Uchaguzi 2020 Lissu umati usikudanganye, wengi hawajajiandikisha

Wanaomshabikia lissu hawajajiandikisha, wanaomshabikia magufuli wamejiandikisha.

Mnawajua vipi?

ukiwa ccm unakuwa mjinga fulani
 
Wafuasi wa CHADEMA na Lissu wamekuwa wakipagawa na kuota kwamba, uchaguzi wa October utawapatia ushindi na kwa mara ya kwanza toka tujipatie Uhuru nchi itaongozwa na upinzani.

Hii ni kutokana na Umati ambao umekuwa ukijitokeza kwenye kampeni za ugombea urais kwa mheshimiwa Tundu Lissu. Niwaambie wafuasi wa CHADEMA endeleeni kufurahia ngojera za mgombea wenu ila Urais mtaendelea kuusikia hadi 2925.

Sababu ya kwanza ni kwamba, watanzania wengi mnaowaona kwenye mikutano, hawajajiandikisha na hata hao waliojiandikisha, kwenye uchaguzi wa mwaka huu hawataamka kwenda kupiga hiyo kura kwa vile inajulikana wazi Mjomba Magu anarudi pale Chamwino na Magogoni.

Pili, vyama vya upinzani vyote vimeshapoteza mvuto kwa wananchi na kuikubali CCM na mgombea wake, kwa yale Serikali ya CCM iliyoyafanya na yanaonekana kwa macho na hata kuyagusa kwa mkono.

Tatu, Viongozi wa vyama vya upinzani wameshapoteza imani kwa wananchi na hasa Wasomi na waelewa wa mambo,ambao miaka michache iliyopita ndiyo tulikuwa tukiunga mkono mageuzi, kwa kuona CCM ni ya watu wasiojielewa. Kupotea kwa imani hii kumetokana na viongozi wenyewe wa vyama vya upinzani kufanya kama taasisi zao, na si za wananchi. Tazama Mbowe na Chadema, Zitto na ACT, hawana tofauti na Mzee Mrema wa TLP, au NCCR ya Mbatia.Ndiyo maana Dr Slaa aliyaona haya mapema akaamua kukaa pembeni.Chadema na wafuasi wenu msijidanganye.
Swali langu tu kwa mwenye uzi. Unajuaje kuwa hawajajiandikisha? Je wale wanaokusanyika kwa wagombea wengine wamejiandikisha? Au its only apply to lissu?
Based on what research umeona hawajajiandikisha?
 
Upuuzi mtupu umati wa lissu hawajajiandikisha ila kwa jiwe wamejiandikisha au sio.
Hujasikia huko kanda ya ziwa shule zilifungwa ili watu wajaze viwanja kama kirumba. Wengi walienda kumuona MONDI baada ya show wanataka kutoka bila kumsikiliza jiwe milango ikafungwa
 
Wafuasi wa CHADEMA na Lissu wamekuwa wakipagawa na kuota kwamba, uchaguzi wa October utawapatia ushindi na kwa mara ya kwanza toka tujipatie Uhuru nchi itaongozwa na upinzani.

Hii ni kutokana na Umati ambao umekuwa ukijitokeza kwenye kampeni za ugombea urais kwa mheshimiwa Tundu Lissu. Niwaambie wafuasi wa CHADEMA endeleeni kufurahia ngojera za mgombea wenu ila Urais mtaendelea kuusikia hadi 2925.

Sababu ya kwanza ni kwamba, watanzania wengi mnaowaona kwenye mikutano, hawajajiandikisha na hata hao waliojiandikisha, kwenye uchaguzi wa mwaka huu hawataamka kwenda kupiga hiyo kura kwa vile inajulikana wazi Mjomba Magu anarudi pale Chamwino na Magogoni.

Pili, vyama vya upinzani vyote vimeshapoteza mvuto kwa wananchi na kuikubali CCM na mgombea wake, kwa yale Serikali ya CCM iliyoyafanya na yanaonekana kwa macho na hata kuyagusa kwa mkono.

Tatu, Viongozi wa vyama vya upinzani wameshapoteza imani kwa wananchi na hasa Wasomi na waelewa wa mambo,ambao miaka michache iliyopita ndiyo tulikuwa tukiunga mkono mageuzi, kwa kuona CCM ni ya watu wasiojielewa. Kupotea kwa imani hii kumetokana na viongozi wenyewe wa vyama vya upinzani kufanya kama taasisi zao, na si za wananchi. Tazama Mbowe na Chadema, Zitto na ACT, hawana tofauti na Mzee Mrema wa TLP, au NCCR ya Mbatia.Ndiyo maana Dr Slaa aliyaona haya mapema akaamua kukaa pembeni.Chadema na wafuasi wenu msijidanganye.
Ujinga, kwani we ndo ulikuwa ukiandikisha wapiga kura, chuja unachotaka kuleta mbele ya watu wenye akili.
 
Lowassa alipigiwa mpaka deki katika barabara aliyokatiza kule Mwanza ulipo fikra siku ya uchaguzi akabaki akishangaa.

Watanzania ni sawa sawa na “wajumbe”, wanaweza kukukarimu mpaka ukajiona unaishi mawinguni.
Usi ishi kwa kukariri.
 
Back
Top Bottom