vile unamtuma mtu 'x' akachukue pesa kwa mtu 'y' kumbe hakika unajua kwamba hawezi kupewa pesa na mtu'y'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…