Mahakama: Lissu ana Kesi ya kujibu kutokana na ushahidi wa Jamhuri uliotolewa (Agosti 21, 2026). Amtaja Rais Samia kuwa shahidi wake

Mahakama: Lissu ana Kesi ya kujibu kutokana na ushahidi wa Jamhuri uliotolewa (Agosti 21, 2026). Amtaja Rais Samia kuwa shahidi wake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Jopo la majaji watatu, wanaoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru wanaosikiliza Shauri la uhaini Namba 19605/2025 dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu wanatarajiwa kutoa uamuzi leo Agosti 21, 2026 kama Mwanasiasa huyo anayo kesi ya kujibu au hana katika shauri hilo.

Ikumbukwe, Agosti 17, 2026, Lissu aliiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia. Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Lissu alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kile alichoita "Prima facie case" (kutokuwa na kesi ya kujibu).

Alieleza kuwa Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka peke yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.
WhatsApp Image 2026-08-21 at 08.43.13.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-21 at 08.43.27.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-21 at 08.43.57.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.55.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.56ee.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.56.jpeg

Ukumbi wa Mahakama wafurika kesi ya Lissu, wengine wakosa nafasi
Ukumbi wa Mahakama Kuu unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kesi ya Tundu Lissu umejaa kufuatia wingi wa wananchi, wadau, wakiwemo wanahabari na wafuasi wa Chadema, ambao wamejitokeza kwa wingi tofauti na ilivyozoeleka.

Imeshuhudiwa takribani waandishi wa habari 50 wamefika mahakamani hapo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari vya kimataifa. Pia, viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo Makamu Mwenyekiti John Heche, tayari wamefika katika ukumbi huo.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamelazimika kukaa kwenye benchi za nje ya ukumbi wa Mahakama, huku wengine wakizuiwa kabisa kuingia ndani kwa kile kinachoelezwa kuwa ukumbi umejaa.



​
Jaji anasoma uamuzi.

Jaji anasoma kwa ufupi (summary) Ameanza kusoma viini vya makosa.

1. Mshtakiwa anatakiwa kuwa mtii kwa Jamhuri

2. Endapo mshtakiwa alitangeneza nia ya uhaini

3. Endapo alidhihirisha nia kwa vitendo au kwa umma

Kiini namba 2 na 3 ndiyi Mahakama imejikita zaidi kuchambua.

Jaji anaendelea kusoma uamuzi.

Mahakama imepitia ushahidi ambao upo katika kumbukumbu na hivyo basi,

Kwa kutambua hakujawa na ubishi kuwa maneno yaliyo katika hati ya mashtaka yakitamkwa mbele ya viongozi wa chama na wanachama

Kosa mbalo Mshtakiwa ameshitakiwa nalo

Ushahidi unamzunguza mshtakiwa kuwa alizungumza mbele yake na mbele ya watu wengine

Kutokana na ushahidi huo Mahakama haingii kwa unadani kuangalia uzito wa ushahidi au kuaminika kwa shahidi.

Kwa kuwa Mahakama haiendi kwa kiwango hiko

===========
Basi Mahakama hii inaona kwa mujibu kwa kifungu cha 312 cha kanuni ya adhabu kuna kesi iliyojengwa

MAHAKAMA INAONA KWAMBA MSHTAKIWA ANA KESI YA KUJIBU.


1787297841195.png

Mshtakiwa anatakiwa kuleta mashahidi wake wakati wa kujitetea. Mahakama baada ya kusema hivyo mshtakiwa ana haki mbili.

1. HAKI YA KUJITETEA

2.HAKI YA KULETA MASHAHIDI WAKE

3.KAMA MSHTAKIWA ATAAMUA KUKAA KIMYA MAHAKAMA INAWEZA KUWAPA UPANDE WA MASHTAKA KUTOA COMMENT ZAO

Jaji; Sasa mshtakiwa atapewa nafasi kusema kidogo kuhusu hizo haki zake ambazo nimeshamueleza

Tundu Lissu: Waheshimiwa majaji baada ya kusikiliza uamuzi wa Mahakama napenda kuijulisha Mahakama ndiyo nitajitetea

Tundu Lissu; Nitajitetea mimi mwenyewe kama shahidi wa kwanza.

Na vile vile nitaita mashahidi ambao naomba Mahakama iwapelekee summons haraka

Shahidi wa kwanza ni SAMIA SULUHU HASSAN

Ndiyo Chief Executive wa serikali inayodaiwa kutishiwa

Kwa hiyo SAMIA SULUHU HASSAN popote alipo apelekewe summons haraka

Vile vile shahidi huyu ni mwenyekiti wa baraza la usalama.

Nataka nijue kama yeye na baraza lake wanajua kuhusu hilo tishio

================

Tundu Lissu; Shahidi wa pili anaitwa Phillip Isdory Mpango. Ambapo wakati huo alikuwa Makamu wa Rais. Kiongozi namba mbili wa serikali. Upande wa utetezi unaamini kuwa ana ushahidi muhimu

Tundu Lissu; Shahidi wa tatu anaitwa Kasimu Majaliwa. Ambapo wakati matukio hayo yaliyotajwa yanatokea alikuwa ni waziri Mkuu. Kiongozi wa serikali na mjumbe wa baraza la usalama wa Taifa.

Tundu Lissu; Shahidi wa nne ni Inspekta Jenerali wa Pilisi Camilius Wambura. Mkuu wa Jeshi la Polisi. Ni mjumbe wa sekretarieti wa baraza la usalama la taifa.

Tundu Lissu; Shahidi wa tano ambaye naomba apelekewe summons ni Jenerali John Nkunda ambaye ni Mkuu wa Majeshi. Ni mjumbe wa Sekretarieti wa baraza la usalama wa Taifa.

Tundu Lissu; Shahidi wa sita ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi (TISS). Nimeambiwa kuwa katika ushahidi wa Taifa shahidi aliulizwa kama Idara ya usalama akasema ndiyo. Nataka waje waseme kuwa kama usalama wa Taifa wanajua kuhusu kesi hii

Tundu Lissu; Shahidi mwingine ni Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) nataka aje ajitetee hapa. Wote hao Waheshimiwa Majaji naomba wapelekewe wito wa mahakama (summons) haraka sana

Tundu Lissu; Wengine ambao naomba wapelekewe summons ni

1.John John Mnyika (KATIBU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO) ili atoe ushahidi wa nani aliye andaa huo mkutano.

2.Amani Sam Golugwa huyu ni NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA)

Anaweza kuwa na cha kusema huo Mkutano uliandaliwaje
Tundu Lissu; Shahidi wa 10 ni John Wegesa Heche ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Vilevile alikuwepo kwenye Mkutano wenyewe kama shahidi wa kuona na kusikia.

Tundu Lissu; Shahidi wa 11 ni Brenda Rupia. Ushahidi ulitolewa kuwa aliwaalika watu wa JAMBO TV katika huo Mkutano. Ni shahidi muhimu. Hao ni mashahidi wa kuanzia Waheshimiwa Majaji. Kama patakuwa na wakuongeza wengine nitaomba kuwaongeza mbeleni.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji nina ombi la Mwisho kabla sijakaa.

Nimekuwa na matatizo makubwa juu ya haki ya Mtuhumiwa kukutana na Mawakili wake na Mashahidi wake.

Hao ambao nimewataja kama mashahidi wanaotoka kwenye chama cha Demokrasia na maendeleo wamepigwa marufuku kunitenbelea gerezani

Pamoja na kwamba wametajwa katika mashahidi na Mahakama kuu lakini wamepigwa marufuku

Sasa Waheshimiwa majaji ili suala nilileta kwenu mapema kwamba kuna shida kuhusu Mawakili kuonana na mimi

Mkatoa ahadi kuwa wakati utakapofika mtafanya uamuzi. Sasa nimefika muda wa kufanya utetezi.

Kama sitoweza kuonana na mashahidi wangu hii haitokuwa kesi bali itakuwa kesi ya Kangaroo

Naomba faragha kuonana na mashahidi wangu. Nisisikilizwe na watu baki wakati naongea na Mashahidi wangu

Watu baki ni maafisa Magereza na wasiohusika. Wanione ila wasisikilize

Tundu Lissu;
Mwisho mawasiliano yangu gerezani yanasikilizwa na maafisa magereza na watu wa ujasusi naomba wasinisikilize naongea na mashahidi wangu. La sivyo haitokuwa fair trial. Nimemaliza kuongea.

Nipo tayari kuanza kutoa utetezi wangu kwa muda ambao nyie mtakuwa mmekubaliana

Jaji; Tuendelee

Amesimama Wakili Mkuu wa Serikali Nassoro Katuga anapekua nyaraka zake

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji upande wa Jamhhuri haupingi mshtakiwa kujitetea

Lakini upande wa Jamhuri una pingamizi kwa baadhi ya mashahidi ambao amewataja kupewa wito wa mahakama (summons)

Tunapinga kwa kifungu 314 (2) na 281 ya sheria ya mwenendo wa mashitaka ya jinai sura ya 20.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa majaji ukiangalia kifungu cha 281 cha sheria hii, Kwa ridhaa yenu nitasoma na kukitafsiri.

Kwamba Msajili wa Mahakama atalazimika ku issue summons kwa mashahidi ambao upande wa Jamhuri waliwataja katika bando kitita au aliwataja mshtakiwa Vifungu ambavyo vina control mwenendo wa kesi.

Kama hawa Mashahidi aliowataja anawataka angewataja wakati wa bando kitita. Waheshimiwa turudi katika kumbukumbu. Mstakiwa alizungumza maneno mengiiiiiiiii bila kuwataja hao mashahidi aliowasema leo.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji ukiangalia kifungu cha 364 kinasema kila hatua inayotakiwa kufuatwa katika kuongeza mashahidi.

Mashahidi ambao hajawataja wakati wa bando kitita anawataja leo. Najua aliwataja katika maelezo ya awali lakini hakutaka kuingilia wakati ule kuiwahi Mahakama.

Mshtakiwa aliwataja Mashahidi 15 leo kidogo wapo 12 lakini aliwataja 15

Upande wa Jamhuri hatukutaka kuleta mapema kwa sababu hatukutaka ku’ pre empty mahakama. Leo anawataja na anataka tupeleke Summons, tena haraka.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa hoja ya pili katika pingamizi letu tungalie neno sahihi ya neno shahidi.

Je tunayetaka kumpa hizo summons ni shahidi?

Jaji; Je, ni mashahidi wapi hao? Ungewataja hao mashahidi.

Nassoro Katuga; Mheshimiwa Majaji mashahidi wote hakuwataja wakati wa bando kitita wala kutoa anuani zao

Kifungu halisi alitakiwa kutumia ni 312. Na Mahakama ndiyo ilitakiwa kuamua.

Sasa je ni kweli ni mashahidi kwa tafsiri ya shahidi? Kwa upekee kabisa upande wa jamhuri mashahidi tunaopinga ni hawa wa kutoka serikalini. Na nitaleza kwa nini

Nassoro Katuga; Waheshimiwa majaji Pale ambapo Mahakama hii tukufu itatoa wito au summons kwa mujibu wa kifungu cha 146 ni kosa la jinai asipotii wito

Kifungu kinaelekeza Mahakama yenu tukufu itoe hati ya ukamataji.

Kwa mazingira hayo Mahakama haiwezi kutoa wito mpaka ijiridhishe kama ni shahidi muhimu Comparable na Competent

Na haiwezi kumuita mtu ambaye ushahidi wake haueleti connection na utetezi wa mshtakiwa. Mahakama haiwezi kutoa order ambayo haiwezi kutekeleza

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji mnaombwa kutoa wito kwa Rais.., haya sasa, Rais hajafika Mahakamani.., Je, mtatoa hati ya kumkamata Rais? Na Rais hajaombwa kuja kutoa ushahidi bali amelazimishwa.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji Naomba niende kwa mashahidi 3 wa Mwanzo. Nimesema mashahidi watatu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Isdory Mpango na Kassim Majaliwa

Kama nimemuelewa kuwa hawa walikuwa ni Viongozi wa serikali amabayo inamtuhumu kuwatishia Kwa mujibu wa Ibara ya 33 (2) kwamba Rais atakuwa Mkuu wa nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri jeshi Mkuu

Lakini katika ibara ya 47 (1) ina zungumzia Makamu wa Rais kuwa anafanya kazi zote za Rais kama Rais hayupo na atafanya kazi zote atakazo agizwa na Rais

Lakini ibara ya 52 inamzungumzia Waziri Mkuu ambaye yeye atafanya Shughuli za kila siku za utekelezaji wa majukumu wa serikali

Nassoro Katuga; waheshimiwa majaji

Lakini ibara ya 52 inamzungumzia Waziri Mkuu ambaye yeye atafanya shughuli za kila siku za utekelezaji wa majukumu wa serikali.

Ibara ya 35 inaeleza kuwa shughuli zote za Serikali zitatekelezwa kwa niaba ya Rais. Mpango atatekeleza shughuli zake kwa niaba ya Rais.

Majaliwa atatetekeleza shughuli zake kwa niaba ya Rais. Rais ndiye kiongozi wa serikali na amiri jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji Mashitaka yetu kwa kurejea mara kwa mara. Kwambashtakiwa alikuwa anaitishia serikali. Iwe imetishika au haijatishika.

Upande wa Jamhuri imeleta mashahidi wa serikali kutoka Jeshi la Polisi.

Wametoa ushahidi kwa niaba ya RaisKwa maneno mengine ni kwamba, kupitia wao mheshimiwa Rais ameshatoa ushahidi wake

Nassoro Katuga; Lakini nimesikia anasema anawaita Mashahidi waje waeleze kuwa Wametishika au hawakutishika. Waheshimiwa majaji ushahidi huu its material.

Aje amuulize mmoja mmoja wewe umetishika au hujatishika. It's material kwa Mahakama hii.

Kwa hiyo utaona Mahakama hii tukufu kutumia ushahidi huu siyo material kwa ushahidi huu kuja kusaidia Mahakama hii tukufuHakuna haja ya kuita Mashahidi hao.

Nassoro Katuga; waheshimiwa majajiHawa Mashahidi wa serikali ambao ushahidi wao umeshatolewa kupitia mashahidi wa serikaliAnataka awaite tena waje kutolea ushahidi dhidi ya ushahidi wa wawakilishi wao.

Ni kama anataka kuja kurudia Cross examinationKinyume na Kifungu cha 156 cha Sheria ya ushahidi kifungu kidogo cha 6. Kinataka Shahidi awe Examined in chief, Then Cross na Mwisho re examinationKinaanza kifungu cha 155 pamoja na 156

Haki ya kufanya Cross examination tena lazima uombe Mahakama imuite kama Key Witness. Kama ushahidi wake ni Muhimu wa Kuweza kuisaidia Mahakama kufikia uamuziKifungu cha 259 ndiyo sahihi.

Nassoro Katuga; waheshimiwa majaji

Kama endapo unaomba Mahakama imuite shahidi halafu aje na siyo kwamba Mahakama imuite halafu wewe uje ufanyie cross Kama unaona shahidi muhimu basi utaomba Mahakama imuite.

Waheshimiwa Majaji tunaona siyo busara Mahakama kutoa wito kwa mashahidi blindly

Kuna siku mshtakiwa ataomba Mahakama imuite Mwenyezi Mungu aje kutoa ushahidi hapa. Kwa hiyo ni upande wa Jamhuri tunaona hakufuata utaratibu kuita mashahidi

Naomba kuhitimisha kwamba maombi ya summons kwa mashahidi hawa 7 Wengine hatuna shida nao ila afuate utaratibu.

Nassoro Katuga; Amemtaja Rais kama Shahidi wake. Lakini Rais anasimamiwa na Sheria ya Presidential affairs act sura namba 9 kifungu cha 9.

Unapotoa summons ni wito wa kumtaka afike na kutii. Kifungu cha 9 (2) kina sema Subject to provision subsection 2.

Mahakamani hii haina Mamlaka katika kifungu hiki cha sheria. Kumtaka Rais afike Mahakamani au kwa shughuli yeyote ya Kimahakama. Naomba Kuwasilisha.

Anasimama Wakili wa Serikali Mwingine Job Mrema

Job Mrema;
Waheshimiwa Majaji Mahakama kuuNaomba kwanza kwa kueleza naunga mkono zote ambazo......

Jaji; Nenda kwemye hoja yako mambo ya kuunga mkono Mahakamani hayapo hapa.

Job Mrema; Waheshimiwa majaji

Section 24 ya Tanzania Intelligence and Security services act CAP 406 revised edition ya 2024

Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa kifungu hiki kinaeleza kuhusiana na usiri wa taarifaKwa kuzingatia kwamba mshtakiwa ametaja baadhi ya mashahidi kama DGIS ili Mahakama hii itoe summons afike mbele ya Mahakama hii aulizwe atakayo ulizwa

Kimsingi anataka kupata taarifa kutoka kwa mashahidi hawa ili aweze kujiteteaHususani kwa shahidi huyu anayemsema kwa cheo chake anafungwa na masharti ya kifungu hiki

Hatuoni ni busara wala siyo sahihi kwa sababu kuna limitations zimewekwa kwa mujibu wa sheria.

Job Mrema;

waheshimiwa majajiNa kifungu hiki hiki kimeweka penal Sanction kutoa kutoa siri.

Tutakuwa tunajiingiza katika mgogoro wa sheria kwa sheria ambayo nimeielezeaWaheshimiwa majaji naomba pia kufanya Marejeo ya Jacob Tibifunga ya Mahakama kuu dhidi ya Republic, Criminal Appeal ya 185 ya 1980

Mahakama kuu ya TanzaniaHii ni Reported Kesi ipo TLR ukurasa wa 125. Tumeamua kufanya marejeo ya Kesi hii. Waheshimiwa majaji mnaweza kupitia.

Job Mrema; Mahakama kuu iliweka msingi ufuatao. Naomba kurejea kama ilivyo andika.

Kwamba kuna wakati Mahakama ikiwa ina exercise mamlaka yake ina uwezo wa kukataa shahidi kuitwa.

Lakini kwa mujibu wa msingi uliotengenezwa katika kesi hii, kwamba kwanini huyo shahidi amekatakiwa kuitwa

Waheshimiwa majaji kama tulivyo eleza katika mawasilisho yetu shahidi namba 1 hadi namba 7 Mashahidi hawa wasiitwe katika shauri hili kwa sababu tulizo zieleza kama ambayo Msingi wa shauri hiki ulivyowekwa tangu 1980Waheshimiwa majaji ni hayo tu

Mahakama ipo Kimya kidogo

Majaji wanatetaTundu Lissu anajiandaa kuwajibu

Jaji; Mshtakiwa

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji naomba kufanya consultation na Mawakili wanguKuna Vifungu vimetajwa kidogo nahitaji kujadiliana

Jaji; sawa

Mawakili wanakwenda kizimbani kuteta na Tundu Lissu
  • Wakili Jebra KamboleWakili
  • Dkt. Rugemeleza Nshala
  • Wakili Dickson Matata
  • Wakili Peter Madeleka
  • Wakili Deogratius Mahinyila
  • Wakili Paul Kisabo
Wanamfungulia Laptop na kumpa Mwenyekiti Tundu Lissu asome sheriaWakati huo majaji wanateta kidogo.

Tundu Lissu; Ahsante Waheshimiwa Majaji

Nimewasikiliza Mawakili wa serikali kwa makini sana.

Naomba kujibu hoja zao kama ifuatavyo

Waheshimiwa majaji kuhusumiana na hoja ya kwanza ya Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro KatugaHoja inayohusiana na haja ya Mtuhumiwa kutaja majina na anuani za mashahidi ninao watazamia kuwaita katika utetezi wangu

Waheshimiwa Majaji hoja hii imekuwa na Mgogoro tangu kwenye Mahakama ya ukabidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Tundu Lissu; katika mahakama ya ukabidhi, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Franco Kiswaga, Baada ya kumwambia nina mashahidi na nikaanza kuwataja alikataa kuwataja na kuwa rekodi mashahidi hadharaniHoja yake ilikuwa hao utaenda kuwataja Mahakama kuu. Mimi siandiki.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji Mtakumbuka nilileta hoja kwamba utaratibu mzima wa committal Proceedings ulivurugwa kwa makusudi.

Moja ya vurugu ni kukataa kuandika mashahidi wangu

Nikasema hapa mbele ya open court hapa na mkasema nitakapofika muda wa kujitetea mkasema mtanipa fursa ya kuwaita mashahidi

Mkaomba niwatajie mashahidi na nikawatajia pamoja na anuani zao

Tundu Lissu; Nassoro Katuga anasema ukurasa wa 136.

Nahisi Nassoro yupo sahihi kuwa siku hiyo niliwataja na mliwaandika nyie wenyewe.

Na palikuwa na mjadala hapa kama Rais anaweza kuitwa au lah. Kuhusu Mashahidi ni akina nani. Ipo katika rekodi ya Mahakama hii.

Tundu Lissu; Anachokitaka Wakili wa Serikali ni kutaka mjikane nyie wenyewe.

Mkanushe ahadi yenu kwamba kutakuwa na fair trial. Kama mtaamua kujikana ni juu yenu,

Mtajua wenyewe. Yalitajwa majina ya mashahidi Kisutu, yakatajwa hapa mwaka jana leo wanasema hayajutajwa. Hii ni juu yenu mtanipa haki ya kujitetea au lah ni shauri yenu.

Mie nawashauri msijikane msimamo wenu juu ya maneno mliyosema wenyewe. Vinginevyo mtathibitisha kwamba Mahakama hii haina uwezo ku’ raise to the occasion katika kesi kubwa namna hii. Msikubali Mahakama hii igeuzwe kuwa Mahakama ya Kangaroo.

Tundu Lissu;

Sasa waheshimiwa majaji hoja ya kifungu cha 281 na 314 (2) haiwezi kutumika tena. Mlishaandika majina ya mashahidi wangu. Hii hoja imeshakuwa overtaken by your own order.

Don’t Revise yourselves.

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji kuna hoja imeletwa hapa kwamba kuna mashahidi ambao hawawezi kulazimishwa kuja Mahakamani. Waheshimiwa Majaji ni issue ya who is Compellable Witness.

The Compellable Witness ipo katika sheria ya ushahidi. Sheria ina sema mashahidi wote ni Compellable isipokuwa wale ambao wametajwa hawawezi kuja Mahakamani.

Tundu Lissu; Na sheria ya Presidential Affair inasema Rais hawezi kupelekewa summons Ikulu na Mikoani lakimi sheria inasema kama kuna summons inaweza kupelekwa kwa katibu Mkuu Kiongozi au personal secretary wa Rais aisaidie Mahakama kumfikiishia Rais hiyo summons.

Huwezi tu kumpelekea moja kwa moja. Inabidi umpelekee kupitia katibu Mkuu Kiongozi au her Personal secretary. Huwezi kumlazimisha lakini unaweza kumpelekea in-direct.

Halafu yeye ataamua aheshimu wito wa Mahakama au asi-uheshimu huo wito wa Mahakama. Section 9 should be read together with Section 10 of Presidential affairs act.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji Mmeambiwa hapa eti msiwaite mashahidi ambao hawatokuja. Kwa maneno mengine Mawakili wa Serikali wanajua hao wakubwa wa serikali niliowataja hawatokuja.

Kwamba nisimuite Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Anasimama Wakili Mkuu wa Serikali Nassoro Katuga Waheshimiwa Majaji sisi hakuna sehemu tuliyosema hawatokuja mahakamani.

Tundu Lissu; Waheshimiwa najaji sijui kama wakili wa serikali anajua contempt of the court.

Nilichokuwa nasema ni maneno yake yeye aliposema kwamba msi’ issue summons kwa sababu hawatokuja.

Wao wamejuaje kwamba tukiwaita kwa utaratibu wa sheria hawatokuja

Nassoro Katuga; Kwa kweli sisi hatujasema kwamba hawatokuja.

Jaji; Wakili wa Serikali hiyo ni tafsiri yake mshtakiwa na huwezi kulazimisha afikiri kama wewe

Tundu Lissu: Waheshimiwa Majaji hawajasema kwanini wakiitwa hawatokuja na hata kuulizwa maswali hawajaulizwa unajuaje hawatokuja

Waheshimiwa Majaji waitwe na wapelekewa summons na Rais aamue kwamba hatokuja kutoa ushahidi wake mbele ya MahakamaniHiyo inamuhusu Rais.

Vipi kuhusu Makamu wa Rais mstaafu? Waziri Mkuu mstaafu?

Wanaofanya kazi kwa niaba ya Rais kwa taarifa zangu kwa sasa hivi ni Dkt. Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba

Waliokuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Rais mwaka jana hawawezi kuacha kuja kwa sababu siyo wasaidizi wa Rais tena.

Na Mkuu wa Polisi? Mkurugenzi wa Idara ya ujasusi na Usalama wa Taifa? Hawa siyo Compellable Witness.? Kwa sheria ipi siyo compellable witness?

Tundu Lissu; Kwa hiyo Waheshimiwa Majaji hakuna afisa yeyote wa Serikali ambaye hawezi kupelekewa summons.

Wala siyo Rais wala siyo Makamu wa Rais Mstaafu wala siyo waziri Mkuu Mstaafu wote hao wanawajibika mbele ya Mahakama.

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji mmeambiwa kwamba hawa wote ushahidi wao siyo material. Nilisema wakati nawataja majina. Rais ni mkuu wa Serikali.

Wakili wa serikali Mkuu amesema Rais ni Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Shtaka linalonikabili linasema nimetengeneza nia ya kuitishia serikali.

Mtu ambaye kosa linamlenga moja kwa moja anawezaje asiwe na ushahidi ambao relevant? Unapozungumza Rais ndiyo Serikali. Ushahidi wake unaachaje kuwa relevant?

Kilichopo hapa hii hoja ni jitihada ya kuhakikisha kwamba Rais anakuwa Juu ya Sheria. Asionekane kwamba anaenda Mahakamani.

Jaji Mkuu Barnabas Samata amewahi kunukuliwa akisema kwamba Rais yupo Juu ya sheria inakiuka Katiba

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji Rais ambaye ni Chief Executive wa serikali ambaye kwa katiba ni Serikali anakuwaje na ushahidi irrelevant kwa kosa la kupindua serikali yake?

Na hoja hiyo haimuhusu Makamu Rais mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu na wote niliowataja. Niliye mtaja ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa na waliokuwa wajumbe wa baraza la usalama wa Taifa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wa taifa ni Wajumbe wa sekretarieti ya baraza la usalama wa Taifa. Ni namna ya kutaka kujua tu wanajua nini juu ya mashtaka haya.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji mkitoa summons kwa Rais asipokuja ni wazi hamuwezi ku’ issue arrest warrant. Hiyo ipo wazi lakini haiwezi kuwa sababu kutokutoa summons. Summons haiwezi kuacha kutolewa kwa sababu unajua hatokuja.

Iende halafu isipokuja sisi raia wake tutajua Rais wetu anajua yeye ni MALKIA ambaye yupo juu ya sheria.

Tundu Lissu; Hao wengine (Mpango na Majawaliwa) wakidharau summons wanatolewa hati ya kukamatwa na Polisi. Mkuu wa majeshi anakamatwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi anakamatwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anakamatwa kwa sababu wao hawapo juu ya sheria na hawana Kinga.

Tundu Lissu; Kuhusu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Hii ni hoja ya Wakili Job Mrema. Naomba niwasomee sheria ya usalama wa Taifa kuhusu siri.

Kifungu 24 kinachozuia kutoa taarifa zitakazofanya sources wa Idara ya usalama wa Taifa wajulikane. Hiko kifungu kina zuia wanaofanya kazi idara ya usalama wa Taifa wasije Mahakamani?

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji sina hakika Mawakili wa Serikali walikuwa wapi wakati wa kesi za uhaini za 1980. Palikuwa na ‘ajenti’ X kama shahidi.

Ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Alikuja kujisema mwenyewe kuwa ni Mahiga. Vijana wengi wanamjua kama Waziri wa Magufuli. Na mashahidi wengine walikuwa ni Watu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Hoja yao haina msingi wowote in fact katika sheria.

Tundu Lissu; In fact kosa kubwa kuliko lote katika nchi unaeezaje kusema Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa hana ushahidi wowote. Ni hoja ya bureeee kabisa. Particularly in Treason case ya namna hii.

Tundu Lissu; waheshimiwa majajiMmeambiwa Mtuhumiwa anataka hao waje ili aje kuwa Cross examine. Waheshimiwa Majaji hiyo hoja kama ingekuwa na maana yoyote angesema kama Wakili Nassoro Katuga nimekaa naye akanisikia. Sasa nakutana naye Mahakamani tu.

Anajuaje kama nataka kuja kuwa cross examine? Nataka waje ni wa examine in-chief. Wao wanajua zaidi Kuliko Mr. katuga au hili Jopo la Mawakili. Kwenye masuala ya uhaini they know better than hawa mawakili. Akija Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ushahidi wake utakuwa muhimu sana.

Aje afanye alichofanya marehemu Mahiga. Kama wanahisi kuna siri za nchi kuna utaratibu wa mashahidi wa kificho.

MAHAKAMA YOTE; 😂😂

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji.Nataka niwape kifungu. Kifungu 192 (1)b Roman one cha sheria ya mwenendo wa Jinai. Mahakama inafanyeje panapokuwa na ushahidi wa namna hii.

Mahakama inatumia kifungu hiki kusitiri mashahidi. Kama Mawakili wa Serikali wana wasiwasi kama siri za usalama wa Taifa zitazungumzwa na sijui wanatoa wapi huo wasiwasi na wao siyo Watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Hasa katika kesi kubwa mbili za uhaini za Mwaka 1980.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji hoja imeletwa hivi kwamba Mashahidi wote waliotoa ushahidi wametoa ushahidi kwa niaba ya Rais.

Eti kwa sababu tu ni Watumishi wa Serikali. Waheshimiwa Majaji hoja hiyo vilevile haina msingi wowote kisheria na Msingi wowote in fact. Kama ingekuwa kweli kwamba Rais hawezi kutoa ushahidi pale ambapo watumishi wa serikali wa wametoa sheria ingesema hivyo Simple.

Sheria yetu haisemi hivyo. Sheria yetu inasema unapotaka Rais atoe ushahidi unapeleka summons kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Personal assistant.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji.Nataka niwape kifungu.

Kifungu 192 (1)b Roman one cha sheria ya mwenendo wa Jinai. Mahakama inafanyeje panapokuwa na ushahidi wa namna hii. Mahakama inatumia kifungu hiki kusitiri mashahidi.

Kama Mawakili wa Serikali wana wasiwasi kama siri za usalama wa Taifa zitazungumzwa na sijui wanatoa wapi huo wasiwasi na wao siyo Watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Hasa katika kesi kubwa mbili za uhaini za Mwaka 1980.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji hoja imeletwa hivi kwamba Mashahidi wote waliotoa ushahidi wametoa ushahidi kwa niaba ya Rais.

Eti kwa sababu tuh ni Watumishi wa Serikali. Waheshimiwa Majaji hoja hiyo vilevile haina msingi wowote kisheria na Msingi wowote in fact. Kama ingekuwa kweli kwamba Rais hawezi kutoa ushahidi pale ambapo watumishi wa serikali wa wametoa sheria ingesema hivyo Simple.

Sheria yetu haisemi hivyo. Sheria yetu inasema unapotaka Rais atoe ushahidi unapeleka summons kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Personal assistant.

Tundu Lissu; Wakili anasema Rais hawezi kutoa ushahidi na huku anasema Rais ameshatoa ushahidi WHICH IS WHICH?

Rais anaweza kutoa ushahidi kama Mwenyekiti wa baraza la usalama wa Taifa. Mkuu wa Jeshi la Polisi atatoa ushahidi kama Member wa baraza la usalama wa Taifa.

Mkuu wa Majeshi hivyo hivyo. Hawaji hapa kwa sababu ni Wateule wa Rais bali wanakuja kama Wajumbe wa hizo taasisi.

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji Mmeambiwa msiite mashahidi blindly. Kwamba mkiita mashahidi blindly kuna siku mshtakiwa ataomba Mahakama imuite Mwenyezi MunguHaya ni maneno ya wakili wa serikali anayeamini Rais ni sawa na Mungu

Hawa wanaitwa kwa sababu ni wajumbe wa baraza la usalama la Taifa na wanaweza kutoa ushahidi wala siyo MiunguMarehemu Rais Mkapa alitoa ushahidi katika kesi ya Profesa Mahalu

Alishastaafu, ndiyo, kwa namna hiyo Phillip Mpango anaweza kutoa ushahidi kama Mkapa

Wakili Nassoro Katuga kasimama kama kajerujiwa hapa anasema Tundu Lissu anafanya rejoinder na analeta vitu vipya

Tundu Lissu; Mheshimiwa Jaji mimi na reply objection yake baada ya mimi kutaja Mashahidi. M

Jaji; tuwe wasikivu hata kama jambo hulipendi. Tuendeleeni

Tundu Lissu; Lissu: Mheshimiwa Jaji Kwa sheria za Tanzania hakuna utaratibu wa Mtu kutoa ushahidi kwa niaba ya mtu mwingine. Hakuna utaratibu wa Rais kutolewa ushahidi na mtu mwingine.

Ndiyo maana kifungu cha 9 na 10 cha sheria ya masuala ya Rais inasema hiyo summons utapeleka kwa wasaidizi wake. Ingekuwa Rais anatolewa ushahidi na mtu mwingine sheria ingesema hivyo?

Kwa hiyo ushahidi wa akina Mahamba ni ushahidi wao wala siyo kwa niaba ya mtu mwingine. Kama Rais ataona kuna irrelevance muache aseme yeye, atoe ushahidi yeye wala siyo wewe from the bar.

Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji kesi ya Jacob ambayo kama nimewasikia sawasawa. Wakili Job Mrema amesema Hakimu anayo mamlaka ya kukataa kuita shahidi pale ambapo shahidi hana uhusiano na kesi iliyopo Mahakamani ili mradi Hakimu aandike sababu za kumkataa Shahidi. Waheshimiwa majaji hii kesi ina ina uhusiano gani na Mahakama hii?

Hii kesi ya Mahakimu ina uhusinao gani na Majaji kujifunza kwa Mahakimu? Pia inasema kama ushahidi hauna uhusiano na kesi. Je, katika kesi kubwa kuliko zote kesi ya uhaini kesi inayohusu baraza la usalama haina uhusiano.?

Je kesi ya serikali inayodaiwa kutishiwa haina uhusiano na baraza la usalama

Tundu Lissu; Je Mkuu wa Polisi,Mkuu wa majeshi na Mkuu wa idara ya usalama wa Taifa hawa wote wajumbe wa Sekretariati kwamba haina uhusiano na uhaini.?

Hata kama kesi ya Jacob ipo sahihi lakini katika kesi hii haipo sahihi. Kwa sababu niliowataja wana uhusiano wa moja kwa moja

Tundu Lissu; Hakuna sheria inayozuia mashahidi niliowataja wasipelekewe summons. Akikataa ni suala jingine. Na wengine wote hao wanaweza kupelekewa Summons.

Pili Waheshimiwa majaji ushahidi wao ni muhimu sana. Kama kweli kulikuwa na matishio kwa serikali yanayodaiwa waseme. Tatu Waheshimiwa majaji nawaombeni msimamie kauli zenu.

Mlisema niwatajie majina ya mashahidi ninaotaka kuwaita nikawataja na mkawarekodi. Umefika wakati wa kutekeleza mlicho’kirekodi na wakati ni sasa.

Ni sasa hivi. Ni watu wakubwa ndiyo. Lakini hizo nafasi zinazowapa ukubwa ndiyo zinahitajika kuja kueleza ukweli.

Tundu Lissu; Kwenye sheria za nchi hii Watuhumiwa wa makosa Jinai wana haki ya kutendewa FAIR TRIAL. Wana haki ya kuwezeshwa na Mahakama mashahidi kuitwa.

Kama hamuwezi kuwaita mashahidi kwa hofu za waendesha mashtaka wa serikali basi hapatakuwa na fair trial. Kama hapatokuwa na fair trial ni Mungu tu ndiyo anajua Mahakama itaonekanaje kwa kuzuia mashahidi. Lindeni haki za mshtakiwa.

Lindeni hadhi ya Mahakama na lindeni fat trial.

NIMEMALIZA

Mahakama ipo kimya kiduchu


Jaji;
Tuendeleeeeeeeee

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji Tuanze na kauli ya mwisho ambayo mshtakiwa amemalizia. Kwamba msitoe uamuzi kwa kuogopa hawa waendesha mashitaka.

Maneno haya yamesemwa ili kuitisha Mahakama Ili isitoe uamuzi sahihiTusiende sana huko ila Mahakama itaangalia kama anaweza Kutisha Mahakama anaweza pia kutisha Serikali. Waheshimiwa Vifungu vya sheria vipo not for cosmetics

Nasoro Katuga; waheshimiwa majaji

Tumeialika Mahakama katika vifungu siyo katika Vitisho.

Mahakama haipaswi kuacha kutumia vifungu vya sheria ili kumfurahisha mtu. Sisi tunasema Mashahidi hawakutajwa mahakama ya hakimu mkazi KisutuNa Kumbukumbu zipo na ndiyo zinatumika. Na kumbukumbu ambazo Mshitakiwa alipewa.

Mshtakiwa akisema leo alisema haikuandikwa haisaidiiKusema kwamba nikisema na haipo katika kumbukumbu za Mahakama ni kutaka kutia huruma na huruma siyo malezi

Jaji; Naomba tutulie

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Vifungu hivi vingekuwa siyo upande wa Jamhuri ingekuwa vitamu. Nimevitaja vifungu hapa mshtakiwa hajavitaja vifungu wala kuvipinga

Tundu Lissu anasimama

Tundu Lissu;
Waheshimiwa majaji reference yeyote aliyosema kuwa natishia Mahakama na kwamba naomba huruma viondoleweKama hakuna sehemu nimesema natishia majaji au kutaja maneno huruma viondoleweKama vitabaki nitaomba kujibu

Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji natoa tafsiri kama alivyokuwa anatoa tafsiri. Yeye kasema kwamba msitoe uamuzi kwa kuogopa Mawakili wa Serikali. Kwa maneno haya natafsiri kwamba anatishia Mahakama

Jaji; Naombeni tutulie hata kama Wakili anasema usichokipenda vumilia. Tukiku’ point tutakuchukulia hatua.

Naomba tuendelee..

Nassoro Katuga: Ahsante Waheshimiwa majaji. Mimi nimetoa kifungu na kueleza kwamba hao Mashahidi hawapo katika kumbukumbu za Mahakama

Hoja ya kwamba alisema hawakuandikwa yeye anajua utaratibu wake. Mshtakiwa anajiwakilisha kwa sababu ni MJUVI wa sheria.

Nassoro Katuga; Hoja ya kwamba aliwataja hawakuandikwa ni hoja ya after thought baada ya sisi kusema yeye hakusema kabla. Kama wewe ni mjuvi wa sheria baada ya kuwa served ulitakiwa kuanzakujiuliza je nilivyo vitaja vimeandikwa..?

Kwa hiyo hoja ilipaswa ifanyiwe kazi kabla ya Kusikilizwa na siyo issue ya kutia huruma hapaRekodi za Mahakama ndiyo zinasema Mashahidi hawa hawakutajwa

Nassoro Katuga; Mheshimiwa kutaja Mashahidi wakati wa PH siyo takwa la kifungu cha 281. Lakini pia siyo takwa la kifungu cha 198.

It's has been a practice. Kwakuwa yeye hakutaja sisi hatuku pre empty tukasema tuone je ata comply kifungu 281. Kwamba kwa sababu aliwataja katika PH na nyie mkaandika basi ndo atawaitaManeno ya Kwamba msikane uamuzi wenu..,

Tumepitia maamuzi yenu hakuna order yoyote kwamba amewataja mashahidiHapakuwa na order juu ya Mashahidi. Hapakuwa na comment ya upande wa mashtaka kuhusu mashahidi. Sheria zipo tu.Mlikuwa wabunge mkashindwa kurebishaa

Tundu Lissu anasimama…… Waheshimiwa Majaji.

Nassoro Katuga; Waheshimiwa naomba kuifuta hiyo imenitoka tu hata nyie nina imani hamjasikia

Nassoro Katuga; Naomba kuendelea. Kwamba suala la Serikali kutishika au kutotishika ni immaterial. Ndiyo maana tukaenda mbali kwamba anasema kusudia kuwa cross dhdi ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri

Sisi hatujatishia Mahakama bali tumeona Mahakama itumie mamlaka yake kuona hawa Mashahidi siyo wa muhimuSuala la kutishika au kutokutishika ni immaterial.

Mahakama iangalie umuhimu wa ushahidi. Na uzuri mshtakiwa amefunguka ameeleza anachotaka kuitia ni nini.

Nassoro Katuga; Tukaenda mbali tuka taja vifungu vya katiba.

Yale maneno kwa niaba ya kwa niaba ya Rais sijui kwanini haya tafsiriwi sawasawaKwa tafsiri rahisi kama yule alifanya kwa niaba ya Rais ni wazi kwamba kile alifanya kwa niaba ya Rais

Kwa sababu yule ni mfanya kazi wakeSijui kwa nini anasema anataka kunyongwa, adhabu zipo nyingi iliwemo conditional dischargeSijui kwanini hazitajwi

Nassoro Katuga; Mashahidi wakiitwa ndiyo tunasema hawawezi kuitwa kuwa examine kutoka upande mwingine baada ya subordinates wao kutoa ushahidi. Wao walishasema kuwa palikuwa na kuvunja amani.

Tundu Lissu: Hilo Waheshimiwa majaji naomba kulijibu kwa sababu hilo ni kosa tofauti na ninalo shtakiwa la kutishia amani

Nassoro Katuga; sijasema umevunja amani nimesema narejea kama mashahidi waliopita wameongea hivyo huwezi kuwaita mabosi wao uwahoji tena kutoka upande wako

Nassoro Katuga; Waheshimiwa majaji hoja ya hawa mashahidi 7 kwamba wakipewa summons hawatokuja.., Sisi tulijikita kwa Mheshimiwa Rais pekee.., Wengine wakiitwa wakikataa itatoka arrest warrant. Sasa sisi tunasema Mahakama lazima itoe summons inayotekelezeka

Nassoro Katuga; Na mshtakiwa amesema kwamba Rais asipokuja Mahakama haiwezi Kutoa arrest warrant sasa hiyo summons ya nini au just for cosmetics tu?

Waheshimiwa Majaji nimeshawishiwa ku issue summons kwa Rais nikirejeshwa kwa Kesi ya MahaluLakini Marehemu Mkapa alikuwa mstaafu wakati anaenda kutoa ushahidi tofauti kumfananisha na Rais wa sasa ambaye yupo MadarakaniNi mazingira ambayo ni tofauti.

Lakini ni utashi Mheshimiwa Rais mwenyewe

Nassoro Katuga; Lakini hatuelezwi kwamba Mahakama ilihangaikia materiality ya ushahidi wake? Kila kesi itaamuliwa kwa Mazingira yakeHata sisi tunasema hawa Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu tunaangalia dhumuni lake na umuhimu wa ushauri wake.

Ingekuwa vifungu vilivyotumika dhidi ya serikali ingekuwa the same basi. Waheshimiwa kwa upande wangu naona niishie hapa

Wakili wa serikali Mkuu Mwinuka; Nilitoa ufafanuzi kuhusiana na sheria ya masuala ya Rais sura ya 9. Mshtakiwa anasema kifungu cha 9 na 10 vinapaswa kusomwa kwa pamojaRai yetu ni vifungu viwili tofauti na haziwezi kusomwa kwa pamoja. Sisi tunaona kifungu cha 9 Kinazuia Kum’ require au ku’ compel Rais kuja Mahakamani

Kifungu cha 10 kinaeleza Makazi ya Rais (state house) katika kutoa nyaraka na hakisemi latika kutoa summons wala hakizungumzii katika compelling ya PresidentKwa vyovyote vile vifungu vya 9 na 10 haviwezi Kusomwa kwa pamoja.

Mahakama inazuia kumetaka au kumleta Rais katika Mahakama hiiWaheshimiwa majaji tunaomba Pingamizi letu ambalo tumewasilisha liamuliwe kwa usahihi

Jaji; Tumesikiliza pande zote mbili Na upande wa serikali wanasema hawana pingamizi kwa shahidi wa 8 hadi 11 Kwa sababu hawa John Heche, John Mnyika na Brenda Rupia kwa kuwa hawana pingamizi waendelee na ushahidi, wakati tunaendelea kufanyia kazi uamuzi Kuhusu hao mashahidi 7 wengine mahakama ipewe muda itaamua

Tundu Lissu: Mheshimiwa Jaji njliomba ruhusa ya kushauriana na mashahidi na mawakili. Kimsingi Mheshimiwa Jaji siyo mazungumzo marefu lakini Mahakama ijue sijazungumza nao tangu mwaka jana November Kwanza, nizungumze nao halafu tuendelee

Jaji; upande wa mashtaka kuna lolote la kusema?

Wakili wa serikali: Hakuna pingamizi.., Lakini tunaomba Mahakama ihairishwe hadi Jumatatu ili kumpa muda wa kujiandaa

Tundu Lissu: Waheshimiwa majaji mimi nipo sensitive sana na maombi ya kuhairisha hairisha sana. Mimi nina mwaka mmoja na nusu gerezani Naunga mkono pendekezo la health break lakini kama mtaridhia waheshimiwa majaji naomba tuanze.

Kama nilivyosema mimi nipo tayari.

Jaji; Kimsingi hata sisi tunona twende health break la turudi kuendelea.., Muda wa health break ndiyo utaongea na mawakili wako na mashahidi wako bila kuathiri mambo ya kiusalama.

Mahakama imehairishwa Jaji amesema ni ‘healthy Break’Kwenye futiboli tunaita ‘water break’World Cup 2026 wameita ‘Hydration Break’Tukirejea, Mashahidi wa Tundu Lissu ambao hawajawekewa mapingamizi, wataanza kutoa ushahidi wao.

Tundu Lissu anasimama kama shahidi namba moja katika kesi yake na anaanza kujieleza;

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji Kama ambavyo nimesema. Mimi ni kiongozi wa chama cha siasa kilichoandikishwa rasmi kwa mujibu wa sheria.

Nafasi yangu ya sasa na nafasi niliyokuwa nayo wakati haya yanatokea ni nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA. Nimekuwa mwenyekiti wa CHADEMA tangu tarehe 22 January 2025, kwa maneno mengine, nimekaa kwenye nafasi hiyo ya mwenyekiti wa Chama kwa takribani wiki tano au sita ndio nikakamatwa na kushtakiwa kwa kosa hili.

Na hilo nitaonesha maana yake nini baadae. Kwa sasa rekodini hivyo hivyo.

Tundu Lissu; Waheshimiwa majaji kabla sijachaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA, nilishikilia nafasi ya makam mwenyekiti bara kwa kipindi cha miaka mitano kuanzi Dec 2019 mpaka Jan 22 2025 nilipochaguliwa kuwa mweyekiti wa Chama Taifa.

Kabla ya hapo nilikuwa mwanasheria wa CHADEMA na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama. Kati ya mwaka 2010 hadi 2017. Specifically hadi tarehe 7 sept 2017. Na ndio tarehe muhimu waheshimiwa majaji, tutairudia tena baadae.

Lissu aanza kujitetea

Mahakama imerejea saa 9:46

Lissu ameshakaa sehemu yake. Majaji wameingia saa 9: 47

Jaji Ndunguru: upande wa mashitaka?

Wakili Ajuaye Nzengeli: Waheshimiwa majaji baada ya mapumziko sasa tuko tayari kuendelea. Quorum iko vilevile.

Lissu: Waheshimiwa majaji mashahidi wangu mliowaruhusu wako ndani ya mahakama, sasa naomba maelekezo kama wanaweza kuwa ndani au watoke nje?

Jaji Ndunguru: Ni utaratibu wa kawaida tu, shahidi mmojabakitoa ushahidi wengine wanatakiwa kuwa nje.

Mashahidi: Mnyika, Heche, Golugwa, Brenda wanatoka nje.

Jaji Ndunguru: Wewe ndio mshitakiwa unaeza kuamua nani aanze.

Lissu anahamishwa kizimba ha kulia wanakosimama mashahidi.

Jaji Ndunguru; Shahidi tuambie jina lako

Lissu: Naitwa Tundu Antiphas Lissu (anataja her herufi moja moja)

Jaji Ndunguru; Umri wako
Lissu: miaka 59
Jaji Ndunguru: kazi yako
Lissu: Wakili wa mahaka kuu na kiongozinwa chama, mwenyekiti.
Dini Yako: Mkristo Katoliki

Jaji Ndunguru: Utakula kiapo
Lissu: nitaapa lakini itabidi mnisaidie maana kwa muda mrefu sijatoa ushahidi. Nimekuwa wakili kwa muda mrefuila sikula kiapo.

Jaji Ndunguru anamlisha kiapo.

Lissu: Waheshimiwa majaji kwankiasi kikubwa yatakuqa ni ya maisha yangu. Mimi ni kiongozi wa chama cha siasa na kazi yangu ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kuna simu inaita, watu wamegeuka kuke kwenye jukwaa la nyuma.

Jaji Ndunguru: Tumfanye nini? Au tumzomee aone aibu? (Watu wanacheka).

Lissu: Wahemiwa majaji nimekuwa mwenyekiti wa Chadema tangu Januari 22, 2025. Kwa hiyo nimekaa kwenye nafasi hiyo kwa takribani wiki 5 ndipo nikakamatwa na hilo nitaonyesha maana yake nini baadaye.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema nilikuwa makamu mwenyekiti kwa miaka mitano tangu septemba 2019 mpaka 2025.
Kabla hapo nilikuwa mwanasheria mkuu wa Chadema na mjumbe wa kamati kuu ya chama kati ya mwaka 2010 hadi Septenba 7, 2017.
Kabla ya hapo nilikuwa Mkurugenzi wa sheria, katiba na haki za binadamu wa Chadema tangu tajribani Julai 2004 nilipojiunga na Chama hadi Novemba 2011. Nafasi hiyo ilinifanya kuwa ex-officio member of Central Committee.
Kwa ushahidi huu mimi ninekuwa katika uongozi wa Chadema katika nafasi za juu mwa takribani miaka 20.
Nje ya uongozi wa chama vilevile nilishikilia nafasi nyingine za uongozi kama ifuatavyo.

Mwaka 2010 nilichaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano nikiwakilisha jimno la Sibgida Mashariki siku hizi linaitqa Ikungi Mashariki na nilichaguliwa kwa tikieti ya Chadema.
Nilichaguliwa tena kwejye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 na nilitumikia nafasi hiyo hadi Juni 29, 2019.
Ilikuwaje, narudi kwenye Septemba 7, 2017, siku hiyo nikiwa Dodoma kwenye vikao vya Bungenilifuatwa kutoka Bungeni mpaka kenye makazi yangu binafsi na kushambuliwa na risasi nyingi sana na watu ambao serikali ya Tanzania inawaita wasiojulikana.

Kufuatia shambulio hilo, nilikimbizwa hospitali ya Dodoma na niksafirishwa.kqa ndege mpaka Nairobi Kenya ambako nilikaa hadi Januari 4, 2018 miezi minne kamili, baada ya hapo nilipelekwa Ubeligiji kwa matibabu zaid9 katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven.

Nilitibiwa katika hospitali hiyo mpaka Januari 2022. Nilikuwa nakwenda kwa surgery narudi.
Kati ya Nairobi na Leuven nilifanyiwa operesheni 25. Operesheni 17 Nairobi hosoital na operesheni 8 Leuven.
Waheshimiwa majaji mkiona navuta mguu ninapotembea ni kwa sababu ya majeraha hayo.

Juni 29, 2019 Marehemu Job Yustino Ndugai alitangaza kunifuta ubunge kwa sababu sijaonekana Bungeni sababu aliyoitoa alisema ni mtoro.

Hiyo sababu iliyofanya nikashindwa kumalizia muhula wa pili wa ubunge wangu. Katika kesi hii, licha ya kuwa mbunge na kuumizwa vibaya nikiwa bungeni, Bunge na serikali ya Tanzania walikataa kata kata kulipia matibabu yangu.

Licha ya sheria ya uendeshaji wa Mbunge kuelekeza kwamba Mbunge akiugua au akipata matatizobya kiafya anatobiwa na Bunge, walikataa.

Nikiwa bungeni nilikuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, kiongozi wa pili kambi hiyo Kiongozi akiwa kiongozinwa kambi rasmi ya upinzani bungeni, mheshimiwa Freeman Mbowe.
Vilevile nilikuwa msemaji mkuu wa kambi hiyo wa masuala ya katiba na sheria na mwanasheria mkuu kivuli.
Waheshimiwa majaji naomba mahakama irekodi kwamba nilifanya kazi yangu ya ubunge kwanumari na heshima kubwa.
Kipindi hicho hicho kuan@ia 2011 mpaka 2015 nilikuwa mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na kwa kipindi hicho 2011 - 2017 niliongoza mapambano ya katiba mpya na mfumo huru wa uchaguzi. Hivyo kilichonileta hapa sio uhaini, bali ni mapambano ya kudai katiba mpya na mfumo huru wa uchaguzi. Ni mapmbano ya kisiasa.
Niliongoza mapambano hayo kwa umahiri mkubwa.
Waheshimiwa majaji, nje ya ubunge ninekuwa rais wa chama cha mawakili wa Tanganyika, tangu Machi 2017 mpaka September 7, 2017. Hauwi rais wa chama cha mawakili kama wewe ni mtu qa hovyo hovyo, mhaini.
Nje ya uongozi wa mawakili wenzangu, hapa nilipo ni makamu mwenyekiti wa vyama vya kidemokrasia duniani (International Democrats Union) shirikisho linalounganisha vyama zaidi ya 80 vya kisiasa duniani. Vikiwemo vyama vinavyotawala huko Ulaya (Ujerumani, Republican US na kwingineko.
Mimi makamu mwenyekiti ninayewakilisha bara zima la Afrika.
Ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima, ninaheshimika ndani ya nchi hii na kimataifa.
Heshima niliyonayo ni kwa sababu ya kupigania haki, demokrasia na utawala sio kwa.sababu nyingine.
Mei 2011 nilipewa tuzo ya heshima ya kuwa mwenza kimataifa International fellow wa chuo kikuu cha Bridgeford kipo jimbo la Connecticut nchini Marekani.

Sababu ya heshima hiyo ni muhimu kuiweka kwenye recoding kwa sababu chuo hicho kilisema ni sababu ya kupigania haki za binadamu, mazingira na demokrasia nchini Tanzania na barani Afrika.
Desemba 2020 nilitunukiwa heshima nyingine na IDU tuzo inayoitwa Bush Thatcher Award. Nilipewq tuzo ya Rais wa 41 wa.Marekani George Bush senior na Margaret Tharcher wa Uingereza. Citation ilisema, Tundu Lissu umekuwa ni kielelezo cha msimamo thabiti wa kupigania haki demokrana utawala bora katika nchi za Afrika.
Ni muhimu vilevile uingize kwenye ushahidi wangu kwamba pamoja na kukaa gerezani muda wote huo, heshima yangu katika nchi hii na duniani, haijapungua, in fact imeongezeka.

Taasisi nyingi sana za kitaifa, kikanda na kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiyabya Ulaya, Jumuiya ya Madola wamesema haya ni mashitaka ya kisiasa, hakuna jinai yoyote na yamedai niachiliwe huru hila masharti yoyote.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu Uswisi limesema sio tu niachiliwe huru, bali nilipwe fudia kwa usumbufu qote nilioupata.
Naomba iingie kwenye ushahidi kwamba, nchi za Jukuiya ya Ulaya zimesimamisha kisaada kwa Tanzania kwa sababu ya kesi hii na Marekani imesimamisha misaada ya Millennium Challenge Account takriban milioni 700 kwa sababu ya mashitaka haya.
Kwa sasa bunge la Marekani linajadili muswada wa kuiwekea Tanzania vikwazo kwa.sababu ya mashitaka haya.
Waheshimiwa majaji dunia haiwezi kukupigania hivi kama wewe ni mtu wa hivyo hovyo. Dunia haiwezi kukupigania kama wewe ni mhalifu. Dunia inakupigania kwa sababu wewe ni mtu wa heshima.

Waheshimiwa majaji shitaka dhidi yangu linahusu kauli niliyoitoa Aprili 3, 2025 kuhusiana na uchaguzi mkuu.

Jaji Ndubguru: Imefika saa 11 sasa tulikiwa tunashauriana hapa tuahirishe mpaka Jumatatu.

Wakili wa Serikali Nzengeli: Waheshimiwa majaji nadhani sasa tufike mwisho tuahirishe mpaka jumatatu.

Lissu: Kuna mambo naomba yaingie kwenye recoding ka la hatujafunga

Mimi nina uzoefu mkubwa sana na masuala ya uchaguzi ya Tanzania. Nilipiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Oktoba 1985 nikiwa na umri wa miaka 18. Kati ya mwaka 1985 na mwaka jana nimeshiriki katika uvhaguzi mkuu kama mgonbea au mpiga kura katika chaguzi zote isipokuwa uchaguzi wa 2000 na yale maafa ya mwaka jana kwa sababu nilikuwa gerezani.
 

Attachments

  • Screenshot 2026-08-21 081436.png
    Screenshot 2026-08-21 081436.png
    1.1 MB · Views: 40
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea leo Agosti 21, 2026, ambapo ambapo Majaji watatu wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam wataamua kama ana kesi ya kujibu au la.
Yes,
kibaraka ana kesi ya kujibu 100%, na kwahivyo ataendelea kusota korokoroni bila mbambamba yoyote my friends, ladies and gentlemen 🐒
 
Serikali iache kujidhalilisha. Mwachieni ndugu yetu akajumuike na familia yake. Hakuna mtu mwenye akili timamu asiyefahamu kama hii kesi ni ya kupikwa. Uonevu, dhulumua na uminywaji wa haki uliopitiliza; ndiyo chanzo kikuu cha chuki na uasi kushamiri ndani ya jamii.
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea leo Agosti 21, 2026, ambapo ambapo Majaji watatu wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam wataamua kama ana kesi ya kujibu au la.
Mmh,Tz hamna mahakama ya kumfunga huyo jamaa! Tena kwa case za uongo ndio kabisa....bibie una chuki na Lissu.
 
Back
Top Bottom