Lissu: Tuliomba uchaguzi uhairishwe kwa mwaka Mmoja ili tuweke mambo vizuri, CCM (Wassira) wakakataa

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,522
Reaction score
40,795
Akitoa utetezi wake Leo, Lissu amedai katika Mkutano wake na watia Nia wa CHADEMA alipendekeza uchaguzi wa mwaka 2025 usogezwe mbele kwa mwaka Mmoja ili serikali pamoja na upinzani wakae na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi.

Ila pendekezo lake likakataliwa na CCM kupitia Makamu Mwenyekiti wa CCM Steven Wassira.

Lissu amesisitiza ya kwamba kama pendekezo lake lingekubaliwa na CCM yale mauaji na ghasia za Octoba 29 yangezuilika..
 
Utetezi wa kukataa kuongeza muda kutoka kwa mdau mmoja ulikuwa:

Katiba haimtambui raisi nje ya kipindi cha kikatiba yaani miaka mi5. So kuongeza muda kwenye kiti cha uraisi ni mtego ili nchi ibaki haina raisi na chain of command kuvurugika kisha yaibuke makundi ambayo tusingejua yametokea wapi maana nchi haina mwenyewe kikatiba.
 
Leo nimefuatilia kesi ya LISSU kuanzia alifu mbaya wasalamu, na nimepata picha kwamba taifa letu linapaswa kupata katiba mpya yenye mamlaka ya usimamizi wa misingi yake, maana kitu kikubwa kabisa hapa ni kwamba misingi ya haki, demokrasia za kisiasa, utawala bora na utawala wa sheria vimeifadhiwa kwenye mamlaka ya mwenye maslahi ya kisiasa, kiukweli mayai haya hayapaswi kuwekwa kapu moja kamwe, Yaani mwenye maslahi ya kisisasa hawezi kamwe kuwa msimamizi wa misingi ya demokrasia ya kisiasa, Baada ya kusema haya naomba nipendekeze kwenu "Rasimu ya katiba yenye muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa", Yaani.

1. Baraza la usimamizi wa taifa;
Baraza hili ni muhimili wa usimamizi wa misingi yote ya kitaifa, mamlaka ya kimuungano, tathmini za kitaifa na muungozo kwa hali ya taifa pale Kanuni za ulinganigu wa nguvu za kikatiba zinapoingia.

2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania; serikali ni muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za serikali na taifa, ulinzi wa taifa na mengineyo kama rasimu hiyo itamkavyo.

3. Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania; bunge ni muhimili wa uwakilishi wa wananchi wenye jukumu la kutunga sheria, kupitisha bajeti za taifa, majadiriano ya muelwkwo wa taifa na mengineyo kama rasimu yenyewe itamkavyo.

4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa Tanzania; Mahakama ni muhimili wa utoaji haki, mfasiri wa katiba na sheria za nchi, mtoa huku wa makosa ya jinai na madai na mengineyo kama rasimu yenyewe itamkavyo. Jambo la kipekee ni kwamba ndani ya muhimili huu kuna mahakama ya katiba yenye mamlaka ya juu na ya mwisho kabisa ya mashauri ya kikatiba nchini.

Muundo huu unahakikisha uwajibikaji, uwazi, uadilifu na kuondoa kabisa ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na mwisho kuibua usawa na mshikamano wa kitaifa.

katika rasimu hiyo inayopatikana katika tovuti ya www.katibampya.com Mihimili hii yote minne imetamkwa kwenye SURA YA NNE ya katiba hiyo kwa kuanza na Baraza ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 kisha kuendelea mihimili mingineyo kwa mpangilio wa nambafi kama ulivyoweka hapo juu.

Aidha pia Sehemu kubwa ya historia ya LISSU imezungumzia Uchaguzi, na niendelee kusema kwamba Rasimu ya katiba kwenye tovuti tajwa haijaishia pekee kwenye Kuanzisha Tume huru ya uchaguzi, katika ibara ya 212, rasimu hiyo emeenda mbali mbaka kuanzisha, "Mchakato wa uthibitisho wa uhalali wa madaraka na kupingwa kwake" katika ibara ya 176.

Embu fikiria Kabra ya kuapishwa kwa Rais, mbunge na Diwani Kuna mchakato Maalumu wa kikatiba wa kuthibitisha Kura, ushindi na hapo ndipo Mahakama ya katiba inaitisha Uhapisho rasmi, Zoezi hilo limewekwa kwa muda wa siku 30 mbaka 73 pekee.

Haya yote ninayoyasema hapa si maneno ya jumla hivyo ni wajibu wako kufika kwenye tovuti hiyo na kusoma rasimu hiyo hasa kuanzia kwenye ibara nilizozitaja hapo juu au kuanza mwanzo hadi mwisho.

Angalizo; Rasimu hiyo ya katiba haiondoa mchakato rasmi wa katiba, Hivyo basi Rasimu hiyo ni maoni ya kisomi, kitaaluma yanayoitaji jicho la kisomi, kitaaluma na raia wote kwa ujumla na kwa maoni haya nina imani pale mchakato rasmi utakapoanza basi Wananchi wote tutakuwa na taswira nzuri ya nini kilicho bora.

chanzo: www.katibampya.com
 
Walipendekeza bunge limuongezee muda kisheria.
 
Kweli kabisa
 
Mama ataongezewa muda ili aweke mambo vizuri (Katiba mpya), hivyo hoja ya Lissu bado inatekelezeka.
 

Ktk vyama 18 kimoja tu kije na takwa la kukiuka Katiba lengo lake Lissu na Genge lake lilijulikana

Akili ndogo kamwe haiwezi kushinda Akili kubwaa✍️
 
Kama mh Lissu yeye ni mwenye Akili kiasi kutaka kusitisha Uchaguzi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Basi kwanini anayakana maneno yake mwenyewe mbele ya Majaji tena mbele ya Viapo

Yani aibu utaona wewe 😂

ndio Lissu maneno yake leo anayakataa mchana kweupe ¿¿¿

Vip Jamhuri ingemsikiliza takwa lake pekeyako kusitisha Uchaguzi ‼️

uyu hasingekuja kubadilisha maneno mbele ya Safari ‼️

Mwisho Serikali ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan kujikuta njia panda baada kuwa
kinyume na Katiba👈

Lissu ni msaniii halikosa Rasta tu
Kwasasa kashaanza kuzifuga✍️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…