Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema yeye binafsi hajutii kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji uliofanyika jana Novemba 27 2024.
Lissu ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na jambo TV akisisitiza "sijutii nimejifunza angalau mimi nimejifunza kwamba tumepotea na nimejifunza kwamba inabidi turudi kwenye hoja za msingi tupambanie mambo ya msingi, katiba mpya, mfumo huru wa uchaguzi sheria mpya taasisi mpya za uchaguzi"
Alipoulizwa juu ya vyama vya upinzani kupoteza imani kwa wananchi na kushuka kwa ushawishi wa vyama hivyo kama itakuwa na madhara kuelekea uchaguzi mkuu mwakani Lissu alijibu kuwa "kama tutaendelea kufikiria kwamba tutashinda tu bila kujali katiba inasemaje juu ya uchaguzi, taasisi za uchaguzi zimeundwa namna gani, zinafanyaje kazi bila kuangalia sheria za uchaguzi zikoje, bila kuangalia haya mambo ya msingi kuamini tu kwamba kushiriki kutatusaidia hatutafika popote"
Lissu ameogeza kuwa "kuna vyama ambavyo vimekuwa vinashiriki uchaguzi huu tangu, angalau sisi tulikuwa tunabishana lakini waangalie wale wote waliokuwa wanashiriki bila kinyongo wako wapi tusipoangalia na sisi tutaenda njia hiyo hiyo tutasinyaa kama walivyosinyaa wengine
PIA SOMA
- LGE2024 - Tundu Lissu: Uchaguzi huu umeisha na sasa tujipange upya na turudi kwenye hoja za msingi ikiwemo Katiba Mpya na Mfumo huru wa uchaguzi
Chanzo: Jambo TV