Hahahaaa...... Kabisa mkuuItabidi aombe radhi kwa kweli, hata mimi nadhani level za lisu hapa bongo ni akina mtemi chenge na mkono maana hao nasikia hawajambo sana kwenye hii fani
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kwani NEC wenyewe wanasemaje?Wengi wa wasiofikiri wanadhani kumkata TL asigombee urais ni kumuondolea umaarufu. This action will make the nation vulnerable to mass unrest. Heri wamuruhusu agombee na tume imtendee haki.
Ninachojua, Watanzania watamchagua tena Ndugu John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020-2025!Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.
Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.
Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa Tundu Lissu, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.
Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. Tundu Lissu ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.
Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.
Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
Huu ni mziki mwingine mkuu,sio ule uliouzoea.Alikatwa Lowassa na maisha yakaendelea, akafanya Jecha yake na Maisha yakaendelea, Who is Lissu Buda?. Kitu pekee ambacho wakataji wanapaswa kuwa na uhakika ni Kama Membe, Zitto, Maalim, Lipumba, Sipunda na Mbatia wataendelea kushiriki uchaguzi baada ya jamaa kukwanguliwa, watakuwa wamemaliza kazi. Watanzania sisi tunajijua, kwetu sisi Mchuma Janga hula na wakwao!
TAL in 2020....tume ya NEC wasituzingue this 2020. Nitapiga kura kwa TAL kwa hasira sana.....nimemaliza chuo since 2015 hadi sasa future haileweki....wallah wallah sawa acha tuoneHakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.