Abuka
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 248
- 242
2. Je, CHADEMA wanaweza kuzuia Uchaguzi? HAPANA hiyo sio kazi yao, mwenye mamlaka ya kutangaza na kuhairisha uchaguzi ni Tume huru ya Uchaguzi pekee.
3. Je, Uchaguzi usipokuwepo, nini kitatokea? Rais aliyepo Madarakani na Makamu wake wa Rais wataendelea kuongoza hadi pale uchaguzi utakapofanyika na viongozi wateule wakaapishwa. Hiyo bado ni hasara kubwa kwa CHADEMA
4. Je CHADEMA wanamaanisha nini kusema hakuna uchaguzi?, wamesema watatangaza Dunia nzima lakini pia watatumia nguvu zao zote kuzuia uchaguzi, maneno ambayo yana viashiria vya fujo, maandamano n.k
5. Je wakitangazia Dunia itafanya nini? Kwa sasa nchi kubwa kama Marekani na Umoja wa Ulaya wametangaza kupitia upya sera zao za mambo ya nje ili pesa ielekee tu kule inapoona kuna tija, hiyo uchaguzi huu tofauti na miaka mingine unaweza usiwe na macho mengi hasa kwa mataifa ambayo hayanufaiki na Tanzania.