Pre GE2025 Lissu tupe ahadi ya kuanzisha CHADEMA TV na Redio endapo utashinda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tundu Lissu tupe ahadi ukishinda Utaanzisha Chadema TV & Radio, Mbowe japo alikuwa na Disco kama Kusaga lakini ameshindwa kwa miaka 20

Sifurahishwi na utaratibu wa Mbowe na Tundu Lissu kila siku kupishana kwenye Vituo vya Tv vinavyomilikiwa na Wanaccm kufanya Kampeni za kunadi Sera zao

Labda Mh Tundu Antipasi Lissu utujulishe una mpango wowote wa kuanzisha Channel ten ya CHADEMA?

Nimekaa pale ๐Ÿผ
 
labda auze Mikocheni na yule mzungu wa ulaya
 
Chama tawala hakiwezi kukubali!
Kupata licence tu itakuwa ni shida na hata ikipatikana masharti sasa!
Mwisho wake ni kufungwa na kupigwa marufuku!
 
Hivi vyama vya siasa vya Marekani na Ulaya vina vituo vyao vya TV?

Amandla...
 
Alitakiwa kuchangisha mil 30 hakupata hata jero seuze za kuanzisha tv na redio
 
Umekaa paleee na lita ya ulanzi plus bagia za Kalenga.Hongo mwagito!
 
Lisu anataka ruzuku ishuke mpk jimboni mambo ya kujitolea hayapo sehemu yoyote duniani
 
Itapata usajili toka Marekani au hapa hapa Tanzania ? Ngoja tuone kama hata barua yenyewe itapokelewa na TCRA. Na je sheria zinaruhusu vyama kuwa na TV/redio ?
 
Hoja KUNTU..wapenda mageuzi wengi wanataka Radio na Runinga ya Chama..INAWEZEKANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ