- Source #1
- View Source #1
Lissu: Viongozi wa dini hasa mapadri na Maaskofu ni Wapuuzi wanapokea rushwa kila kukicha
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tangu mwaka 2019 alipochaguliwa kutumikia nafasi hiyo, pia alikuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka 2020 ambapo wagombea wengi wa upinzani hawakufanikiwa kushinda nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi huo.
Lissu ni mwanasiasa anayesifika kwa kuwa muwazi na msema kweli kutokana na haiba yake ya kukosoa na kutokufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na masuala mbalimbali yenye maslahi kwa umma.
Mnamo tarehe 12 Novemba 2024 Lissu alizungumza na waandishi wa habari akiwa mkoani Singida, pamoja na mambo mengine alikosoa ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia katika michakato mbalimbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo pia alitumia nafasi hiyo kukemea rushwa ndani na nje ya chama chake. Unaweza kurejea mikutano hiyo ya Lissu na waandishi wa habari hapa na hapa.
Kumeibuka posta inayoonekana kama ya Jambo Tv ambayo imeambatanishwa na ujumbe unaosemeka kuwa Lissu: Viongozi wa dini hasa Mapadre na Maaskofu ni wapuuzi wanapokea rushwa kila kukicha. Tusiwategemee, waache kuongea sana watuache tufanye siasa.
Je, Uhalisia ni upi kuhusu posta na ujumbe huo?
JamiiCheck imefuatilia na kuaibini kuwa Posta hiyo haikuwahi kuchapishwa kwenye kurasa zozote Rasmi za Jambo Tv na wala hakuwahi kuandika ujumbe kama unavyosomeka kwenye posta hiyo japo Lissu aligusia rushwa kwenye mkutano aliofanya na Waandishi wa habari akiwa Singida Novemba 12, 2024 ambapo maneno ya kwenye posta hiyo yamepotoshwa kutoka kwenye maneno aliyosema siku hiyo.
Aidha, Lissu aligusia kuwa Samia amekuwa akitoa pesa kwa Makanisa, Mapari na Maaskofu ambayo yeye aliita pesa hiyo kuwa ni Rushwa huku akihoji hela ya kufanya vitu vya msingi hamna ila ya kugawa kwenye makanisa ipo
Tukabilianne na Samia kama tulivyokabiliana na Magufuli, njia itakuwa ngumu sana, njia mbeleni itakuwa ngumu sana lakini ndio njia pekee, haya longolongo hii haitupeleki popote.
Kwa hiyo kitu cha msing ni kujipanga upya, tufanye mabadiliko ya msingi kwenye nchi yetu, ndiyo tuzungumze chaguzi, vinginevyo itakuwa siyo mambo yaleyale kwa sababu ukisema mambo yaleyale maana hakutakuwa na mabadiliko, mabadiliko yatakuwepo na yatakuwa mabaya sana kwa nchi yetu na kwa Wananchi wetu.
Hivi mnafikiri kama bandari zimekwenda, viwanja vya ndege vimekwenda, hifadhi za wanyama pori, misitu vinakwenda, madini yalishakwenda zamani tutabaki na nini? Nyie mtabaki na nini na watoto wenu na wajukuu zenu?
Hela za kufanya mambo ya msingi hamna hela ya kuhonga makanisa na viongozi wa kidini iko kwa mabilioni, mmefanya hesabu ya pesa ambazo Samia amezitoa kanisani kati ya mwaka jana na mwaka huu, zinapita zaidi ya shilingi bilioni 1, jiulize Samia anazipata wapi?
Anazipata wapi? Mmewahi kuona Nyerere akihonga Makanisani, Au mwinyi, Au Mkapa Au hata Kikwete, Magufuli sijui, nilikuwa mgonjwa mimi nilikuwa napigania uhai, naambiwa Magufuli alikuwa anachangisha sadaka kanisani.
Huyu Mama Askofu akinyenyuka hivi anapigwa rungu la milioni 150, padri akitoka huko anapigwa na milioni 50, akitoka huko anapigwa na milioni 100, mnafikiri hizo hela ni za nani?
Na kwa nini zinatapanywa hivyo, hiyo siyo Rushwa ni nini Waheshimiwa, Rais anazitoa wapi? Au mnafikiri kama alivyokuwa anafikiri Magufuli kwamba hela yote ya Nchi hii ni ya kwake, ndivyo anavyofikiria:-Tundu Lissu akiwa Singida Novemba 12, 2024