lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Movie ilanza steringi alitoka kazini na dereva wake, alipofika maeneo ya nyumbai akashambuliwa na maadui kwa kila Aina ya silaha.
Maadui wakakimbia wakajua wamemuua, wamemaliza.
Wakaenda kwenye kambi Yao wakasherehekea, huku wakimpa taarifa kubwa la maadui kuwa wmemaliza kazi. Kitongoji chote na miji ya jirani kukawa na simani,hofu na kukata tamaa,wakazi was kitongoji wakawa wakilia kimyakimya,kwani Genge la maadui lilikua na Tabia ya kutesa watu kwenye kitongoji na vijijini.
Steringi ndio alikua akiwapa moyo na akiweza kuwakemea maadui, alikwamisha dili za maadui.
Kubwa la maadui likaendelea kutamba kila Aina ya Tambo na kuendelea kukosesha raha Wana kitongoji na wanavijiji.
Habari za steingi ndio zikawa zimefika mwisho.
Siku zikawa zinapita na taarifa tofautitofauti zikawa zinaibuka kidogokidogo kuwa steringi hajafa ,kubwa la maadui likawa na mashaka, lakini lilipofatilia taarifa likaambiwa hajiwezi kwa lolote,Ni kwamba hawezi hata kusimama,hivyo hawezi hata kurusha ngumu,kwisha habari yake.
Wanakijiji na wanakitongoji wakata tamaa. Majambazi yakaendelea kutamba kitongoji na vijiji vya jirani, kila yalichotaka yalichukua kibabe,Tena yalichukua hadharani bila kuogopa mtu Wala kitu.
Kila majambazi yakionekana kwa mbali yanakuja na magari Yao, wanakitongoji walikimbilia ndani, majumbani mwao, walifunga milango na kuzuia na vitu vizito milangoni na kwenda madirishani kuchungulia majambazi watafanya Nini.
Wakazi walikata tamaa kabisa,hofu,mashaka na uoga vilitamalaki.
Baada ya miaka takriban mitatu hivi,wakazi wa kitongoji na vijiji wakiwa kwenye shughulizao mbalimbali za kujitafutia maisha,wengine wakiwa mashambani,wengine masokoni na wengine kwenye shughuli nyingine wakamuona mtu mmoja kwa mbaaaaaaali,akija kwa kutembea huku akichechemea,alikua akija kutokea njia itelemshayo ikishuka toka kilimani.
Alikua akitembea kwa kujikongoja na kibegi chake mgongoni. Watu waliokua huko atokeako wakawa wakimfananisha,wakaanza kuoneshana,wengine wakamsogelea kila na yeye alipokua akisoge.
Waliendela kumsogelea naye akija taratibu kwa upole zaidi.
Wakazi wakaanza kupiga makelele ya kumtambua,watu wengine wakamzunguka kuhakikisha kama ndiye yeye.
Baada ya kugundua Kuna wengine walifurahi na wengine waliogopa,walijua majambazi wakijua karudi wakuja kuamsha timbwili la kufa mtu ili kummaliza hivyo kupelekea kitongoji kuteketea.wengi walirudi majumbani,na wengine walitoroka kwenda Miki ya mbali ili kuepuka maangamizi.
Ikumbukwe kwamba kuna Marafiki wa steringi walisalimu amri na kujiunga na maadui,hivyo kupelekea maadui kuwa na Siri nyinginza steringi na za kitongoji,na ukizingatia kuwa steringi anachechemea amevunjwa vunjwa viingo, wakazi wakawa hawana matumaini tena ya hata kujaribu kukabiliana na Genge la maadui.
Wengi walinywea,wengine walijificha na Kama nilivyosema hapo juu wengi walisepa.
Steringi akaanza kuwaelimisha wakazi wachache Sana waliokua na ujasiri kidogo wa kubaki na na kumsikiliza ,aliwaambia kuwa,yeye amekuja kuwakomboa kutoka mikono ya majambazi,katika hao wachache waliobaki kumsikiliza na wengine kumshangaa kwa kuokoka kwakwe,wachache wao Tena wakaona huyu kachanganyikiwa huyu,pengine like Shambulio limempa uchizi,baadhi Yao wakondoka,likabaki kundi dogo sana likimsikiliza na kumuunga mkono.
Kaa kutumia haohao wachache waliobaki akaanza kuwapa mikakati ya kulifutilia mbali Genge la majambazi,
Aliwapa mbinu,mipango na njia atakazo zitumia kuliangamiza Genge Hilo.
Alianzisha mafunzo yanukakamavu na mbinu za kukabiliana Ana kwa Ana,uso kwa uso,mkono kwa mkono kwa uchache wao,na udhaifu wao dhidi ya maadui wenye kila Aina ya zana ,fedha na hila.
Steringi akapanga watu wake vizuri kila Kona kukusanya taarifa na na kutoa ishala pale adui anapokuja ili kuanza kuangamiza adui mmoja baada ya mwingine.
Kweli bana.adui aktuma ujumbe wa vitisho,maadui wakaja wakapata kipigo kimoja matata Sana,wakarudi mbio kutoa taarifa kwa kubwa lao na kuongeza idadi ya wapiganaji wake.
Wakaja Mara ya pili wakiwa wengi zaidi,wakapata pigo Kali kuliko la kwanza ,maadui wakachanganyikiwa,baada ya kuona vipigo wanavyopewa maadui,wakazi wa kitongoji na vijiji wakanza kufungua milango,na kujitokeza,wale waliokimbia wakaanza kurudi na hatimae Steringi akapata uungwaji mkono na wanakijiji na wanakitongoji wengi.
Ndipo mashambulizi yakabadilika na kuelekea kwa adui kwa nguvu.Hivi Sasa Stringing na watu wake wanakomboa Kijiji kimoja kila baada ya kingine, na sasa hivi Steringi Yuko kwenye eneo la maadui anapiga vibaya Sana.
Watu imani imerudi wengi wamesema watajitokeza kwa wingi kwenda kuteketeza makazi ya Kubwa la maadui.
Siku iliyopangwa kuvamia ngome ya Kubwa la maadui Ni tarehe 28-10-2020.