Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ndio maana kuna No Reform No ElectionTume yenyewe ya uchaguzi inalipwa na hazina,vyama vya upinzani ruzuku hutoka hazina,wabunge malipo hutoka hazina,rais kisheria anaweza lifuta bunge
Hakuna asiyeguswa na rais,kuuondoa uchaguzi toka serikali kuu ni hekaya za abunuwasiNdio maana kuna No Reform No Election
Hajui nani asimamie uchaguzi,anapinga tu wanaosimamia sasaAmependekeza angetaka nani asiamie uchaguzi?
Amandla...
Tume HURU ya Uchaguzi.Amependekeza angetaka nani asimamie uchaguzi?
Amandla...
Itateuliwa na nani? Itaajiriwa na nani? Italipwa na nani? Itatoa wapi wasimamizi katika vituo? Nini kitaifanya ikubalike kuwa ni Tume Huru?Tume HURU ya Uchaguzi.
Watanzania wasio watumishi wa uma ni asilimia 98%Amependekeza angetaka nani asimamie uchaguzi?
Amandla...
Unajaribu kumuelimisha mtu wa Team Mbowe ambaye anajifanya hajui Uchaguzi wetu unavyoendeshwa Kisa yanasemwa na Tundu Lissu.Watanzania wasio watumishi wa uma ni asilimia 98%
Hapo zamani watumishi wa umma hawakuwa wana siasa. Ndio maana walikuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi na upatikanaji wao ulitokana na watendaji waliomo serikalini. Ma Katibu Wakuu, ma Katibu Tawala, Wakurugenzi wa taasisi za seikali walikuwa ni watendaji ( technocrats) sio wana siasa. Wanasiasa walikuwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Katika mfumo huo pasingekuwa na haja ya mtumishi wa umma kwenda mahakamani kudai haki yake kwa sababu mabosi wake wangekuwa technocrats ambao mojawapo ya majukumu yao ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma hawaonewi na wana siasa. Lakini leo unaweza kuta kiongozi wa UVCCM akimfokea mganga mkuu bila hofu yeyote.hekaya za abunuhasi utawezaje kutenganisha utumishi na serikali alafu mtumishi wa umma ana haki ya kudai haki yake mahakamani hata kama rais akimtimua ndo maan kuna judicial review rejea kesi ya Komanya kitwana.
kwani zamani huo uchaguzi ulikua hauibwi? Yale yale tu japo ni kweli Magufuli changed the systemHapo zamani watumishi wa umma hawakuwa wana siasa. Ndio maana walikuwa chini ya Katibu Kiongozi Mkuu na upatikanaji wao ulitokana na watendaji waliomo serikalini. Ma Katibu Wakuu, ma Katibu Tawala, Wakurugenzi wa taasisi za seikali walikuwa ni watendaji ( technocrats) sio wana siasa. Wanasiasa walikuwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Katika mfumo huo pasingekuwa na haja ya mtumishi wa umma kwenda mahakamani kudai haki yake kwa sababu mabosi wake wangekuwa technocrats ambao mojawapo ya majukumu yao ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma hawaonewi na wana siasa. Lakini leo unaweza kuta kiongozi wa UVCCM akimfokea mganga mkuu bila hofu yeyote.
ni kiongoz wa watumishi wa umma
Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na watendaji Wakuu wake wangepatikana vipi? Na nani angewateua? Hata Kenya makamishna wa Tume yao wanateuliwa na Rais lakini ni lazima wapitishwe na Bunge. Na ni lazima wasiwe wanachama wa chama cha siasa. Hawa ndio wanamchagua Mtendaji Mkuu. Sasa hapo kwetu ambao Bunge ni asilimia 90 chama kimoja huo uhuru utatokea wapi? Kinacho takiwa ni kuondoa kabisa siasa katika utendaji wa umma.Unajaribu kumuelimisha mtu wa Team Mbowe ambaye anajifanya hajui Uchaguzi wetu unavyoendeshwa Kisa yanasemwa na Tundu Lissu.
Chaguzi zetu Wasimamizi ni Watendaji wa Kata, Walimu, Maafisa Ugani na Watumishi wengineo wa Halmashauri. Watendaji Hawa wanapokea amri za Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya na Maafisa Usalama wa Taifa kuwa waharibu Chaguzi Kwa faida ya Wagombea wa CCM.
Katika uhalisia wake tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika Uendeshaji na usimamizi wa chaguzi zetu. Tume inatakiwa kuwa na Watendaji katika Level ya Jimbo la Uchaguzi. Leo katika kila Halmashauri Kuna mtu anaitwa Afisa Uchaguzi mtu huyu Bado anawajibika Kwa Mkurugenzi ambaye ni muajiri wake. Pesa ya kumlipia Mshahara mtu huyu inayotoka Hazina ingelipa Afisa Uchaguzi ambaye ni Mfanyakazi wa Tume na akawajibika Kwa Mwenyekiti/Mkurugenzi wa Tume.
So kupata Watumishi sio tatizo na pesa za kuwalipa sio tatizo Kwa sababu hata Sasa wapo ila ni kuwahamisha tuu line of reporting isiende Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Bali Kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
Muundo wa Tume uwe ni Taasisi HURU bila ya kuingiliwa uwe kama Kenya.Itateuliwa na nani? Itaajiriwa na nani? Italipwa na nani? Itatoa wapi wasimamizi katika vituo? Nini kitaifanya ikubalike kuwa ni Tume Huru?
Amandla...
Usisahau pia kisheria Bunge linaweza kumfuta rais kama akivunja Katiba...rais kisheria anaweza lifuta bunge