Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wanatumia makamasi badala ya akili.Hivi Katuga na wenzie wanatumia akili hizi hizi zetu?
Na anaiiingiza kwa kutokujua maana ana uwezo mdogo wa sheria. Katuga anapewa maagizo toka juu anayabeba kwa kuhofia kuwaambia ukweli wa ugumu wa kisheria kwani watamuona ana uwezo mdogo, hivyo anabeba hivyo hivyo akitegemea jaji ataamua kwa utashi wa serekali. Kwa bahat mbaya hata Jaji anakosa mpenyo wa kisheria wa kuibeba serekali kwani mshitakiwa yuko vizuri kisheria.Katuga anaiingiza serikali mtegoni, ngoja tuone.
Katuga na mabosi wake wanaompa maelekezo ni vilaza ndiyo maana hawaoni hatari iliyo mbele yao kwa uhuni wanaotaka kuufanya.Na anaiiingiza kwa kutokujua maana ana uwezo mdogo wa sheria. Katuga anapewa maagizo toka juu anayabeba kwa kuhofia kuwaambia ukweli wa ugumu wa kisheria kwani watamuona ana uwezo mdogo, hivyo anabeba hivyo hivyo akitegemea jaji ataamua kwa utashi wa serekali. Kwa bahat mbaya hata Jaji anakosa mpenyo wa kisheria wa kuibeba serekali kwani mshitakiwa yuko vizuri kisheria.
Kwa jinsi mahakama zetu zilivyo na uwezo duni kama zilivyo taasisi nyingine za umma, hii kesi imewawia ngumu, kwani uwezekano ww kutenda hila umekuwa mdogo kutokana na umahiri wa mtuhumiwa katika sheria.
Pigia mstari maneno, "...umahiri wa mtuhumiwa katika sheria."Na anaiiingiza kwa kutokujua maana ana uwezo mdogo wa sheria. Katuga anapewa maagizo toka juu anayabeba kwa kuhofia kuwaambia ukweli wa ugumu wa kisheria kwani watamuona ana uwezo mdogo, hivyo anabeba hivyo hivyo akitegemea jaji ataamua kwa utashi wa serekali. Kwa bahat mbaya hata Jaji anakosa mpenyo wa kisheria wa kuibeba serekali kwani mshitakiwa yuko vizuri kisheria.
Kwa jinsi mahakama zetu zilivyo na uwezo duni kama zilivyo taasisi nyingine za umma, hii kesi imewawia ngumu, kwani uwezekano ww kutenda hila umekuwa mdogo kutokana na umahiri wa mtuhumiwa katika sheria.
Mungu amewapiga upofu ili ulimwengu upate kujua uovu wa serikali haramu iliyojiweka madarakani kwa kumwaga damu za maelfu ya Watanganyika.Wanajiingiza mtegoni wenyewe, sijui kama wanaelewa hawa wanasheria!
Mjanja sana Lisu, hataki kabisa mambo ya 29/10 yatajwe hapa kwenye hii kesi anatumia lugha kali kuwatisha watu eti kwamba atibua mazito.Ni janja tu , anajua yakiumganishwa hayo ya 29/10 mambo yanaweza yakambadilikia.Mahakama imesikiliza hoja za upande wa mashitaka na mshitakiwa kuhusu notice inayohusiana na ushahidi wa ziada, ambapo mshitakiwa Tundu Lissu amesisitiza kwamba jambo hilo halina msingi kisheria.
Katika kesi inayohusiana na matukio ya uchaguzi mkuu wa 2025, Jaji Ndunguru alieleza kuwa hoja zote zimepitiwa na kuwa na onyo kwa pande zote: “Vijembe vyenu msivilete,” akisisitiza kuwa mshitakiwa anapaswa kuendelea na hoja zake.
Lissu, akijibu, alieleza kuwa upande wa mashitaka umeleta “open statement” inayohitaji Mahakama kuamua, lakini hatua hiyo si sahihi kwa sababu inajaribu kuongeza ushahidi wa shahidi ambaye tayari maelezo yake yamesomwa mahakamani. Shahidi huyo ni ACP Amin Mahamba, na Lissu amelekeza Mahakama kwenye kurasa mbalimbali za rekodi ya committal proceedings na rekodi ya Mahakama kuonyesha kuwa ushahidi wake tayari umesomwa.
“Notice yao haileti shahidi mpya bali inaongeza ushahidi wa shahidi aliyepo. Hii sio notice ya additional witness, bali notice ya additional evidence ambayo kisheria haipo,” Lissu alisema. Alisisitiza kuwa kuiruhusu notice hiyo kutaifungua “sanduku la Pandora” la matatizo yasiyoweza kudhibitiwa, hususan kuhusiana na matukio ya Oktoba 29, 2026.
Fuatilia mwenendo wa Keshi hapa > Kesi ya Lissu: Mahakama kujadili ombi Jamhuri kuongeza ushahidi wa ziada leo Februari 23, 2026
Lissu alisisitiza: “Wanataka tuzungumze mambo ya Oktoba 29, mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Nilikuwa jela siku hiyo, na hawa wanajaribu kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe hiyo kupitia mlango wa nyuma. Ikiwa wanataka kurekebisha taarifa, wafuate kifungu cha 294 cha CPA.”
Katuga, upande wa mashitaka, alijaribu kuingilia kuzungumzia ushahidi, lakini Lissu aliendelea kusiwe na mjadala usiofaa: “Si ndiyo anayelazimisha haya mwenyewe? Wanakatazaje nisiyazungumzie?”
Baada ya hoja za upande wa mashitaka na mshitakiwa, Lissu alikubaliana kuwa upande wa mashitaka wafanye reply au rejoinder, na yeye atamaliza hoja. Alisisitiza wazi kuwa Mahakama isiruhusu kujadili matukio ya Oktoba 29 kwani yangeibua masuala mapya ambayo yanaweza kupelekea mashitaka mapya dhidi ya Watanzania wengine.
Katika hali hii, Mahakama imebaki na hoja za wazi kutoka pande zote, huku Lissu akiweka wazi kuwa atakabiliana na lolote litakaloibuliwa ikiwa notice hiyo itaruhusiwa.
Mkitaka kujadili October samia atafungwaMjanja sana Lisu, hataki kabisa mambo ya 29/10 yatajwe hapa kwenye hii kesi anatumia lugha kali kuwatisha watu eti kwamba atibua mazito.Ni janja tu , anajua yakiumganishwa hayo ya 29/10 mambo yanaweza yakambadilikia.