Tatizo la watanzania kubwa ni kujenga matumaini makubwa kwa viongozi wanasiasa ambao hata kumbukumbu ziko wazi kwamba ni watu wabaya. Huyu Rais alishakuwa waziri, alikuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba, akawa makamu wa Rais na akatoka waziwazi na kutamba jinsi watakavyoharibu uchaguzi.
Leo hii eti wanaharakati na wapinzani wanamsifia weee, utasikia mama anaupiga mwingi! Uko wapi? Fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hajagusa, paye kapunguza asilimia moja tu na hakuna nyongeza ya mshahara, ajira zimejaa madudu Kama siku za Mwendazake. Wasaidizi wake karibia wote ni wale wale. Sioni jipya la kusifia. Wakosoaji endeleeni na kazi yenu, acheni kujipendekeza. Yule ni CCM na haitabadilika.