View attachment 3647625
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amefikishwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam leo, Agosti 10, 2026, kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili.
Kesi hiyo imeanza tena baada ya kusimama kwa takribani miezi mitano tangu Februari 24, 2026.
Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalohusishwa na kauli alizotoa kuhusu kusudio la kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kesi hiyo inasikilizwa kwa mfululizo kuanzia Agosti 10 hadi Septemba 7, 2026, chini ya Jopo la Majaji watatu, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Vikao vya maandalizi ya uendeshaji wa kesi hiyo vilifanyika kuanzia Agosti 5, 2026, vikihusisha Mahakama, upande wa Jamhuri, mshitakiwa Tundu Lissu pamoja na mawakili wake.
Kwa sasa, kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi.
Baadhi ya mashahidi, wakiwemo askari polisi na mashahidi wasiokuwa askari ambao ni mashahidi wanaolindwa, tayari wametoa ushahidi wao.
Lissu amekuwa akishikiliwa gerezani tangu alipokamatwa Aprili 9, 2025, na kushtakiwa siku iliyofuata kwa makosa ya uhaini na uchochezi.
View attachment 3647626
Kesi inaanza…
Baada ya kuanza kwa kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Lissu aliomba kuzungumza, ambapo amesema kumekuwa na ucheleweshwaji wa kesi yake wa makusudi.
“Serikali kukimbilia Mahakama ya Rufani ilikuwa ni kunipotezea muda wangu tu. Nilisema hili wakati ule, leo narudia tena. Leo ni siku 166 tangu 24 February 2024 tulivyoondoka hapa. “Tumerudi hapa baada ya kupotezewa siku 166. Nasema hii kwa kuwa nilisema hapo awali, itakapofika siku itabidi tuzungumze kuhusu hii kesi ya bure tu inayofanywa na hawa mawakili wa Serikali na huyo anayewatuma. Someone will have to pay for this,” amesema Lissu.
Kwa upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga amejibu maelezo ya Lissu akisema kuwa sio sahihi na Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya kuchelewesha kesi bali kilichotokea ni upande huo ulikuwa unatekeleza haki yake ya kisheria ya kuomba marejeo ya shauri Mahakama ya Rufani baada ya kuhisi kuna sehemu Majaji hawakuamua kwa usahihi.
“Haikuwa nia ya upande wa Jamhuri kuchelewesha kesi.Kuhusu kushinda na kushindwa, kushindwa kwa Wakili mwenye weledi ni jambo la kawaida” amesema Katuga
Baada ya hayo Jaji Dunstan Ndunguru alitaka kesi iendelee na sasa shahidi ambaye ni ACP Amini Mahamba anaendelea kutoa ushahidi wake.
Shahidi anaanza kutoa ushahidi
Shahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Amini Mahamba Kamishna Msaidizi wa Polisi anatoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa Serikali.
Shahidi: Nilipokea taarifa na nikaanza safari kuelekea ofisi za mkuu wa upelelezi kanda maalumu ya DSM ZCO baada ya kufika nilikutana na maofisa wengine kisha nikakaribishwa ofisini na kupewa mrejesho juu ya walipofikia yeye na timu yake ya upelelezi.
Kwenye jalada niliona jina la mshitakiwa ambayae yuko mbele yetu ambaye ni Tundu Antipas Lissu. Baada ya hatua hizo niliwapangia majukumu, kupeleleza, kukusanya taarifa kuhoji.
Wakili wa Serikali: Wewe unasema ndio ulisimamia upelelezi kwenye hizo timu kama unakumbuka kulikuwa na nani na nani.
Shahidi Mahamba: Timu ya ukamataji, Mkaguzi wa polisi msaidizi Michael ndio alikuwa kiongozi wao ……. Inspekta Nunu na wengine. Shahidi anaendelea kuwataja kwa majina
Baada ya kupanga majukumu mimi na ile timu tulitazama ile video picha mjongeo toka akaunti ya youtube ya Jambo TV.
Wakili: Waambie majaji ni video gani hiyo.
Shahidi: Ilikua ni video ya Tundu Lissu akihutubia.
Wakili: Mliweza vipi kuiangalia?
Shahidi: Tukiwa pale ofisini kuna kompyuta maalumu ambayo anaitumia inspekta Michael ndio tuliitumia kuangalizia hiyo video"
Wakali: Mahakama inataka kujua mliitazama kwa kiwango gani?
Shahidi: Tuliitazama kuanzia mwanzo mpaka mwisho, hiyo video ilikua ndefu na tulitazama kwa masaa mawili na Zaidi.
Wakili: Katika hiyo video ulimwona nani?
Shahidi: Nilimuona Tundu Lissu na alikua amevaa vazi rasmi la chama la rangi ya kaki akiwa amesimama kwemye mimbari akitoa hotuba na kulikuwa na bendera ya chama na nyuma bendera kama ya taifa.
Wakili: Iambie Mahakama rangi za bendera ya taifa ni zipi.
Shahidi: Rangi za bendera ya taifa ni bluu, njano kijani na nyeusi.
Wakili: Haya rangi za bendera ya Chadema ni zipi?
Shahidi: Kuna nyeupe, buluu bahari nyekundu na nyeusi.
Wakili: Tuambie kipi kingine uliona?
Shahidi: Pia alikuwa amevaa miwani na alikua akihutubia umma.
Wakili: Unaweza ukaimbia Mahakama lugha aliyokua akitumia mshitakiwa.
Shahidi: Lugha iliyokua ikitumika ni lugha yetu ya taifa Kiswahili.
Wakili: Wewe ulikua ukiratibu zoezi zima la upeleleze ulipata nini kwemye hiyo video kilichoonesha hapa kinafungamana na jalada lilokuwa mbele yenu.
Shahidi: Baada ya kutazama ile video tulibaini kulikuwa na kulikuwa na kosa kutokana na maneno mengi aliyotamka ila kwa kesi hii naomba nirejee machache.
Ananukuu, “Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi… akaendelea kusema ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko kwa sababu tunaenda kukinukisha sana huu uchaguzi tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana,” mwisho wa kunukuu.
Wakili: Sasa shahidi hebu iambie Mahakama haya maneno baada ya kuyasikia ilipata tafsiri gani?
Shahidi: Kwa mujibu wa yale maneno aliyoyasema mimi pamoja na timu yangu ndipo tuliona mshitakiwa Tundu Antipass Lissu alikuwa na nia ya kuitisha serikali ili ifanye anayotaka, kitendo cha kuitisha serikali kwa kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uasi ndio uhaini wenyewe huo.
Wakili: Unasema uhaini kwa mujibu wa kifungu gani Shahidi Hilo kosa lipo kwa mujibu wa kifungu ….. Kwa mujibu wa uchunguzi wetu tuliofanya tulibaini Tundu Lissu alikuwa akihutubia raia na kwa kuwa ni Raia wa Tanzania anawajibu wa utii kwa Jamhuri ya Muungano, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakili: Hayo maneno yalikuaje ya kitisho kwa serikali hebu waambie majaji
Shahidi: Mshitakiwa alipotamka yale maneno yanaviashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani na kutamka yale maneno ni kuitishia serikali kwa uwazi.
Wakali: Halafu?
Shahidi: Aliidhirishia serikali nia yake kwa kuchapisha maneno hayo kwemye mtandao wa youtube wa Jambo TV.
Wakili: Kingine mlichokiona cha kuigusa serikali ambayo ni wajibu wake kulinda amani'
Shahidi: Uchaguzi ulizungumziwa ni uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais na uchaguzi upo kwa mujibu wa katiba.
Wakili: Waambie majaji ni nani mwenye jukumu la kulinda nchi.
Shahidi: Ni wajibu wa serikali.
Wakili: Ni nani ambaye anachukua hatua sheria pale inapokuwa imevunjwa?
Shahidi: Ni serikali.
Wakili: Unapotishia kuvunja amani nani anaathirika?
Shahidi: Anayeathirika unapotishia kuvuruga uchaguzi ni ule muhimili mmoja wa serikali ambao ndio unajukumu la kusimamia na kutekeleza sheria ndani ya nchi.
Wakili: Tuambia kama uliwahi kufanya uchunguzi juu ya haya maneno ulifahamu uchaguzi ungevurugwa vipi?
Shahidi: Katika upelelezi wetu tulioufanya hayo maneno ya kukinukisha yalilenga kufanyika kwa matendo ambayo yangezuia uchaguzi usifanyike.
View attachment 3647627
Lissu: Msiruhusu upande wa mashitaka kuleta vitu ambavyo hawajanituhumu navyo
Wakati shahidi akiendelea kutoa ushahidi wake, Lissu aliomna kuongea, ambapo alipinga upande wa mashitaka kuleta vitu ambavyo hajatuhumiwa hivyo.
“Waheshimwa majaji, siyo kila shahidi anaruhusiwa kutoa ushahidi wa kila kitu. Mkiruhusu upande wa mashtaka waingize ushahidi wa shahidi huyu utakuwa ni ushahidi wa ziada, ni kwamba tutahama kutoka katika kesi ya uhaini iliyopo mbele yetu, na tuanze kujadili kesi ya kujadili kuchana karatasi za kura.
“Walete ushahidi wa mambo ambayo wananituhumu nayo katika hati ya mashtaka. Walete ushahidi wa mashtaka ya uhaini. Mahakama ikiruhusu kuleta mambo yasiyokuwepo, inaruhusu kufungua sanduku la pandora.
“Humo ndani ya sanduku kumejaa uchafu na madudu ya kila aina. Mahakama isiruhusu jambo hilo,” amesema Lissu.
Hata hivyo, wakili wa Serikali alijibu hoja hiyo akisema:
“Waheshimiwa majaji ushahidi unapimwa na mahakama, na hazuiwi kusema huyu ni mpelelezi sasa anazuiwa vipi asiseme walichokibaini na huu sio ushahidi mpya. Mashahdi wengine walisema pia uchaguzi ungezuia vipi kumzuia kusema sio sawa na mahakama hii nina amini inatenda haki.”
Baada ya majadiliano kidogo, Jaji alimruhusu wakili wa serikali kuendelea na akaanza kumuelezea Jaji msingi wa swali alilomuuza shahidi hasa kwenye kipengele cha kukinukisha.
Lissu akaongea tena, “Waheshimiwa majaji, shahidi hana haki ya kutoa ushahidi anaoufikiria. Anatoa ushahidi unaendena na shauri husika kitu anachosema kiwe inaendana na kesi, kuna maneno mengi sana kwenye kesi hii tutakinukisha, na mengine yako kwenye hati ya mashitaka lakini hakuna maneno ya kuchana karatasi za kura, tutapiga watu. Mkiruhusu haya meneno, mtafungua sanduku la wadudu wabaya kuingia na mtashindwa kuendesha kesi hii vyema.
Ni rai yangu masiruhusu upande wa mashitaka kuleta vitu ambavyo hawajanituhumu navyo, hatari ni kwamba mkiruhusu ukaingia kwenye rekodi mtalazimika kuutolea uamuzi na wanafahamu hivyo mkiruhusu tutahama kwenye kesi ya uhaini na kwenda kwenye kuchoma karatasi za kura sisi waaadawa wanahaki ya kupinga ushahidi unapokuwa sio sahihi na msiruhusu mambo ambayo hayapo naomba msiruhusu.”
Baada ya hapo, majaji waliongea tena kidogo, kisha Jaji Ndunguru akatoa maelekezo:
“Tukitazama hapa notisi tuliyotoa awali naona ndio huko tunataka kuelekea wakili mwongoze shahidi vizuri hataki kwenda kwenye mambo ya Oktoba 29, ambayo tulishakataa tangu awali.”
Wakili: Serikali inaomba mahakama iwaruhusu kuendelea maana hata mashahidi waliopita walisema mambo yaliyofungamana na mambo kama kuzia kura na mengine hii haitakuwa sawa.
Baada ya hapo, Jaji Nduguru akamwambia asuburi kwanza.
Wakili: Walikua wamewakamata watu kwa sababu gani?
Shahidi: Ilikuwa ni kwa kuchochea na kushawishi watu kufanya maandamano na wakaniambia tayari walikuwa wameshafungua majalada kwa baadhi ya maeneo.
Shahidi aliomba ruhusa atoke akajisitiri na majaji wakamruhusu
Kesi hii itaendelea kusikilizwa mwendo wa saa nane.