PreGE2025 Lissu na kauli mbiu ya “No Reforms, No Election” ni mipango ya Mungu au ya Shetani kutusambaratisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Haya maandiko yako yamenikumbusha Operation mockingbird, namna kitengo cha Marekani kilivyolipa hela waandishi wa habari ili kuandika uongo mzuri (propaganda) kuhusu Marekani dhidi ya Soviet.
Mimi naandika just for the love of it,situmwi na yeyote,silipwi na yeyote,I speak my mind freely, ninachoandika sio propaganda ni ukweli mtupu,tena ukweli mwingine ni ukweli mchungu!。
P
 
Nimepitia kwa umakini mkubwa andiko hili. Nilichogundua ni Kwamba "Tutafute hela" ndugu zangu ili tusinunuliwe. Njaa ni Mbaya
kama unaamini naandika kwasababu ya njaa,endelea kuamini,mimi naendelea kuandika kusaidia kuelimisha jamii。
P
 
Ukila Hela za watu unaweza kurupushwa hata saa Tisa usiku ukiwa uchi WA mnyama ukaacha unyumba na KUSHIKA keyboard 🎹 Yako kuanza kuandika Kile mlambisha asali anataka....
Sijala pesa ya mtu
LISSU amewashika pabaya sana HII NO REFORMS NO ELECTION imewashika pabaya sana...
its true,haswa hili la kukinukisha uchaguzi usifanyike!,Mimi naamini Lissu ni mpango wa Mungu,kupona kwake ile assassination atempt ni muujiza wa Mwenyezi ili Lissu aendelee kuwepo kwa kusudi fulani la Mungu!。 Moyo wangu unaniambia kusudi hilo ni Lissu kugombea na kuingia ikulu,hivyo Lissu ni mpango wa Mungu kugombea,hii ya no election na kukinukisha ni mpango wa mwovu shetani,amekuwa possessed na evil spirit,na kugeuka agent wa shetani bila yeye kujijua!,uchaguzi utafanyika kama kawaida,Lissu Chadema hawawezi kuzuia kitu!,watatoka empty,bila ruzuku,Chadema ni majalala!。
In loving memory of president John magufuli " Mayala kwetu kule wasukuma maana yake ni Njaa" wakuu tutafte pesa aisee
RIP JPM!
P
 
Mkuu huyo agent wa Shetani anatokea wapi kama kazi za Shetani zinafanyika anavyotaka? Anatokeaje kama kuna Rushwa,Ufisadi,Dhuruma,Matumizi mabaya ya fedha za umma,wizi wa kura,uvurugaji wa Uchaguzi,mauaji ya wananchi wakati wa uchaguzi,uporaji wa haki na ukandamizaji wa haki za wananchi,nk?
Anayehubiri Tanzania ni Nchi ya Amani wakati hayo yapo ni Shetani.
Shetani anatokea wapi kama kungekuwa na Tume Huru,Shetani anatokea wapi kama Katiba ingekuwa ya Kweli?
Ukiona hayo yote yapo Na watu wamekata tamaa! Mungu anamtuma Nabii wake kuja kuwawaokoa watu wake!
Lakini ukisoma Biblia ni Nabii gani ambaye hakupitia mateso,kupigwa mawe na Kuawa?
Akina Daniel walitupwa katika tundu la sindano,wengine walitupwa kwenye matanuri ya moto,wengine walitupwa kwenye mashimo marefu,wengine walikatwa misumeno,nk
Sasa Mkuu unamwonaje Lissu ni agent wa Shetani au ni Nabii wa Mungu?
 

Shetani ni ccm na agents wake ni wale wote wasiotaka mabadiliko.
Tukumbuke kuwa wananchi wanataka mabadiliko na kwa kuwa hawayaoni wengi hawajihusishi na mifumo ya kitapeli ya ccm!
Yaani kifupi wananchi walishasusa kitambo! Nchi ya watu zaidi ya 65+ Rais anachaguliwq kwa kura zisizozidi 10M
 
Mkuu ninakufahamu physically. Una heshima kubwa sana katika tasnia ya habari. Ila nasikitika huwa sisomi takataka zako. Huna utu, huna huruma, kwa, madhila ya binadamu waliyopitia/wanayopitia. Tumia muda kuandika mambo ya maana, badala ya kujipendekeza.
 
Asiyekua na ignorance, insanity, selfishness asiyeweza kukiangamiza chama chake kwa ignorance, insanity, selfishness na sio insane huyu hapa anatoa maelezo kamili.

Your browser is not able to display this video.
 
Msamehe bure tu huyu Mzee Mayalla
 
Huo mpango ni wa Watanzania. Ulianza tangu Madam akiwa makamu mwenyekiti wa katiba MPYA. Reform ya katiba MPYA ilianza tangu enzi ya JMK akiwa Rais. Sasa wewe unayesema ni wa Chadema umezaliwa lini.?Siyo kwamba hujui ila unajitoa ufahamu.
 
Kuna namna hii No Reform No Election inakunyima kabisa usingizi mleta mada ambaye ni kada rasmi wa CCM. Hii sijui ni mada yako ya ngapi ndani ya masaa 24.
Kuna kitu kizito nimenusa.
Muda utajibu.
Posho si walimualika katibu mkuu wao kuwa mgeni rasmi jukwaa la wahariri.. hapo akaunti zimetapika noti balaaa kila baada ya nusu saa anaanzisha uzi.
 
Na bado.. endeleeni kudemka
 
Huo mpango ni wa Watanzania. Ulianza tangu Madam akiwa makamu mwenyekiti wa katiba MPYA. Reform ya katiba MPYA ilianza tangu enzi ya JMK akiwa Rais. Sasa wewe unayesema ni wa Chadema umezaliwa lini.?Siyo kwamba hujui ila unajitoa ufahamu.
Si kwamba sijui. Najua. Nilichokataa na kuendelea kukataa ni kudai ni mpango wa Mungu. Hayo mengine hayakuibuliwa kwenye madai niliyojaribu kukanusha
 
Kipindi cha chaguzi ndio mwaka wa KUVUNA kwa makanjanja wengi. Huyu bwana anapigania tumbo lake tu, basi.
 
When you write too much, think too much.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…