Pre GE2025 Lissu: Watumishi wa Umma hawatakiwi kusimamia Uchaguzi kwa vile ni Watumishi wa Rais

Pre GE2025 Lissu: Watumishi wa Umma hawatakiwi kusimamia Uchaguzi kwa vile ni Watumishi wa Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hivi ndivyo Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu alivyomuelisha Kada wa ccm Balile wa Jukwaa la Wahariri

Lissu amedai kwamba Watumishi wa Tanzania wanawajibika kwa Rais na wanaweza kutimuliwa kazi na Rais wakati wowote akitaka wala bila kufuata sheria za Utumishi wa umma , na mtumishi huyo hana pa kwenda kulalamika na ili asifutwe kazi itabidi apendelee chama cha Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa ccm

Screenshot_2025-03-02-21-43-34-1.png
Screenshot_2025-03-02-21-43-34-2.png
 
Tume yenyewe ya uchaguzi inalipwa na hazina,vyama vya upinzani ruzuku hutoka hazina,wabunge malipo hutoka hazina,rais kisheria anaweza lifuta bunge
 
Kwa mawazo yangu CDM wanatakiwa kuwa radical zaidi. Wanatakiwa kudai kuwa mtumishi wa umma hatakiwi kuwa kada na siasa zisiruhusiwe katika utumishi wa umma. Wakurugenzi wa Halmashauri, Ma DAS, Ma RAS, ma Katibu Wakuu, walimu wakuu, wakurugenzi wa uchaguzi n.k. wawe ni technocrats na wasiwajibike kiutendaji kwa wanasiasa. Ikiwa hivi hata Tume ya Uchaguzi itakuwa huru kweli.

Amandla...
 
hekaya za abunuhasi utawezaje kutenganisha utumishi na serikali alafu mtumishi wa umma ana haki ya kudai haki yake mahakamani hata kama rais akimtimua ndo maan kuna judicial review rejea kesi ya Komanya kitwana.
 
Watanzania wasio watumishi wa uma ni asilimia 98%
Unajaribu kumuelimisha mtu wa Team Mbowe ambaye anajifanya hajui Uchaguzi wetu unavyoendeshwa Kisa yanasemwa na Tundu Lissu.

Chaguzi zetu Wasimamizi ni Watendaji wa Kata, Walimu, Maafisa Ugani na Watumishi wengineo wa Halmashauri. Watendaji Hawa wanapokea amri za Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya na Maafisa Usalama wa Taifa kuwa waharibu Chaguzi Kwa faida ya Wagombea wa CCM.

Katika uhalisia wake tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika Uendeshaji na usimamizi wa chaguzi zetu. Tume inatakiwa kuwa na Watendaji katika Level ya Jimbo la Uchaguzi. Leo katika kila Halmashauri Kuna mtu anaitwa Afisa Uchaguzi mtu huyu Bado anawajibika Kwa Mkurugenzi ambaye ni muajiri wake. Pesa ya kumlipia Mshahara mtu huyu inayotoka Hazina ingelipa Afisa Uchaguzi ambaye ni Mfanyakazi wa Tume na akawajibika Kwa Mwenyekiti/Mkurugenzi wa Tume.

So kupata Watumishi sio tatizo na pesa za kuwalipa sio tatizo Kwa sababu hata Sasa wapo ila ni kuwahamisha tuu line of reporting isiende Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Bali Kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
 
hekaya za abunuhasi utawezaje kutenganisha utumishi na serikali alafu mtumishi wa umma ana haki ya kudai haki yake mahakamani hata kama rais akimtimua ndo maan kuna judicial review rejea kesi ya Komanya kitwana.
Hapo zamani watumishi wa umma hawakuwa wana siasa. Ndio maana walikuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi na upatikanaji wao ulitokana na watendaji waliomo serikalini. Ma Katibu Wakuu, ma Katibu Tawala, Wakurugenzi wa taasisi za seikali walikuwa ni watendaji ( technocrats) sio wana siasa. Wanasiasa walikuwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Katika mfumo huo pasingekuwa na haja ya mtumishi wa umma kwenda mahakamani kudai haki yake kwa sababu mabosi wake wangekuwa technocrats ambao mojawapo ya majukumu yao ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma hawaonewi na wana siasa. Lakini leo unaweza kuta kiongozi wa UVCCM akimfokea mganga mkuu bila hofu yeyote.

Amandla...
 
Hapo zamani watumishi wa umma hawakuwa wana siasa. Ndio maana walikuwa chini ya Katibu Kiongozi Mkuu na upatikanaji wao ulitokana na watendaji waliomo serikalini. Ma Katibu Wakuu, ma Katibu Tawala, Wakurugenzi wa taasisi za seikali walikuwa ni watendaji ( technocrats) sio wana siasa. Wanasiasa walikuwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Katika mfumo huo pasingekuwa na haja ya mtumishi wa umma kwenda mahakamani kudai haki yake kwa sababu mabosi wake wangekuwa technocrats ambao mojawapo ya majukumu yao ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma hawaonewi na wana siasa. Lakini leo unaweza kuta kiongozi wa UVCCM akimfokea mganga mkuu bila hofu yeyote.

ni kiongoz wa watumishi wa umma
kwani zamani huo uchaguzi ulikua hauibwi? Yale yale tu japo ni kweli Magufuli changed the system
 
Unajaribu kumuelimisha mtu wa Team Mbowe ambaye anajifanya hajui Uchaguzi wetu unavyoendeshwa Kisa yanasemwa na Tundu Lissu.

Chaguzi zetu Wasimamizi ni Watendaji wa Kata, Walimu, Maafisa Ugani na Watumishi wengineo wa Halmashauri. Watendaji Hawa wanapokea amri za Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya na Maafisa Usalama wa Taifa kuwa waharibu Chaguzi Kwa faida ya Wagombea wa CCM.

Katika uhalisia wake tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika Uendeshaji na usimamizi wa chaguzi zetu. Tume inatakiwa kuwa na Watendaji katika Level ya Jimbo la Uchaguzi. Leo katika kila Halmashauri Kuna mtu anaitwa Afisa Uchaguzi mtu huyu Bado anawajibika Kwa Mkurugenzi ambaye ni muajiri wake. Pesa ya kumlipia Mshahara mtu huyu inayotoka Hazina ingelipa Afisa Uchaguzi ambaye ni Mfanyakazi wa Tume na akawajibika Kwa Mwenyekiti/Mkurugenzi wa Tume.

So kupata Watumishi sio tatizo na pesa za kuwalipa sio tatizo Kwa sababu hata Sasa wapo ila ni kuwahamisha tuu line of reporting isiende Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Bali Kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na watendaji Wakuu wake wangepatikana vipi? Na nani angewateua? Hata Kenya makamishna wa Tume yao wanateuliwa na Rais lakini ni lazima wapitishwe na Bunge. Na ni lazima wasiwe wanachama wa chama cha siasa. Hawa ndio wanamchagua Mtendaji Mkuu. Sasa hapo kwetu ambao Bunge ni asilimia 90 chama kimoja huo uhuru utatokea wapi? Kinacho takiwa ni kuondoa kabisa siasa katika utendaji wa umma.

Amandla....
 
Itateuliwa na nani? Itaajiriwa na nani? Italipwa na nani? Itatoa wapi wasimamizi katika vituo? Nini kitaifanya ikubalike kuwa ni Tume Huru?

Amandla...
Muundo wa Tume uwe ni Taasisi HURU bila ya kuingiliwa uwe kama Kenya.
 
Ni muhimu kuainisha nini kitaifanya iwe huru kama hiyo ya Kenya. Ama sivyo utaambiwa mbona tayari tuna Tume Huru ya Uchaguzi?

Aidha, chombo kinachohakikisha kuwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ni Huru ni Mahakama Kuu huru. Bila kuwa na Mahakama iliyokuwa Huru hamtakuwa na Tume iliyokuwa Huru.

Iliyowatilia kifua wakina Halima ni Mahakama. Kama ingesimamia haki shauri lao lingeisha mapema kwa kutoa uamuzi wa uhalali wao haraka sana.

Amandla...
 
Back
Top Bottom