Uchaguzi 2020 Lissu pumzika, katika kipindi hiki cha week moja, nchi na Dunia itakusemea kuliko ambavyo ungesema wewe

Uchaguzi 2020 Lissu pumzika, katika kipindi hiki cha week moja, nchi na Dunia itakusemea kuliko ambavyo ungesema wewe

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,494
Reaction score
2,540
Husika na kichwa hapo juu.

Uwezi jua Mungu anakuhepusha na Nini kingekupata kwenye harakati zako ndani ya week ijayo.

Uliona jinsi katazo la kutumia helicopter lilivyokuwezesha kuwafikia wengi na kukupa mguso wa uhalisia wa maisha halisi ya Watanzania kuliko ungekua unaruka angani.

Amini pia mahamuzi haya yatakupa fursa ya kuzungumziwa kuliko mtia nia yoyote.

By the way, umefanya kazi kubwa sana katika round ya pili. Nature imekupa fursa ya kupumzisha mwili na akili . Jipe muda wa kupanga hoja za round ya mwisho. Jipe muda wa kuandaa timu yenu ya ushindi hasa katika masuala ya mawakala wenu watakavyo ruka viunzi na sayansi ya bao la mkono.

Relax! Enjoy your history.

Everything happens for a reason.
 
Msaidieni ndugu yenu asije sema anaonewa badae kwa vitu vidogo sana.

Mtu anaweza kukudhulumu 10,000 wewe kwa hasira ukamkata shingo akafa, utakua umetenda kosa la mauaji,10,000 ilikua n haki yako kabisa ila ungeweza tumia busara kudai hela yako uliyodhulumiwa kuliko hasira ambazo zinaenda ku cost maisha yako yote yaliyo salia duniani. Lissu anaweza kuwa na haki lakini msipo msaidia njia sahihi ya kudai haki mnaenda kumsababishia matatizo yatayomcost maisha yake yote.
 
Sure, adhabu hii ni promotion kwake. So anahitaji kutulia na ku-enjoy.
 
CCM wamezidiwa sana akili na CDM naona kuna watu wanahaha kutoka mtandao mmoja hadi mwingine wanakimbizwa huku wanakimbilia huko, halafu wanarudi hali ni mbaya sana. Nawapongeza wana CDM na wapenda mabadiliko wote kwa jinsi mnavyowadhibiti wanasiasa matumbo. Heko!
 
Kweli kabisa. Lissu 'chill'. Umefanya kampeni ya nguvu huku ukiwa na furaha tele. Haya yanafanyika kukuondoa kwenye reli ili wewe pamoja na Chadema muanze kampeni za fujo kupambana na polisi. Kusimamishwa kampeni ni kampeni tosha kwako.

Wewe ni tishio! Hiyo ratiba ya hizo siku saba za kuwanadi wagombea wa ubunge na udiwani anaweza kuendelea Mbowe na Mnyika bila wasi kwani wana uzoefu wa kutosha kwenye ulingo wa siasa. Tunza nguvu za kurudi kutoka kifungoni kwa kishindo.

Issue nzito za kuleteleza uitwe na ufungiwe tena ziongee siku tatu za mwisho wa kampeni ukijua hakuna muda wa kutosha kukuandia barua, kujibu malalamiko saa 24 na kwenda kwenye hiyo kamati. Yaani ikiwezekana kesho ibukia kijiweni au sokoni na kadhalika. Ongea na wananchi. Picha za matukio yako na wananchi ni kampeni tosha.
 
Historia ni mwl mzuri. Meli ya MV Bukoba ilizama ikiwa inakaribia bandari ya Mwanza. Pale bandari ya Bukoba iliwaacha abiria kadhaa.

Wakaifuata bandari ya kemondo jirani na bandari ya Bukoba kama km 20 kwa barabara. Wakapanda. Kuna waliokufa .meli imekuacha. Achana nayo
 
Wacha Vimsemeeeee ila Ikulu haendi kwa kusemewa anaenda kwa kupigiwa kura na wapiga kura hanaaaa hahahahaha patamu hapi.
 
Kazi muhimu na pengine ngumu kuliko zote iliyobaki kwa watanzania wakisaidiwa na dunia ni kupata tume ambayo itamtangaza mshindi aliyeshinda kihalali. Kama kuna taasisi au taifa ambalo linaitakia mema Tanzania basi lisaidie hapo
 
Mtu anaweza kukudhulumu 10,000 wewe kwa hasira ukamkata shingo akafa, utakua umetenda kosa la mauaji,10,000 ilikua n haki yako kabisa ila ungeweza tumia busara kudai hela yako uliyodhulumiwa kuliko hasira ambazo zinaenda ku cost maisha yako yote yaliyo salia duniani. Lissu anaweza kuwa na haki lakini msipo msaidia njia sahihi ya kudai haki mnaenda kumsababishia matatizo yatayomcost maisha yake yote.
Upande wa siasa za kiafrika haipo hivyo ndg mtanzania, kutokana na mifuno mibovu na kikandamizi huwezi ruhusu mtu akudhulumu pesa yako then unamuangalia anavyoondoka kisa uoga, hii dhana ni sawa na imani ya dini, imesababisha watu wengi kuishi kwa hofu sana, matokeo unayafahamu.
 
Bwana yule yupo garage. Ni Lori la mkaa. Trip moja porini, trip ya pili garage.
 
Back
Top Bottom